Baada ya Lowasa kukataliwa Kanda ya Ziwa, Apson Mwang'onda na Tupa wawasili Bukoba kuokoa Jahazi

View attachment 189135
Pichani Lowasa akiteta jambo na Steven Wassira mara baada ya kuahirishwa kikao cha Bunge Maalum la Katiba saa saba mchana leo. Nimemsikia Wassira akimtania Lowasa kuwa nimeona kupitia Jamiiforums harakati zako Kanda ya Ziwa. Lowasa akajibu kuwa tuyaache hayo.

Angalieni miguu ya lowasa ilivyo legea wakuu kama ametoka kuruka kichura punde kweli anaumwa.
 
Wadau, baada ya Edward Lowasa kupitia taarifa ya hali ya kisiasa aliyopata akiwa ziarani Mkoa wa Mara hivi karibuni kubaini kuwa kwa sasa amepoteza mvuto Kanda ya Ziwa na kwamba baadhi ya makada wake wamehama kambi, amemtuma Mwenyekiti wa Kamati ya Wezesha Lowasa Aende Ikulu, Apson Mwang'onda kwenda kuweka mambo sawa. Kwamba, Apson Mwa'onda amewasili Mjini Bukoba ambako amepanga kuanza ziara kwenye mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kuongeza morali na kubwa zaidi kuwamwagia fedha walengwa fedha ambazo amepewa na Lowasa.

Apson Mwang'onda ameambatana na Francis Tupa ambaye hivi karibuni amemteua kuwa mhamasishaji wa Wastaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa ili wajiunge na Kambi ya Lowasa. Francis Tupa ni Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye nimedokezwa kuwa aliwahi kuwa Afisa Usalama wa Taifa Mkoa. Katika ziara hiyo ya kanda ya Ziwa, Apson na Tupa wameanzia Bukoba baada ya kupata taarifa kuwa baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliochukua shilingi laki Mbili (200,000) wameapa kusaliti kambi hiyo kwa vile Lowasa ni fisadi na afya yake ni mgogoro hali ambayo inamuondolea sifa za kugombea nafasi ya Urais.

Wakiwa Kanda ya Ziwa, Apson na Tupa wamepanga kukutana na viongozi wa Mkoa na Wilaya wa CCM ambao ni kambi ya Lowasa ili kuwapa mikakati mipya ya kuimarisha kambi hiyo. Pia watakutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka kanda hiyo ili kuboresha kiwango cha fedha baada ya kupata malalamiko kuwa laki mbili walizopata ni fedha kidogo. Kiasi cha fedha ambacho wajumbe hao watapata bado hakijabainishwa isipokuwa taarifa zilizopo ni kwamba wajumbe walioipa mgongo kambi hiyo watapewa kiasi kikubwa zaidi ya wale wanaonekana ni 'royal' kwa Lowasa. Pia Apson na Tupa wamepanga kumnyamazisha Anthony Dialo kutokana na hivi karibuni kujitokeza hadharani na kumshambulia Lowasa hali ambayo wameitafsiri kuwa ni ishara mbaya kwa Kambi ya Lowasa hasa kutokana na kwamba Dialo alikuwa kambi yao na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana Kanda ya Ziwa.

Wadau, nitaendelea kuwajuza kwa kadri iwezekanavyo juu ya ziara hiyo na kila kitu kitakuwa wazi kupitia mtandao huu. Hii sasa ni kufuru. Kama Lowasa anaendelea kumwaga fedha ili tu aende Ikulu ilhali nyoyo za hao wanaopewa fedha hazipo pamoja naye, hakika ni isirafu iliyopindukia. Ni wakati muafaka sasa Kwa Lowasa kujitathmini upya ili asiendelee kupoteza fedha alizopata kwa njia za kifisadi. Pia ni wakati muafaka kwa Apson na timu yake kuachana na biashara hii ambayo bila shaka inaendelea kuwadhalilisha na kushusha hadhi zao ndani ya taifa hili.

unafahamu unachokifanya je kama ndio unazani mwalimu wako wataaluma ya uandishi alikuambia kuwa ukishajua kuandika sasa shusha matusi kwa viongozi wa kaya zako... fanya kila jambo kwa sababu na maslahi ya wanao kuzunguka ukiwa unajua namna ya kumsaidia dada yako aliekosa maabara katika shule yake ya kata na si kuvunja matumaini ya yeye kwenda mbele .... usitumike kiasi hichi... Chabruma
 
Last edited by a moderator:
Jamani CHABRUMA na nyie wengine wote ambao kila kukicha mnakuja na thread kuhusu LOWASA ebu mwacheni huyu mzee apumzike, punguzeni maneno kwenye mitandao, maamuzi tuachieni sisi wa TZ ndo tutaamua, kama mtu anamwaga pesa zake basi mwacheni nyie subilieni maamuzi ya wananchi basi.
Mkuu, tutaachaje sasa kuandika ilhali ukweli ndo huo? Mbona mijadala ya Katiba Mpya imekuwa mingi na hakuna anayeilalamikia?
 
unafahamu unachokifanya je kama ndio unazani mwalimu wako wataaluma ya uandishi alikuambia kuwa ukishajua kuandika sasa shusha matusi kwa viongozi wa kaya zako... fanya kila jambo kwa sababu na maslahi ya wanao kuzunguka ukiwa unajua namna ya kumsaidia dada yako aliekosa maabara katika shule yake ya kata na si kuvunja matumaini ya yeye kwenda mbele .... usitumike kiasi hichi... Chabruma
Mkuu, mimi situmiki hata kidogo na sitaacha kuanika wazi njama za huyu fisadi
 
dawa ya wajinga kama nyie nikupuuzwa,msimu kama huu mzee atakuwa anasubiri kuapishwa ntafurahi kuziona comment zenu za kipuuzi kama hizi hapa jamvini
 
Nani kakulazimisha kusoma sisi wengine tunafurahia sana mabadiko yake ngoja kesho atakuja na hili "Japhta2003 kugombea ujumbe wa nyumba kumi kumi"

Mkuu huna kingine cha kuandika au cha kufanya?.kila siku Lowasa,wengine tumrshaanza kuchoka sasa habari zako,kwani unarudia hayo hayo.hakuna jipya hapa
 
Mkuu, mimi situmiki hata kidogo na sitaacha kuanika wazi njama za huyu fisadi

kama hutumiki hizo pesa anazogawa lowassa katika upeo mdogo anamiliki BOT unaelewa namna ya kujenga hoja....unataka kuniambia funguo za BOT ANATEMBEA NAZO...
 
AISEE NA MIMI NIKITAKA KUMPIGIA DEBE HUYU MZEE NIMUONE NANI ILI NIPATE BAKAA,NJAA JAMA NJAAA,WAPI PESA YA LOWASA TUFANYE KAMPENI?:typing::typing:
 
unafahamu unachokifanya je kama ndio unazani mwalimu wako wataaluma ya uandishi alikuambia kuwa ukishajua kuandika sasa shusha matusi kwa viongozi wa kaya zako... fanya kila jambo kwa sababu na maslahi ya wanao kuzunguka ukiwa unajua namna ya kumsaidia dada yako aliekosa maabara katika shule yake ya kata na si kuvunja matumaini ya yeye kwenda mbele .... usitumike kiasi hichi... Chabruma
namtetea Chabruma kwa hili, Mbona sijaona matusi aliyoyaporomosha? au chuki binafsi?
 
hii inahusiana vipi na post ya Chabruma?

FUATILIA MJADALA HOJA ZINAJENGWA KWA MTIRIRIKO..... amesema kuwa lowassa anagawa pesa kila mahala sasa je lowassa ni begi la BOT.... bila shaka wewe ni kijana tafuta namna ya kuweza kujenga hoja hasa pale ambapo watanzania wenzako tunazulimiwa na jasho letu na matapeli wa pesa za ESCROW ufisadi ambao hauja wahi kutokea kama kweli mnataka ukombozi na si kuwaandama viongozi wazalendo...
 
Back
Top Bottom