Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
(KIJANA);Baba,nimepata mchumba hapo mtaa wa pili,anaitwa Sandra! (BABA);Ooops,samahani kijana wangu,ila usimwambie mama yako,sandra ni dada yako,si unajua mambo ya ujana mwanangu! (KIJANA);{siku nyingine},baba nimepata mchumba anaitwa angel,anaishi pale kwa mwalimu Mushi. (BABA);Duuh,mwanangu una mkosi wewe!samahani kijana wangu sikukwambia,huyo naye pia ni dadako ila kuwa kama mwanaume usimwambie mamako!. >>>>>Kijana aliondoka huku machozi yakimbubujika,akaenda kumweleza mama yake ukweli wote.Mama akamwambia kwa upole;'usihofu mwanangu,hata hivyo huyu si babako mzazi,kwa hiyo chagua kati ya Sandra na Angel uoe unayempenda!'.