Babu aliyetaka CCM ife kabla yake na kushangiliwa kwenye TV agongwa na gari na kufariki...

Duh.. vyanzo vyangu mbadala vya habari vinadokeza kuwa yule Mzee aliyezungumza kwenye ITV kwa uchungu mkubwa na kutaka CCM ife kabla yake na kushangiliwa sana amegongwa na gari na pamoja na jitihada za kumuokoa amefariki dunia usiku huu saa saba. Nimeweza kuzungumza na vyanzo vya karibu vya familia na vimethibitisha habari hii.

Ajali ilitokea juzi (Alhamisi) maeneo ya Ubungo (sina uhakika) na gari lililohusika na ajali hiyo linadaiwa kukamatwa lakini bado taarifa hizi za gari na dereva wake sijawa na uhakika nazo sana. Ila ni kweli mzee Mahimbo amefariki dunia. Tarehe 30 Julai, mzee huyo alizungumza kwa ukali sana na kuonekana kwa namna fulani "kukashfu" serikali na hasa alipodai kuwa yeye hatokufa hadi CCM ife. Siku mbili baadaye amekutwa na ajali ambayo imechukua maisha yake.

Nina details nyingine ambazo kwa wakati huu naziweka pembeni kwa makusudi - mwenye uwezo wa kujumlisha anaweza kuhisi.

Mkuu, wacha kuwajengea watu hisia ambazo sizani kama zipo!!! Hata kama CCM na serikali yake ni Mafia namna gani; sizani kama wanaweza kupoteza muda na mtu mmoja kama huyo ambae hana influence yoyote.
 
Nafuatilia nini kimetokea, siamini, ni kawaida ya siasa za kikomunisti kutaka kupingana na ukweli. Inawezekana walishindwa kuelewa tamthilia za mzee wa watu wakafikiri akitoa roho maneno yake yatakuwa yamefutika. Mungu ilaze roho ya marehemu.............sisi waja wako bado tunapigania haki yetu ya msingi ya kula milo mitatu kwa siku.
 
Ccm majuha kweli. Sasa kwa kumtanguliza ndio hawatapasuka? Tena wamejiharakashia kama walivyomharakisha mahimbo
 
MM, this is just an amaizing coincidence of an isolated event. Sio kazi ya 'the oparatives', now days, they don't oparate that way!.
RIP Mzee Mahimbo.
 
Mkuu, wacha kuwajengea watu hisia ambazo sizani kama zipo!!! Hata kama CCM na serikali yake ni Mafia namna gani; sizani kama wanaweza kupoteza muda na mtu mmoja kama huyo ambae hana influence yoyote.
Kumbe wewe 'unazani,' huna uhakika...
 
Back
Top Bottom