Baba Levo akiri kuwa ana wake Wawili

gstar

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
759
1,250
1705691524945.png

Baba Levo
Baada ya mahusiano ya Baba Levo na mzazi mwenziye anayejulikana kama Mama Ruby au Salma kuvunjika, inasemekana kwamba mkewe huyo Salma alilaghaiwa na vibopa ili amwache Baba levo akaenda afrika ya kusini kula bata. Huku nyuma Baba levo alihangaika sana kwenye mahusiano kwakuwa alikuwa hana mtu akampata msichana anayejulikana kwa jina la Asma. Huyu Asma ni mwigizaji na mchekeshaji wa stejini, alimchukua akamweka ndani na mapenzi yao yakawa moto moto.

Kwa mujibu wa baba levo mwenyewe anasema kwamba Asma alipendwa na watoto wake kiasi cha kuwita mama, hata mtoto wa mama Ruby aliyezaa na baba levo naye alilelewa vyema na bidada huyo bila ubaguzi wowote. Basi bi mkubwa mama ruby baada ya maisha kumshinda na kumwona mzazi mwenziwe akiwa ametakata na huku dili kadha wa kadhaa zikizidi kumwangukia na safari za nje kila kukicha akabidi arudi kumwomba msamaha mwenzi wake huyo.

Alimwomba msamaha mwenzi wake kwa kusema kwamba dunia ilimhadaa na watu wa mjini walimdanganya sasa ameamua kurudi ili alee watoto wake pamoja na mwenzi wake huyo. Bila hiyana baba levo alimkubalia ombi lake hilo lakini akamwambia kwamba atumie mitandao ya kijamii kumuomba msamaha kwani mara walivyo achana pia alitumia mitandao hiyo hiyo kumchafua, basi bidada Salma akaonekana kwenye mitandao akimwomba msamaha Baba Levo na kuahidi kuto kurudia kosa alilolifanya la kumcheat mpenzi wake huyo.

Basi Baba Levo kwakuwa alikuwa na mahusiano na Asma tayari ambayo yalisha ota mizizi ilibidi kumwomba Asma atoke pale nyumbani na kisha kumpangia nyumba maeneo ya Sinza na kumpa gari mpya ya kutembelea, hivyo hakumwacha Asma bali aliendelea naye kwa siri. Kwahivyo alikuwa na wake wawili mke mkubwa na mke mdogo mkubwa akiwa Mama Ruby na mdogo akiwa Asma.

Kivumbi kilianza pale ambapo Baba Levo alisafiri kuelekea China kutangaza kampuni ya Silent Ocean, inasemekama aliporudi alirudi na zawadi za kila aina lakini zote ziliishia kwa nyumba ndogo yaani Asma! Ndipo mtifuato ulipozuka kutoka kwa Mama ruby. Inakuwaje kumletea zawadi huyo mchepuko za pesa nyingi na mimi hukuniletea chochote? Baba Levo mwenyewe alipohojiwa na kituo cha Wasafi alikiri kumletea zawadi mchepuko huyo lakini alisema zawadi alizompa hazifikii zile alizopeleka kwa Mama Ruby, ila kinacho msumbua mkewe ni wivu na si kingine.

Kwahiyo mpaka sasa Baba levo anasema kwamba ameamua kuhamia kwa Asma na yeye hamuiti mchepuko bali mke na sababu ni kuwa mke mkubwa ndio chanzo, alisha onyesha mapungufu tangu mwanzo pale alipo ondoka nyumbani na kisha kurudi kuomba msamaha. Na pia anasema hawezi kumwacha Asma labda kama mzazi mwenziye ataona ameshindwa aondoke yeye kwani hakuna huduma anayo ikosa kutoka kwake. Haya wananzengo kwa wale ambao hamkuupata huu umbeya nimewasogezea hapa.
 
Ila baba levo ajitahidi kuwa anafanya mazoezi kidogo, angalau push up mbili tatu kila asubuhi na jioni.

Lile tumbo mbele na kile kishuzi nyuma havimpi muonekano mzuri.
 
Washaur wakiwa wawili na Yule mwenzake
 
Uyu uyu ba-levo
1. Aliyewai kukiri Analipiwa ada zote za watoto wake na platnumz

2. Aliyewai kukiri kua tayar kumzalia platnumz Mtoto MDA wowote atakapohitaji
 
Mkuu mm nimewahi kaa nae mahali na kumhoji maana nimejuana nae toka hajawa diwan ni bishoo tu wa kigoma pale mwanga.alinielexa aliyopitia na namna kamsoma mondi yaan ni kwel ukijishusha kwa mondi utakula hela .mengine siwezi sema ntamuharibia libarua.ila yy muasisi wa neno chawa ila mjini kuishi kwa kucheza na akili za matajiri ndo kulifanya dar iitwe bongo. Bongo kuishi kuna aina za ajabu mingi mfano doto magari yaan yeye unaambiwa hata umpe mil 100 rushwa aipeleke kwa afisa yeyote inafika salama afu hana tamaa hata umpe laki 3 anashukuru kwa magoti.uchawa upo maofisini.kanisani .kwenye familia etc na kigezo kikuu ni kutokuwa na mshipa wa aibu.japo ni kweli uchawa ni level ya watu wajinga walioshindwa maisha na huwa mwisho wao mbaya sana .
 
Baada ya mahusiano ya Baba Levo na mzazi mwenziye anayejulikana kama Mama Ruby au Salma kuvunjika, inasemekana kwamba mkewe huyo Salma alilaghaiwa na vibopa ili amwache Baba levo akaenda afrika ya kusini kula bata. Huku nyuma Baba levo alihangaika sana kwenye mahusiano kwakuwa alikuwa hana mtu akampata msichana anayejulikana kwa jina la Asma. Huyu Asma ni mwigizaji na mchekeshaji wa stejini, alimchukua akamweka ndani na mapenzi yao yakawa moto moto.

Kwa mujibu wa baba levo mwenyewe anasema kwamba Asma alipendwa na watoto wake kiasi cha kuwita mama, hata mtoto wa mama Ruby aliyezaa na baba levo naye alilelewa vyema na bidada huyo bila ubaguzi wowote. Basi bi mkubwa mama ruby baada ya maisha kumshinda na kumwona mzazi mwenziwe akiwa ametakata na huku dili kadha wa kadhaa zikizidi kumwangukia na safari za nje kila kukicha akabidi arudi kumwomba msamaha mwenzi wake huyo.

Alimwomba msamaha mwenzi wake kwa kusema kwamba dunia ilimhadaa na watu wa mjini walimdanganya sasa ameamua kurudi ili alee watoto wake pamoja na mwenzi wake huyo. Bila hiyana baba levo alimkubalia ombi lake hilo lakini akamwambia kwamba atumie mitandao ya kijamii kumuomba msamaha kwani mara walivyo achana pia alitumia mitandao hiyo hiyo kumchafua, basi bidada Salma akaonekana kwenye mitandao akimwomba msamaha Baba Levo na kuahidi kuto kurudia kosa alilolifanya la kumcheat mpenzi wake huyo.

Basi Baba Levo kwakuwa alikuwa na mahusiano na Asma tayari ambayo yalisha ota mizizi ilibidi kumwomba Asma atoke pale nyumbani na kisha kumpangia nyumba maeneo ya Sinza na kumpa gari mpya ya kutembelea, hivyo hakumwacha Asma bali aliendelea naye kwa siri. Kwahivyo alikuwa na wake wawili mke mkubwa na mke mdogo mkubwa akiwa Mama Ruby na mdogo akiwa Asma.

Kivumbi kilianza pale ambapo Baba Levo alisafiri kuelekea China kutangaza kampuni ya Silent Ocean, inasemekama aliporudi alirudi na zawadi za kila aina lakini zote ziliishia kwa nyumba ndogo yaani Asma! Ndipo mtifuato ulipozuka kutoka kwa Mama ruby. Inakuwaje kumletea zawadi huyo mchepuko za pesa nyingi na mimi hukuniletea chochote? Baba Levo mwenyewe alipohojiwa na kituo cha Wasafi alikiri kumletea zawadi mchepuko huyo lakini alisema zawadi alizompa hazifikii zile alizopeleka kwa Mama Ruby, ila kinacho msumbua mkewe ni wivu na si kingine.

Kwahiyo mpaka sasa Baba levo anasema kwamba ameamua kuhamia kwa Asma na yeye hamuiti mchepuko bali mke na sababu ni kuwa mke mkubwa ndio chanzo, alisha onyesha mapungufu tangu mwanzo pale alipo ondoka nyumbani na kisha kurudi kuomba msamaha. Na pia anasema hawezi kumwacha Asma labda kama mzazi mwenziye ataona ameshindwa aondoke yeye kwani hakuna huduma anayo ikosa kutoka kwake. Haya wananzengo kwa wale ambao hamkuupata huu umbeya nimewasogezea hapa.
Umbea umepungukiwa vi picha. Tuone nani ana kalio, shepu
 
Back
Top Bottom