Baba mdogo/mama mdogo

aksaf2003

Member
Nov 4, 2010
7
0
Hivi haiwezekani kuwa na neno moja tu likaweza kuwakilisha hii maana ya baba/mama mdogo, bila ya kurudia neno baba au mama
 
Najua umerejea Kiingereza, huko wao hutumia uncle na anti, pia Waarabu na jamii zao, wao hutumia ami kumaanisha baba mkubwa na baba mdogo. Ila mimi sioni tatizo kwenye maneno tunayotumia sasa...
 
Duh! Ni swali ambalo siku nyingi limekuwa likiniumiza kichwa. Kwa nini dada/ndugu wa kike wa baba anakuwa Shangazi, lakni ndugu/kaka yake anakuwa Baba mdogo; na ndugu wa kiume wa mama ni Mjomba, lakini ndugu/dada wa mama ni Mama mdogo.
 
Hivi haiwezekani kuwa na neno moja tu likaweza kuwakilisha hii maana ya baba/mama mdogo, bila ya kurudia neno baba au mama


Ndugu wa kike wa baba anaitwa shangazi

Ndugu wa kiume wa baba anaitwa Ami

Ndugu wa kike wa mama anaitwa Khalti

Ndugu wa kiume wa mama anaitwa Mjomba
 
ninaona ni bora nitioe mfano wa moja ya matatizo ambayo labda yanaweza yakajitokeza ,hivi kama wewe ni baba au mama na ikatokea kuwa na kutokufahamiana hop nyumbani,na ukajaribu kutumia busara ili mzozo huwo usiendele kwa kuamua hilo ukaona ni bura kuondoka hapo kwa muda na kwa kuwa ulijaliwa kuwa na mtoto mdogo kias cha miaka miwili na nusu basi pia ukamchukuwa na ukaelekea kwa shemegi yako/kaka /dada,na mlipo fika huko ukatoa utambulisho kwa mtoto kwa kumuambia kuwa huyu ni mama/baba ako mwingine na baada ya muda kupita makarudi nyumbani,na kwa furaha aliyonayo mtoto ya kufahamu familia yake kabla hata ya kuulizwa akanza kusimulia leo tumekwenda kwa baba/mama mingine.
kwa kuwa hatuna neno moja lenye kumaanisha MAMA/BABA mdogo sidhani kuwa hizo busara zako kamazitaleta hiyo amani ulioitegemea
 
Back
Top Bottom