Baada ya Mbowe kugeuka na kuwa kama kina Shibuda, John Cheyo na Mrema ni upi mustakbali wa siasa za upinzani Tanzania?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,504
51,099
Kwa hali inavyoendelea nchini ni dhahiri hakuna tena upinzani. Bali kuna uungwaji mkono juhudi unaofanywa na wapinzani kwa CCM ila kila mmoja kwa staili yake. ACT Wazalendo wanakula pamoja na CCM kule Zanzibar na CHADEMA nao wanatafuta robo mkate wao huku Tanganyika.

Kabla CHadema hawajaanza kupetiwapetiwa, Kutomaswatomaswa na kulambishwa asali na CCM hii ya leo ya Kinana na Samia, walikuwa wakitokwa povu sana kuhusu ACT Wazalendo kuingia katika serikali ya umoja wa Kitaifa huko Zanzibar. ACT walikuwa wakijitetea kuwa eti ni takwa la kikatiba kuingia humo huku CHADEMA wakiwaita ACT Wasaliti kwa hoja ya kuwa wamewasaliti Wazanzibar kwa kushiriki kula matunda ya uchaguzi haramu.

Leo tunaona CHADEMA nao wamekinga mkono kula ruzuku ambayo hapo mwanzo walisema ni haramu kwa kuwa imetokana na uchaguzi haramu. Kiufupi wamelamba matapishi yao!.

Ukiachilia mbali hilo, CHADEMA walikuwa wakijulikana sana kuwatukana akina hayati Lyatonga Mrema , John Cheyo na Shibuda kuwa eti ni makada wa CCM kutokana na kuwa na siasa za mrengo wa kukubaliana na CCM katika mambo mengi. Leo tunamuona Mwenyekiti Mbowe naye akigeuka kuwa Cheyo na Shibuda aliyechangamka zaidi.

Mbowe leo kaibeba rasmi mikoba ya John Cheyo na ameanza kutumia arguments zilezile za John Cheyo kuwa anataka siasa za "maridhiano", ambazo kimsingi siasa za hivyo ni za kutomasanatomasana, kubembelezanabembelezana ilimradi tu kila mtu aachiwe sphere yake ya influence ili aweze kula kwa urefu wa kamba yake.

Tujiulize, Hizi sifa ambazo Mbowe anazitoa kwa Samia zina tofauti gani kwa mfano na Sifa za Cheyo au Shibuda walizokuwa wakizimwaga kwa Magufuli?

Hii inaonyesha kuwa pengine ukiwa mpinzani na ukaanza kuzeeka, unaanza kuwa na tabia za OLD MAN CCM SYNDROME. Yaani unaanza kuwa na tabia zile za kiCCM CCM. Unaanza kujisogeza kwa CCM, unaanza kuongea kama wanaCCM, na unaanza kubehave kama wanaCCM

Huu ni muda muafaka kwa wanaCHADEMA kumtafakari Mwenyekiti Mbowe kuona kuwa , Je ni kweli siasa hizi za kulala kitanda kimoja na CCM anazoanza kuzifanya zinatokana na utafiti wa kina na upeo wa kisiasa au zinatokana na

1. Mosi, Je ana makubaliano ya siri na CCM ikiwa kama sababu ya kuachiwa kwake kutoka Jela na kwa hivyo anafuata script aliyotengenezewa AU

2. Je ana masilahi binafsi ikiwemo ya kibiashara au kurudishiwa mali zake alizoporwa na serikali ya CCM kipindi cha Mwendazake?

3. Au je ni uzee na uchovu(wa Kisiasa) kwa hiyo ndo ameamua kwenda na falsafa maarufu ya "Kama huwezi kuwashinda, basi ungana nao?".

Katika nchi yoyote ukiona UPINZANI unafanya ROMANCE na Chama Tawala, Jua kuwa hakuna upinzani hapo bali kuna genge la wapiga dili wa kisiasa
 
Kwa hali inavyoendelea nchini ni dhahiri hakuna tena upinzani. Bali kuna uungwaji mkono juhudi wa Wapinzani kwa CCM kila mmoja kwa staili yake. ACT Wazalendo wanakula pamoja na CCM kule Zanzibar na CHADEMA nao wanatafuta robo mkate wao huku Tanganyika.
Tuacheni kejeli instead tuwapongeze Samia na Mbowe kwa kuweka masilahi ya nchi yetu mbele kuliko kitu kingine chochote.

Hii nchi angeendelea kuwa hai yule HAYAWANI wa Chato ingekuwa nchi ya hovyo kuliko Yemen na Somalia
Muache aendee kuoza huko aliko
 
Kabla CHadema hawajaanza kupetiwapetiwa, Kutomaswatomaswa na kulambishwa asali na CCM hii ya leo ya Kinana na Samia, walikuwa wakitokwa povu sana kuhusu ACT Wazalendo kuingia katika serikali ya umoja wa Kitaifa huko Zanzibar.
Wakati wanateseka kipindi cha Magufuli ulitoa msaada gani kwao waache wafanye wanaloliona ni sahii kwao
 
Tuacheni kejeli instead tuwapongeze Samia na Mbowe kwa kuweka masilahi ya nchi yetu mbele kuliko kitu kingine chochote.

Hii nchi angeendelea kuwa hai yule HAYAWANI wa Chato ingekuwa nchi ya hovyo kuliko Yemen na Somalia
Muache aendee kuoza huko aliko
Ilifikia hatua hataki mwana ccm aende kumuanglia mwanachadema kama anaumwa
Siasa sio uadui ila kwa magufuli siasa ni uadui
 
Tuacheni kejeli instead tuwapongeze Samia na Mbowe kwa kuweka masilahi ya nchi yetu mbele kuliko kitu kingine chochote.

Hii nchi angeendelea kuwa hai yule HAYAWANI wa Chato ingekuwa nchi ya hovyo kuliko Yemen na Somalia
Muache aendee kuoza huko aliko
Hujawahi kufanya hivyo kwa John Cheyo na siasa zake za kushirikiana na CCM
 
Wapinzani sisi hatuelewi huo msimamo wa viongozi wa CDM kwa muongozo wa Mbowe. Wao viongozi waendelee na siasa za kujikomba, lakini sisi hatuna muda huo. Kama Mbowe aliweza kumpokea Lowassa na watu wakamvumilia, basi safari hii atajua hana ushawishi huo aliodhani anao. Ni muda mrefu Mbowe alishaonyesha kupoteza mwelekeo.
 
Wakati wanateseka kwa kufilisiwa, na kuwekwa rumande kwa kesi za mchongo, na wengine kuuliwa mlitoa msaada gani kwao
 
Wakati wanateseka kwa kufilisiwa, na kuwekwa rumande kwa kesi za mchongo, na wengine kuuliwa mlitoa msaada gani kwao
Kuteseka ni sehemu ya struggle. Kama hutaki kuteseka kaa pembeni ili walio tayari hata kufa ili kuleta mabadilikio ya kweli washike usukani. Kuliko kusaliti stuggle na kuanza kujikombakomba kwa CCM bora ukae pembeni ulee wajukuu au ule bata kadri unavyoweza
 
Back
Top Bottom