Usiwaambie watu mambo ya ndani ya ndoa yako

Restitius Respicius

New Member
Jul 6, 2020
1
9
1. Usimwambie mtu yeyote jinsi mwenzi wako alivyo dhaifu. Mtu anaweza kutumia hilo dhidi yako/ao.

2. Usiwaambie watu jinsi mnavyogombana na mwenzi wako, wawaone mmekamilika kutoka nje wakati mnatatua mambo ndani.

3. Hata rafiki wa karibu usimwambie pesa ngapi unapata pesa kiasi hani kutoka kwa mumeo, ikiwa watakuuliza, waambie anatoa zaidi ya ulivyotarajia.

4. Wanaume, msiwaambie marafiki zenu jinsi mkeo anavyokuwa mzuri kitandani, hiyo ni siri kati yako na mkeo.

5. Kamwe usimwambie mama yako jinsi mwenzi wako anavyoenenda katika ndoa, hutapenda matokeo ikiwa ni mama mkwe mwenye wivu.

6. Wanawake, rafiki anaweza kuwa anamtamani mumeo kwa hiyo usimwambie chochote kuhusu mumeo wanaweza kuvutiwa nae zaidi yako na ukamkosa.

7. Hata kama ni kiongozi wa dini hafai kujua mara ngapi mnagombana na mumeo, wengi wao watatumia kama mahubiri. Zungumza na Mungu pekee.

8. Usimwambie watoto kwamba baba/mama yao ni mtu mbaya. Inaweza kuwafanya wawachukie.

9. Usiwaambie watu kuhusu makosa ya zamani ya mwenzi wako, ni hatari sana kwa ndoa yako.

10. Usiwaambie watu wajaribu kumshawishi mwenzi wako ili kuthibitisha uaminifu wao. Wanaweza kumshinda kwa mapenzi. Kuzuia ni bora kuliko kutibu.

Darasa limekwisha
 
Kama mume / mke hatakuwa mwepesi kujadili mambo yake na mwenza wake, yatatoka nje tu.

Lazima kuwe na breather kwenye ndoa, ikikosekana, itapumulia nje tu hakuna namna.
 
Kuna wanawake ni wapuuzi sana, hupenda kusimulia udhaifu wa mume wake kupiga shoo kwa wanawake wenzake au michepuko yao. Wanasimulia hadi ukubwa na udogo wa kitu.
Kuna mke wa mtu ni rafiki yangu yan hayo yote huwa ananiambia sijui ananiamini vipi
 
Yaani unakuta mwanaume mzima akigombana na mkewe anachukua simu na kuanza kuongea na Dada zake au mama yake badala yakukaa chini nanmkewe, je hao waitwe misukule part 2 au waitwaje nahao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom