Bahari ni kiboko ya usafiri wa wachawi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Kuna njia kuu tatu zinazotumiwa na mwanadamu kwa ajili ya usafiri yani kutoa sehemu moja mpaka nyingine nazo ni maji anga na ardhi .

Lakini kwa mchawi ni mbili anga na ardhi , majini wengi wanaikwepa na kuiogopa hasa na wale wachache wanaitumia ni mpaka wapate kibali cha ufalme wa majini .

Mchawi atatumia ungo-hii ni advanced tech ya usafiri na inajumuisha mambo mengi ila ni salama na ni ya haraka zaidi kama ulivyo usafiri wa ndege za kawaida pia ni usafiri wa masafa marefu
Usafiri mwingine ni wa ardhini huu hauna hatari nyingi na gharama pia ni ndogo , chombo chake kwa sehemu kubwa ni Mnyama fisi, tatizo moja la huu usafiri ni inland routes tena za masafa mafupi na wachawi daraja la chini .

Lakini ni mara ngapi umeshasikia usafiri wa wachawi baharini? Ni aghalabu kusikia hii kitu hata kutumia mazao bahari kama makombe na samaki kwenye shughuli za kiganga ni mara chache mno.

Sababu moja kuu ni kwamba maji ndio yanayotajwa la dunia robo tatu ya uso wa dunia ni maji na hata mwili wako pia, kwahiyo ufalme wa maji kwa maana ya majini ndio ufalme wa giza wenye nguvu zaidi na sophisticated zaidi kiasi kwamba ufalme wa giza wa ardhini unapwaya na kugwaya kwa ufalme wa maji .

Ndio maana huwezi kusikia hata siku moja eti mchawi kaanguka baharini au kuna chombo kinachotumiwa na wachawi kusafiria baharini.
 
Sasa uchawi wao kama ni advance wanaufanyia wapi au kwa ajili ya kuharibu nini
 
Ule unaogopeka kwakuwa una nguvu sana na mara nyingi madhara yake hayana matibabu
Hiyo kitu si mchezo kuna mzee wangu mmoja alikuwa akifanya kazi penye boat miaka hiyo ulikuwa ukipiga nae story unaweza usilale usiku kuna vitu vingine mtu akikwambia unaweza sema kamba.Kuna hii moja ya kuwa kuna majoka makubwa huwa yapo majini sasa kuna waqt hupazwa(yaani hunyanyuliwa juu na kupotea mawinguni)na anasema mkiwa hapo ufukweni mnasikia kitu kama minyororo inavuta kitu kizito kisha panakuwa na ka wingu kazito.
Je unaweza kulizungumzia hili?
 
Naskiaga kuna mbunge mmoja mpya alikuwa mfanyabiashara wa supermarket naye alikuwa mfuasi wa kuzama huko. Majin ?????
Ambaye amefilisika sasa? toka kanda ya ziwa? Haya mambo ni vigumu kuyajua hasa kwakuwa ni siri ya mtu na mojawapo ya viapo au maagano ni kutosimulia chochote. ..watu watabaki tu na speculations kutokana na mienendo yako
 
Mshana Jr hayo mambo unayasoma kwenye vitabu au mungu kakujalia kuyapata ndotoni????
 
Ambaye amefilisika sasa? toka kanda ya ziwa? Haya mambo ni vigumu kuyajua hasa kwakuwa ni siri ya mtu na mojawapo ya viapo au maagano ni kutosimulia chochote. ..watu watabaki tu na speculations kutokana na mienendo yako
Hahahahah ndio we ni kiboko unajua hiz mambo
OK bas em nijuze kwann amefilisika????
 
Hiyo kitu si mchezo kuna mzee wangu mmoja alikuwa akifanya kazi penye boat miaka hiyo ulikuwa ukipiga nae story unaweza usilale usiku kuna vitu vingine mtu akikwambia unaweza sema kamba.Kuna hii moja ya kuwa kuna majoka makubwa huwa yapo majini sasa kuna waqt hupazwa(yaani hunyanyuliwa juu na kupotea mawinguni)na anasema mkiwa hapo ufukweni mnasikia kitu kama minyororo inavuta kitu kizito kisha panakuwa na kawa wingu zito.
Je unaweza kulizungumzia hili?
Unaposoma habari za maajabu ya bahari kuna mambo mengi mno ya kutisha ambayo hayajulikani na wengi na hayana tafsiri kamili juu ya uhalisia wake na malengo yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom