Babu wa loliondo atuombee kwa mwenyezi mungu kuhusu ndoa

Safina

JF-Expert Member
Jun 18, 2009
497
64
Habari za mchana wana jf wenzangu!!!!!!

Wengi tumeamini katika tiba anazozitoa BABU!!! Saratani, ukimwi, kisukari, shinikizo la damu.

Nimekaa hapa ofisini nimewaza hivi, kuna hili tatizo kubwa na sugu namaanisha tatizo la ndoa/mapenzi, mwanzoni watu wanakuwa na mapenzi moto, moto, kidogo, kidogo mkishazoeana penzi linaanza kuchuja na mwisho kuisha kabisa. Jamani tupelekeni maombi kwa babu aongee na Mwenyezi Mungu, kama alivyompa huu upako wa kutibu haya magonjwa mengine, apate basi upako wa kutibu na hili gonjwa sugu la ndoa/mapenzi.

Katika mazingira tunayoishi sasa hivi, kama sio mama yako mzazi kukusimulia kuhusu baba, basi dada, kama sio dada, kaka, shangazi, mjomba, wifi, jirani, bosi, secretary, yaani hakuna amani kabisa katika hiki kitu kinachoitwa mapenzi kwa sasa. Mimi nikifanikisha kwenda kwa babu na katika sala zangu kuanzia sasa hivi nitamwomba Mwenyezi Mungu amwonyeshe babu mzizi mwingine maalumu kwa ajili ya hili gonjwa na gonjwa hili akinywa mama na baba anakuwa ameponyweshwa na akinywa baba basi na mama atakuwa ameponyeshwa na hii iwe maalumu kwa wanandoa tu. Nadhani sijajichosha, wala kuwachosha.
 
Babu sio Nabii ni mtu tu kama sisi, tusifilisike kiimani kiasi hiki ni bora matumaini yetu tukiyaweka kwa Mungu Mwenyezi. Babu ana mwisho siku yake ikifika naye atakufa tu! Hana ujanja wa kupambana na mauti lakini Mungu wetu hafi, haumwi yupo MILELE na MILELE.
 
Matumaini yetu tumeyaweka kwa Mungu na ndo maana nimesema atuombee tupewe kikombe kingine, sikusema yeye ni nabii wala yeye ni Mungu.
 
mhh!! Safina unapenda kuombewaaaaaa???? si ujiombee mwenyewe????
 
Habari za mchana wana jf wenzangu!!!!!!

Wengi tumeamini katika tiba anazozitoa BABU!!! Saratani, ukimwi, kisukari, shinikizo la damu.

Nimekaa hapa ofisini nimewaza hivi, kuna hili tatizo kubwa na sugu namaanisha tatizo la ndoa/mapenzi, mwanzoni watu wanakuwa na mapenzi moto, moto, kidogo, kidogo mkishazoeana penzi linaanza kuchuja na mwisho kuisha kabisa. Jamani tupelekeni maombi kwa babu aongee na Mwenyezi Mungu, kama alivyompa huu upako wa kutibu haya magonjwa mengine, apate basi upako wa kutibu na hili gonjwa sugu la ndoa/mapenzi.

Katika mazingira tunayoishi sasa hivi, kama sio mama yako mzazi kukusimulia kuhusu baba, basi dada, kama sio dada, kaka, shangazi, mjomba, wifi, jirani, bosi, secretary, yaani hakuna amani kabisa katika hiki kitu kinachoitwa mapenzi kwa sasa. Mimi nikifanikisha kwenda kwa babu na katika sala zangu kuanzia sasa hivi nitamwomba Mwenyezi Mungu amwonyeshe babu mzizi mwingine maalumu kwa ajili ya hili gonjwa na gonjwa hili akinywa mama na baba anakuwa ameponyweshwa na akinywa baba basi na mama atakuwa ameponyeshwa na hii iwe maalumu kwa wanandoa tu. Nadhani sijajichosha, wala kuwachosha.

Hilo kweli ila nawe kwanini ukae ofisini ukiwaza juu ya babu tu wakati huo muda ni wa mwajiri wako okey hata wewe unaweza kuomba ili Mungu akuonyeshe ingawa babu yeye hakuomba apewe hiyo dawa.

Tusimjaribu Mungu ......labda kwa sadaka na zaka tu.
 
Mi nafikiri kila mtu na matatizo yake kikombe kimoja tu kinaponya kuna mdada mmoja kaenda kunywa apate mume kashuhudia, kanywa mwaka jana sasa hivi ana mchumba keshatoa mahari. mimi nikipata tu nafasi na mungu akipenda lazima niende loliondo sitaki kupitwa maana hawakawii kumpoteza watu wa madawa ya kizungu
 
Mwisho tutaomba Babu aonyeshwe mizizi ya utajiri na kufaulu bila kusoma
 
Back
Top Bottom