Baba mdogo wa mume wangu amekasirika mimi kumkiss mume wangu

Habari za Leo Waungwana!

Nyumbani kwetu tumejiwa na mgeni ambae ni Baba mdogo wa mume wangu. Atakuwa kwetu kama 15 days. Amekuja medical na mkewe na watoto wa3. Tangu wamekuja leo ni siku ya 4.

Cha kushangaza leo asubuhi wakati watoto wanakwenda school wamekuja kutuaga which is normal. Huwa wanatukumbatia then wanaondoka na sisi pia me and my Hubby we Kiss and hug kila mtu anaingia kwenye gari yake safari ya kazini inaanza.

Huyu Mzee kuona leo namuhug mume wangu ili niingie kwenye gari katoka ndani mbio kamuita Hubby. Sasa sikuweza kuondoka ikabidi nisiingie kwenye gari nimsalimie, hakutaka hata kujibu salamu. Anagomba anamwambia my Hubby malezi gani haya unayolea watoto wako na mkeo? Hamuoni aibu mnakumbatiana, mambo ya kufanya chumbani mnafanya hapa, tabia gani hii mnatuonyesha nini?

Tangu nimeingia hapa naona tuu asubuhi mwaaaaaaaaaa! jioni mwaaaaaaaaaaa! Kama hamtaki wageni nyumbani kwenu semeni bwana msitunyanyase. Mimi sikuwa na la kusema nilirudi tena nikajikuta namhug tena my hubby nikamwambia siku njema tutaongea baadae.

Mzee kasema nataka kuongea na wewe mama mwenye nyumba jioni.

Ikumbukwe huyu baba ana wanawe na hawaongei wapo mji huu niliko mimi, watoto wake wa kike 38 na mwengine 41 na 28 ndio alokuja nao. Wote wa kike hawajaolewa kwa midomo yao. Wako kwangu lakini wanamwambia dada apike wanachotaka wao, wao hawawezi kula chakula cha kuchemsha kama wako Hospital.

Sasa najiuliza huyu mzee anataka nimjibu nini? Nimehisi nimnyamazie wakati anaongea sababu its just a matter of 11days anaondoka zake au atahisi nikinyamaza ntakua nimemdharau?

Waungwana naomba busara zenu as sio kama namchukia ila sipendi mtu anipangie sheria nyumbani kwangu. Ingekua nimevua nguo sawa lakini it was just a normal hug and kiss to my hubby na hata akiwepo nani tumeshazowea
kokote kule hata tuwe tumegombana as long as mmoja wetu ametoka akirudi Kiss and Hug ni must.

Weka picha
 
Mmezidi kujifanya wazungu bila kujali kuna wageni.Haya mambo mmeyaiga tuu halafu mwataka kila mtu aone.Pia wewe mama huna adabu yaani mmeo anagombezwa kwa suala hilo halafu unalirudia tena hapo hapo.Umemsababishia matatizo mumeo na usishangae akakubadirikia badaye

Sio mbele ya wageni tu mkuu hata mbele ya watoto. ujinga gn huu et uzungu ndo maana watoto wengi wameharibika, mambo ya chumbani yanawekwa hadharani na ya hadharani ndo yanafichwa chumbani!! God have mercy with us
 
Tueshimiane,niko kwangu sijakwenda nuymbani kwake au kwa mtu,maisha yangu na familia yangu yeye mgeni wakupita njia asinipangie,anakwa wanawe alowazaa kumemshinda kwa mdomo wake ...

we boya umezidi kuigaiga ujinga. unaiharibu familia yako kwa mikono yako mwenyewe.

endelea hvyo hvyo kwa kuwa umemgeuza mmeo ndondocha
 
Ishi kama jamii nyingine inavoishi ukileta uzungu mbele ya mwafrica lazma uchukiwe hata kitendo cha kukurupuka unaleta uzi hapa inaonyesha hauko sawa!!!
 
Ishi kama jamii nyingine inavoishi ukileta uzungu mbele ya mwafrica lazma uchukiwe hata kitendo cha kukurupuka unaleta uzi hapa inaonyesha hauko sawa!!!
Hapo ndio mwisho wa ushauri wako eeh? haya Ahsante pia umejaribu si haba..
 
Nimegundua ni stori ya kutunga.Ila kama ni kweli hongera mama kujaliwa kama ulivyotaka iwe maishani mwako.Usiseme yote bakishia na kesho.
Sioni sababau ya kutunga maneno na sio Hulka yangu,mwenyezi mungu akujaalie na wewe kama alivyowajaalia wengine...
 
MKWEO YUKO SAHIHI HIVI HUONI AIBU KUKUMBATIANA MBELE YA MKWEO? HIVI BABA YAKO MZAZI AKIJA UTAKUMBATIWA MBELE YAKE MUWE NA STAHA JAMANI UZUNGU MNAOIGA UNAVUNJA MAADILI NA SIYO ETI KWAKUWA UKO KWAKO BASI UKOSE ADABU NA HASA IKIZINGATIWA WAGENI WAKO WAMEFIKA KWAKO KWA SHIDA BASI NDIYO UWANYANYASE KWA KUFANYA MAMBO YA AIBU MBELE ZAO KWANI UKIJIZUIA KWA MUDA WA HIZO WIKI MBILI UTAKUFA? HATA MAADILI YA DINI ZOTE HAYAKUPI UHURU HUO UNACHOKIFANYA NI ULIMBUKENI WA KUIGA MAMBO YA KIZUNGU WAKATI HUKU NI AFRICA KILA JAMBO LINA MAHALI PAKE MAMA SIYO KILA MAHALI UNAJIANIKA HAPANA MUOMBE MSAMAHA MKWEO MMEKOSA KWA MUNGU NA MBELE YAKE MKWEO HATA MUMEO NAYE NI LIMBUKENI KAMWE SIWEZI KUKUMBATIANA NA MKE WANGU MBELE YA WAZAZI WA PANDE ZOTE MBILI NI UKOSEFU WA ADABU.
Kama baya kwako wewe kwetu sawa tu,na kama unadhani tunaiga wazungu siwezi kukubadilisha mawazo yako,yeye wanawe wa kike wana vaa mini ndani ya nyumba na hasemi kwa hiyo kiss ndio aliona kitu kikubwa sana? kunyanyasa yeye ndio anae taka niwanynyase wafanya kazi wangu kwakutaka kuleta rules zake ambazo hazitokubalika,anyway usijichoshe sana mwache mzee ametuliza anamaliza sikuzake wala usijali...
 
Weeee..siku hizi watoto wana ngozi laini fimbo 2 tu ngozi inachanika...polisi jamii wanarara mbere na wewe...Ila pole sana wageni ni baraka lkn wengine wanaleta kisirani. Muombe Mungu akupe hekima ya kuishi nao...
lol..shukran...
 
Tena nikipata mgeni, ndio naongeza mapenzi kwa mume wangu, this is my life. Na hata mama mkwe na baba mkwe wawepo, mlango sifungagi kama kawaida yangu, tunakula mzigo hivo hivo, kwani mapenzi yao? si bora wawe biz na mapenzi yao kuliko kufuatilia mapenzi ya wengine.

Basi kama yeye ni baba bora, angewalea watoto wake vizuri ili wadumu kwenye ndoa zao,

Mwambie kama hapendi basi hasiangalie, akiona munafanya hivo ageuze shingo, au afumbe macho
Kwani unadhani inamkera basiii? alikua anatafuta sababau tuuu,amesha zowea manake no changes so far na life goes on na amepoa...
 
MKUU.

ACHA KUENDEKEZA UMAGHARIBI SANA-
KAMA KUNA BABA/YENU KUWENI NA ADABU!

HALAFU HIYO KUWASEMA NDUGU WENGINE WA MIAKA 38, 41 NA 28 AMBAO HAWAJAOLEWA INAHUSIANA NINI NA MALALAMIKO DHIDI YA BABA MKWE WAKO MDOGO???

UWASILISHAJI WAKO UNAASHIRIA KABISA UNACHUKIA UWEPO WAO
KIASI CHA KUHESABIA HADI HIZO SIKU ZILIZOSALIA KWA USONGO.

JE,
ANGEKUWA MZAZI WAKO ND'O ANAKEMEA HIVYO NA KAJA KWA AJILI YA MATIBABU KWA MIEZI MIWILI INGEKUWAJE???
------------------

TAMBUA:
HUYO BABA HAKUPANGII NAMNA YA KUISHI NYUMBANI KWAKO,
ILA KWA TAMADUNI ZILIZOWAKUZA WAZAZI WETU
KUKUMBATIANA NA MABUSU HADHARANI SIO STARA.

---------
VINGINEVYO
WEKA PICHA NIKUSHAURI FASTA HAPA.

ANGALIZO:
MIMI SIO WA MCHEZO MCHEZO,
NA HUWA SIJARIBIWI KABISAAA!!!

Tamaduni sio kwa style alio ileta yeye,kwanza kabla hujaanza kunyoosha watoto wawemzio unaangalia wako kama wako sawa,alikuja kumleta mkewe matibabu sio anaeumwa,wangalie la mgonjwa sio mengine...
 
Sioni sababau ya kutunga maneno na sio Hulka yangu,mwenyezi mungu akujaalie na wewe kama alivyowajaalia wengine...

Mimi hata akinijalia itakuwa ni kwa makusudi maalumu.Kwamba niwe kama bomba tu la kupitishia "baraka" kama zenu kwenda alikokusudia.Hakuna kitu tunapata au tunatoa kwa nguvu zetu wenyewe.Mpende huyo mtesi wako kuliko marafiki zako.Adui hutokea kuwa rafiki wa kweli kweli na rafiki ndio huweza kuwa maadui wa kweli kweli.Ukijua namna ya kumu-handle huyo mtu(mkwe) hakika atatokea kuwa mkwe mzuri na rafiki mzuri.Nyumba hujengwa na mwanamke tena kwa ulimi wake na sio vitambaa vya makochi au mageti ya kuingilia magari.
 
Hana mda anakwenda zake siku zake zimeshawadia...
 
Kama baya kwako wewe kwetu sawa tu,na kama unadhani tunaiga wazungu siwezi kukubadilisha mawazo yako,yeye wanawe wa kike wana vaa mini ndani ya nyumba na hasemi kwa hiyo kiss ndio aliona kitu kikubwa sana? kunyanyasa yeye ndio anae taka niwanynyase wafanya kazi wangu kwakutaka kuleta rules zake ambazo hazitokubalika,anyway usijichoshe sana mwache mzee ametuliza anamaliza sikuzake wala usijali...

Kumbe ulikuja kutujulisha lifestyle ya nyumbani kwako na siyo kutaka ushauri wakati una majibu yako endelea hivyohivyo kama hukufundwa na wazazi wako JF siyo mahali pake.
 
Kumbe ulikuja kutujulisha lifestyle ya nyumbani kwako na siyo kutaka ushauri wakati una majibu yako endelea hivyohivyo kama hukufundwa na wazazi wako JF siyo mahali pake.
Pole una seem kua na Tafran ya nafsi yako,usinuneee,na hata kama huna ushauri wa kutoa sio lazima kila uzi lazima ujibu kama hujapenda Topic pita kwa salama na amani,mie mwenzio sijanuna wala hujanikera wewe wala mtu yoyote,kwa hisani yako usijikere sawaaaa,sipendi mtu akereke.
 
Wabongo mara nyingine tunapenda ku complicate mambo.

Hapo kuna ku complicate mambo pande zote mbili. Kwa huyo baba mdogo na kwa hao mtu na mkewe.

Huyo baba mdogo ana complicate mambo kwa kutaka kuleta sheria zake za shamba huko mjini.

Anatakiwa kushukuru kapata mwenyeji mjini. Kama hapendi utamaduni wa hapo aondoke.

Hao mtu na mkewe wana complicate mambo kwa kumfuga huyo baba mdogo anayewaletea sharia zake za shamba mjini. Mtu mzima umeoa una kwako halafu baba mdogo anakupangia sheria kwako kivipi?

Kesho akisema hataki mkeo apake lipstick, utasemaje?

Unamwambia tu, mzee, hapa tunaishi hivi, kama hupendi una ndugu wengine mjini, fungasha virago.

Tatizo tunawaonea haya sana hawa ndugu wenye mila za kikoloni.
That's my gentleman
 
Kaa na mumeo muamue nini cha kufanya. Kama mnataka kubadili namna mnavyoishi kwa hizi siku 11 ni hiari yenu la mnataka kuendelea kuishi ambavyo mmekuwa mnaishi na hugs & kisses basi hakuna ubaya. Hawezi kuja mtu kwenu ambaye hajui namna mnavyoishi akakasirika kwa kuona tu mnaonyesha mapenzi kati yenu kwa kukumbatiana wakati mnaagana. Kama anaona karaha afunge virago akatafute pa kuishi ambapo hakutakuwa na kero kama za hapo kwenu.

Habari za Leo Waungwana!

Nyumbani kwetu tumejiwa na mgeni ambae ni Baba mdogo wa mume wangu. Atakuwa kwetu kama 15 days. Amekuja medical na mkewe na watoto wa3. Tangu wamekuja leo ni siku ya 4.

Cha kushangaza leo asubuhi wakati watoto wanakwenda school wamekuja kutuaga which is normal. Huwa wanatukumbatia then wanaondoka na sisi pia me and my Hubby we Kiss and hug kila mtu anaingia kwenye gari yake safari ya kazini inaanza.

Huyu Mzee kuona leo namuhug mume wangu ili niingie kwenye gari katoka ndani mbio kamuita Hubby. Sasa sikuweza kuondoka ikabidi nisiingie kwenye gari nimsalimie, hakutaka hata kujibu salamu. Anagomba anamwambia my Hubby malezi gani haya unayolea watoto wako na mkeo? Hamuoni aibu mnakumbatiana, mambo ya kufanya chumbani mnafanya hapa, tabia gani hii mnatuonyesha nini?

Tangu nimeingia hapa naona tuu asubuhi mwaaaaaaaaaa! jioni mwaaaaaaaaaaa! Kama hamtaki wageni nyumbani kwenu semeni bwana msitunyanyase. Mimi sikuwa na la kusema nilirudi tena nikajikuta namhug tena my hubby nikamwambia siku njema tutaongea baadae.

Mzee kasema nataka kuongea na wewe mama mwenye nyumba jioni.

Ikumbukwe huyu baba ana wanawe na hawaongei wapo mji huu niliko mimi, watoto wake wa kike 38 na mwengine 41 na 28 ndio alokuja nao. Wote wa kike hawajaolewa kwa midomo yao. Wako kwangu lakini wanamwambia dada apike wanachotaka wao, wao hawawezi kula chakula cha kuchemsha kama wako Hospital.

Sasa najiuliza huyu mzee anataka nimjibu nini? Nimehisi nimnyamazie wakati anaongea sababu its just a matter of 11days anaondoka zake au atahisi nikinyamaza ntakua nimemdharau?

Waungwana naomba busara zenu as sio kama namchukia ila sipendi mtu anipangie sheria nyumbani kwangu. Ingekua nimevua nguo sawa lakini it was just a normal hug and kiss to my hubby na hata akiwepo nani tumeshazowea
kokote kule hata tuwe tumegombana as long as mmoja wetu ametoka akirudi Kiss and Hug ni must.
 
Huyo mzee amefeli hadi huruma. Yaani wanae wa umri wa miaka 41 hadi 28 nao wanaona sawa kuongozana wote watatu kupeleka baba hospitali? Na kukaa hapo kwako?

Msamehe bure. Usinune, wachukulie wote kama wagonjwa wa akili. Akiona hugs zinamsumbua atahama (ila naamini yeye Na wanae hawana ubavu huo)
 
Back
Top Bottom