Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,482
- 40,001
Duh.. vyanzo vyangu mbadala vya habari vinadokeza kuwa yule Mzee aliyezungumza kwenye ITV kwa uchungu mkubwa na kutaka CCM ife kabla yake na kushangiliwa sana amegongwa na gari na pamoja na jitihada za kumuokoa amefariki dunia usiku huu saa saba. Nimeweza kuzungumza na vyanzo vya karibu vya familia na vimethibitisha habari hii.
Ajali ilitokea juzi (Alhamisi) maeneo ya Ubungo (sina uhakika) na gari lililohusika na ajali hiyo linadaiwa kukamatwa lakini bado taarifa hizi za gari na dereva wake sijawa na uhakika nazo sana. Ila ni kweli mzee Mahimbo amefariki dunia. Tarehe 30 Julai, mzee huyo alizungumza kwa ukali sana na kuonekana kwa namna fulani "kukashfu" serikali na hasa alipodai kuwa yeye hatokufa hadi CCM ife. Siku mbili baadaye amekutwa na ajali ambayo imechukua maisha yake.
Nina details nyingine ambazo kwa wakati huu naziweka pembeni kwa makusudi - mwenye uwezo wa kujumlisha anaweza kuhisi.
UPDATED 1:Mwili wa Marehemu umeondolewa toka hospitali ya Muhimbili na kupelekwa hospitali ya Jeshi la Lugalo ili kufanyiwa uchunguzi. Kwa mujibu wa chanzo changu toka ndani ya ofisi za hospitali hiyo "inavoonekana kuna kamchezo kidogo kwn pale muhimbili hakupatiwa huduma yoyote si drip wala panadol"
UPDATED 2: Mazishi yanatarajiwa kuwa Jumatatu hii.
UPDATED 3: Inadaiwa kuwa Polisi wamefanikiwa kulipata gari lililohusika na ajali hii japo mmiliki wake hajulikani na dereva hajajitokeza bado (isia zangu ni kuwa - reasonably - litakuwa gari la wizi. Nasubiri kusahihiswa hisia izo.