Unajua neno "baba" ni zaidi ya watu wengi wanavyofahamu?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Kikwetu, inapotokea mtu ana ugomvi na mwenzake, na wameamua watafute Suluhu nje ya mahakama, sharti mojawapo la kikao kukaa ni kila mmoja kuwa na "baba" kwenye hicho kikao. Ajabu ni kwamba, wakati mwingine "baba" anaweza akawa na umri mdogo kuzidi mwenye kesi.

Lakini kwa sababu amekwenda kwa jina la "baba", ataheshimika kama "baba" mtu hata kama yeye ana miaka thelathini na "mtoto" wake ana miaka hamsini.

Inasemekana, Forojo Ganze aliwahi kumwita Julius K. Nyerere "baba", na Nyerere naye kuitikia "Naam mwanangu", ilhali Nyerere alikuwa mdogo kwa Ganze.

Forojo Ganze alizaliwa mwaka 1902 na Julius Nyerere mwaka 1922.

Katika kitabu cha Historia ya Askofu wa kwanza wa EAGT, Moses Kulola, imeandikwa kuwa baada ya Nyerere kustaafu Urais, alikuwa na kawaida ya kumtembelea Kulola nyumbani kwake Capri Point jijini Mwanza, hasa alipokuwa akienda Musoma kupitia Mwanza. Alipokuwa akikutana naye, alikuwa akimwita Kulola "baba".

Lakini Nyerere alikuwa mkubwa kwa Kulola. Nyerere alizaliwa mwaka 1922 na Kulola mwaka 1928.

Kwenye Biblia, Yusufu alipokutana na mdogo wake, Benjamin, ambaye walikuwa wamepotezana kwa miaka 22, alimwambia, "Mungu akufadhili, mwanangu" (Mwanzo 43:29). Benjamin alizaliwa miaka michache baada ya Yusufu kuzaliwa.

Baada ya Yusufu kujitambulisha kwa ndugu zake waliokuwa wamemwuza alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba, aliwaambia, "Basi, si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na mtawala katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri" (Mwanzo 45:8).

Nimetoa mifano tofauti kuonesha kuwa neno "baba" lina maana zaidi ya ile iliyozoeleka kwa watu wengi.

Kwa ufahamu wako, neno "baba" lina maana gani?

Kama wewe ni mwanaume, unafikiri kuna mtu ambaye ingawa huna uhusiano naye wa damu, lakini unahisi huenda Mungu kakuweka uwe kama baba kwake? Kama ndivyo, Unafanya nini kutimiza huo "wito"?
 
Baba wa kiroho mtapigwa za uso sana,mpaka mpauke.

Ole wenu kizazi chenye kupenda ishara ,hamtapata ishara isipokua ishara ya Yona, 12 mathayo 39- 40.
 
Baba ina thamani kubwa sana, Yesu alipokuwa juu ya msalaba pamoja n uhusiano wake mkubwa na Mungu lakini kuna sehemu alifika akahitaji msaada wa baba, baada ya mateso na maumivu kuwa makubwa sana alihisi kuachwa na baba yake.
 
hii baba kweli ni cheo cha heshima,hata wamama hupenda kuita namna hii watoto wao wa kiume,kuonyesha ni kwa namna gani wamewapa mamlaka akilini mwao.
 
Hivi ndivyo nijuavyo!
~ Baba ni MSINGI

~ Baba ni MWANZILISHI

~ Baba ni MWALIMU

~ Baba ni MSTAWISHAJI

~ Baba ni MTIMIZA MAHITAJI

~ Baba ni MLINZI

~ Baba ni MTETEZI

~ Baba ni MLEZI

~ Baba ni NGUZO

~ Baba ni MWONYAJI

~ Baba ni MTIA MOYO

~ Baba ni MFARIJI

Kwa hiyo kila mwanaume anapaswa kuwa baba ingawa si kila mwanaume ni baba!
 
Mimi mama yangu huniita mzazi ila maajabu ni dada yangu humwita mwanae baba.
Kuna wengine majina yao ni "Baba", kama ni mwanafunzi, utamkuta kaandikishwa shuleni kwa jina hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom