Baada ya Lowasa kukataliwa Kanda ya Ziwa, Apson Mwang'onda na Tupa wawasili Bukoba kuokoa Jahazi

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau, baada ya Edward Lowasa kupitia taarifa ya hali ya kisiasa aliyopata akiwa ziarani Mkoa wa Mara hivi karibuni kubaini kuwa kwa sasa amepoteza mvuto Kanda ya Ziwa na kwamba baadhi ya makada wake wamehama kambi, amemtuma Mwenyekiti wa Kamati ya Wezesha Lowasa Aende Ikulu, Apson Mwang'onda kwenda kuweka mambo sawa. Kwamba, Apson Mwa'onda amewasili Mjini Bukoba ambako amepanga kuanza ziara kwenye mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kuongeza morali na kubwa zaidi kuwamwagia fedha walengwa fedha ambazo amepewa na Lowasa.

Apson Mwang'onda ameambatana na Francis Tupa ambaye hivi karibuni amemteua kuwa mhamasishaji wa Wastaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa ili wajiunge na Kambi ya Lowasa. Francis Tupa ni Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye nimedokezwa kuwa aliwahi kuwa Afisa Usalama wa Taifa Mkoa. Katika ziara hiyo ya kanda ya Ziwa, Apson na Tupa wameanzia Bukoba baada ya kupata taarifa kuwa baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliochukua shilingi laki Mbili (200,000) wameapa kusaliti kambi hiyo kwa vile Lowasa ni fisadi na afya yake ni mgogoro hali ambayo inamuondolea sifa za kugombea nafasi ya Urais.

Wakiwa Kanda ya Ziwa, Apson na Tupa wamepanga kukutana na viongozi wa Mkoa na Wilaya wa CCM ambao ni kambi ya Lowasa ili kuwapa mikakati mipya ya kuimarisha kambi hiyo. Pia watakutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka kanda hiyo ili kuboresha kiwango cha fedha baada ya kupata malalamiko kuwa laki mbili walizopata ni fedha kidogo. Kiasi cha fedha ambacho wajumbe hao watapata bado hakijabainishwa isipokuwa taarifa zilizopo ni kwamba wajumbe walioipa mgongo kambi hiyo watapewa kiasi kikubwa zaidi ya wale wanaonekana ni 'royal' kwa Lowasa. Pia Apson na Tupa wamepanga kumnyamazisha Anthony Dialo kutokana na hivi karibuni kujitokeza hadharani na kumshambulia Lowasa hali ambayo wameitafsiri kuwa ni ishara mbaya kwa Kambi ya Lowasa hasa kutokana na kwamba Dialo alikuwa kambi yao na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana Kanda ya Ziwa.

Wadau, nitaendelea kuwajuza kwa kadri iwezekanavyo juu ya ziara hiyo na kila kitu kitakuwa wazi kupitia mtandao huu. Hii sasa ni kufuru. Kama Lowasa anaendelea kumwaga fedha ili tu aende Ikulu ilhali nyoyo za hao wanaopewa fedha hazipo pamoja naye, hakika ni isirafu iliyopindukia. Ni wakati muafaka sasa Kwa Lowasa kujitathmini upya ili asiendelee kupoteza fedha alizopata kwa njia za kifisadi. Pia ni wakati muafaka kwa Apson na timu yake kuachana na biashara hii ambayo bila shaka inaendelea kuwadhalilisha na kushusha hadhi zao ndani ya taifa hili.
 
Hii sasa kufuru. Kwa nini Lowasa atumie kiasi kikubwa hivi cha fedha kama anajiamini kuwa anakubalika na wananchi wengi?
 
Hapo ndipon LOWASSA anabugi stepu sasa, hivi maafisa usalama wa Taifa ukiachilia mbali waliostaafu, hata walioko kazini. wanafahamika kwa wananchi hadi wakubali kuwashawishi? mbona nasikia hao watu wanaofanyakazi kwa siri sana, wananchi watawafahamu vipi?
 
Wasifanye kama walivyowafanyia mwalimu na yule daktari wa mifugo toka Zenji.
 
Mkuu, wewe nenda kwenye hoja badala ya kumjadili mtu

nimeona thread zako nying lazma uanze na Lowasa mida flani umekuja unadai katoa laki2 kwa wajumbe,tuna mambo mengi ya kufanya hebu achana na siasa za maji taka,au umeahidiwa u-DC na hao wanaokutumia,bado hatujamaliza mambo ya katba we unataka kututoa kwenye agenda kwa ulafi wako wa kuzawadiwa cheo
 
Mkuu, Chabruma ni noma, nadhani LOWASSA akimjua anaweza kumfanya kitu mbaya kwa jinsi anavyomwanika.
Mkuu, hata kwenye vita ya Kagera, si wote walioenda kupigana na Nduli Idd Amin walirudi salama. Wengi walijeruhiwa na kubaki vilema na wengine waliuawa lakini wote wanaitwa mashujaa kwa vile walifanikisha lengo la kumpiga adui. Nipo tayari kwa lolote
 
Safari hii mmbebanwa mpaka kwenye makalio,,,jamaaa yenu mbona bado hajaota ndoto lakini wapambe mnabanwa na haja???
 
Back
Top Bottom