gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 759
- 1,250
Baba Levo
Kwa mujibu wa baba levo mwenyewe anasema kwamba Asma alipendwa na watoto wake kiasi cha kuwita mama, hata mtoto wa mama Ruby aliyezaa na baba levo naye alilelewa vyema na bidada huyo bila ubaguzi wowote. Basi bi mkubwa mama ruby baada ya maisha kumshinda na kumwona mzazi mwenziwe akiwa ametakata na huku dili kadha wa kadhaa zikizidi kumwangukia na safari za nje kila kukicha akabidi arudi kumwomba msamaha mwenzi wake huyo.
Alimwomba msamaha mwenzi wake kwa kusema kwamba dunia ilimhadaa na watu wa mjini walimdanganya sasa ameamua kurudi ili alee watoto wake pamoja na mwenzi wake huyo. Bila hiyana baba levo alimkubalia ombi lake hilo lakini akamwambia kwamba atumie mitandao ya kijamii kumuomba msamaha kwani mara walivyo achana pia alitumia mitandao hiyo hiyo kumchafua, basi bidada Salma akaonekana kwenye mitandao akimwomba msamaha Baba Levo na kuahidi kuto kurudia kosa alilolifanya la kumcheat mpenzi wake huyo.
Basi Baba Levo kwakuwa alikuwa na mahusiano na Asma tayari ambayo yalisha ota mizizi ilibidi kumwomba Asma atoke pale nyumbani na kisha kumpangia nyumba maeneo ya Sinza na kumpa gari mpya ya kutembelea, hivyo hakumwacha Asma bali aliendelea naye kwa siri. Kwahivyo alikuwa na wake wawili mke mkubwa na mke mdogo mkubwa akiwa Mama Ruby na mdogo akiwa Asma.
Kivumbi kilianza pale ambapo Baba Levo alisafiri kuelekea China kutangaza kampuni ya Silent Ocean, inasemekama aliporudi alirudi na zawadi za kila aina lakini zote ziliishia kwa nyumba ndogo yaani Asma! Ndipo mtifuato ulipozuka kutoka kwa Mama ruby. Inakuwaje kumletea zawadi huyo mchepuko za pesa nyingi na mimi hukuniletea chochote? Baba Levo mwenyewe alipohojiwa na kituo cha Wasafi alikiri kumletea zawadi mchepuko huyo lakini alisema zawadi alizompa hazifikii zile alizopeleka kwa Mama Ruby, ila kinacho msumbua mkewe ni wivu na si kingine.
Kwahiyo mpaka sasa Baba levo anasema kwamba ameamua kuhamia kwa Asma na yeye hamuiti mchepuko bali mke na sababu ni kuwa mke mkubwa ndio chanzo, alisha onyesha mapungufu tangu mwanzo pale alipo ondoka nyumbani na kisha kurudi kuomba msamaha. Na pia anasema hawezi kumwacha Asma labda kama mzazi mwenziye ataona ameshindwa aondoke yeye kwani hakuna huduma anayo ikosa kutoka kwake. Haya wananzengo kwa wale ambao hamkuupata huu umbeya nimewasogezea hapa.