Ninawapongeza wazazi wote wanaopambana kulea watoto wao wenyewe kwa namna yoyote ile

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,239
22,318
Wakuu dunia imefikia pabaya. Watu wamekuwa na roho za kikatili zisizoelezeka. Wahanga wa matukio ya kikatili ni watu dhaifu na mafukara ambao hushindwa kupata haki kwa sababu haki zao huporwa na wenye hela waliowafanyia ukatili. Hizi nyakati sio za kuacha mwanao akakae na kulelewa kwa bibi, babu, baba mdogo, mjomba, shangazi au mtu mwingine yeyote. Baba na mama pambaneni katika hali yoyote ile kulea watoto wenu. Mtakuwa mmewaepusha na mengi mno.

Vitendo vya kikatili kwa watoto hasa ulawiti na ubakaji vimekithiri barani Afrika. Hawa wanaoitwa binamu, mjomba, baba mdogo na jamaa zetu wengine wamekuwa wakitajwa sana kuhusika na huu unyanyasaji. Nimeshuhudia ndugu wengi waliokulia kwa bibi kujamiiana kama vile ni jambo halali. Kimsingi baba na mama ndo wenye uchungu na mtoto na sio mtu mwingine yeyote. Kama unajua hauko tayari kulea mtoto tumia condom ili kuepusha matatizo yasiyo na lazima.

Watu wengi maarufu wanaoonekana kama vile wamechanganyikiwa na kutokuwa na aibu huwa wanapambana na kumbukumbu za mambo mabaya waliyowahi kufanyiwa utotoni.
 
Bila shaka single Maza inawahusu wakishashusha engine mtoto akikua kua mtoto anaachiwa bibi yeye huyo anarudi tena mjini kuendelea kudanga
 
Back
Top Bottom