Babu aliyetaka CCM ife kabla yake na kushangiliwa kwenye TV agongwa na gari na kufariki...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Duh.. vyanzo vyangu mbadala vya habari vinadokeza kuwa yule Mzee aliyezungumza kwenye ITV kwa uchungu mkubwa na kutaka CCM ife kabla yake na kushangiliwa sana amegongwa na gari na pamoja na jitihada za kumuokoa amefariki dunia usiku huu saa saba. Nimeweza kuzungumza na vyanzo vya karibu vya familia na vimethibitisha habari hii.

Ajali ilitokea juzi (Alhamisi) maeneo ya Ubungo (sina uhakika) na gari lililohusika na ajali hiyo linadaiwa kukamatwa lakini bado taarifa hizi za gari na dereva wake sijawa na uhakika nazo sana. Ila ni kweli mzee Mahimbo amefariki dunia. Tarehe 30 Julai, mzee huyo alizungumza kwa ukali sana na kuonekana kwa namna fulani "kukashfu" serikali na hasa alipodai kuwa yeye hatokufa hadi CCM ife. Siku mbili baadaye amekutwa na ajali ambayo imechukua maisha yake.

Nina details nyingine ambazo kwa wakati huu naziweka pembeni kwa makusudi - mwenye uwezo wa kujumlisha anaweza kuhisi.

UPDATED 1:Mwili wa Marehemu umeondolewa toka hospitali ya Muhimbili na kupelekwa hospitali ya Jeshi la Lugalo ili kufanyiwa uchunguzi. Kwa mujibu wa chanzo changu toka ndani ya ofisi za hospitali hiyo "inavoonekana kuna kamchezo kidogo kwn pale muhimbili hakupatiwa huduma yoyote si drip wala panadol"

UPDATED 2: Mazishi yanatarajiwa kuwa Jumatatu hii.

UPDATED 3:
Inadaiwa kuwa Polisi wamefanikiwa kulipata gari lililohusika na ajali hii japo mmiliki wake hajulikani na dereva hajajitokeza bado (isia zangu ni kuwa - reasonably - litakuwa gari la wizi. Nasubiri kusahihiswa hisia izo.
 
Duh.. vyanzo vyangu mbadala vya habari vinadokeza kuwa yule Mzee aliyezungumza kwenye TV kwa uchungu mkubwa na kutaka CCM ife kabla yake na kushangiliwa sana amegongwa na gari na pamoja na jitihada za kumuokoa amefariki dunia usiku huu saa saba. Nimeweza kuzungumza na vyanzo vya karibu vya familia na vimethibitisha habari hii.

Ajali ilitokea juzi (Alhamisi) maeneo ya Ubungo (sina uhakika) na gari lililohusika na ajali hiyo linadaiwa kukamatwa lakini bado taarifa hizi za gari na dereva wake sijawa na uhakika nazo sana. Ila ni kweli mzee Mahimbo amefariki dunia. Tarehe 30 Julai, mzee huyo alizungumza kwa ukali sana na kuonekana kwa namna fulani "kukashfu" serikali na hasa alipodai kuwa yeye hatokufa hadi CCM ife. Siku mbili baadaye amekutwa na ajali ambayo imechukua maisha yake.

Nina details nyingine ambazo kwa wakati huu naziweka pembeni kwa makusudi - mwenye uwezo wa kujumlisha anaweza kuhisi.

@mwanakijiji, vp ile taasisi haikushiriki kweli? matani tu mjumbe dunia ina mambo
 
Hoja iko wapi hapo? Kwamba CCM ni wachawi? Mods mnatoa uhuru uliopitiliza kwa kuruhusu imani hasi kama hizi kupenya kwenye hii site. Hili jukwaa limefanyiwa marekebisho lakini hata sioni faida yake. Sasa hii ilete hisia kwamba watu wote waliokufa wiki iliyopita, mwezi uliopita au mwaka uliopita wamerogwa na CCM?
 
Mbona unaishuku CCM? Ni wewe ndiye uliyesema "amekufa kifo cha kawaida"... well kwanini ulifikiria hivyo hadi ukasema kwani kuna kifo kisicho cha kawaida?
 
Mbona unaishuku CCM? Ni wewe ndiye uliyesema 'amekufa kifo cha kawaida'... well kwanini ulifikiria hivyo hadi ukasema kwani kuna kifo kisicho cha kawaida?
Na wewe ni kitu gani kilichokupelekea kuripoti hicho kifo hapa? Kuna wazee wangapi wamekufa wiki hii ambao hatuna habari zao?
 
Back
Top Bottom