Baada ya kupata matatizo, mchumba wangu akaolewa na mfanyakazi mwenzangu

Habari wana jf.

Ni siku nyingine tulivu namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiona siku hii ya Leo maana wengi walitamani lakini hawajafanikiwa kuiona na wengine wapo mahospitalini eeh mungu wasaidie wapone.

Katika maisha wanawake si Wa kuwaamini kwa asilimia 100 zote hapana kabisa..Mwaka 2009 niliajiriwa baada ya kuanza kazi mwaka huo 2009 nilijikita zaidi katika kujiendeleza kielimu nilijiunga na Chuo kikuu huria na hatimaye mwaka 2012 nilihitimu Degree yangu..

Mwaka huo waliajiriwa wafanyakazi wengine ...walikuwepo ma binti kadhaa pamoja na wanaume kadhaa kama ilivyo wafanyakazi wanapoajiriwa kidogo mambo yao huwa yanakuwa hayajakaa sawa sawa..Nilitokea kumpenda binti mmoja kati ya wale wageni nikasema huyu ndiye na lazima atakuwa mke wangu...

Kiukweli nilimpenda na hata yeye pia alinipenda uhusiano wetu ulikuwa imara baadae Mimi na yeye tukawa tunatembeleana kwa kuwa naye alikuwa amepanga nikawa naenda kwake nalala au yeye anakuja analala kwangu.

Mwaka 2013 mwezi Wa 11 nilipatwa na matatizo kazini na kupelekea kufikishwa mahakamani kwa kosa la MAUAJI...wakati nikiwa gerezani nikisubilia vikao vya jaji kwa sababu Mimi nipo pembezoni mwa Tanzania.....nilikaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa ndio jaji alikuja na kuanza kusikiliza kesi yangu katika kipindi chote hicho.....Huyo mchumba wangu alikuwa akija na kuanza kunifariji sana Mara nyingi alikuwa akija siku za jumapili pale Gerezani aliniahidi atanivumilia...

Kwa kuwa mshahara ulikuwa ukiendelea kusoma nilimkabidhi kadi yangu ya bank na vitu vyangu vyote nilimkabidhi yeye ...mwaka 2015 mwanzoni ndipo nilipatikana na HATIA YA KUUA BILA kukusudia na nikahukumiwa kwenda Jela miaka 5...alilia sana huyo mchumba wangu nilimsihi asilie maana hii yote ni mipango ya mungu nilimuambia asijali Mimi nitatoka tu maana HAKI YA MTU HUWA HAIPOTEI.

Wakati nipo Gerezani baada ya hukumu ile akaanza kubadilika nilikaa mwezi mzima bila kumuona nikaanza kusikia kwa watu kuwa mchumba wako yule Fred ambaye ni mdogo wako kikazi nasikia wanatoka....
niliumia sana kusikia vile niliamua kukata Rufaa na Bahati nzuri niliachiwa huru mwaka Jana....niliwakuta teyari wamwashaoana...na wanaishi kama mke na Mme nilmfuata nikamuambia anipe vitu vyangu kwa aibu yule Dogo alijificha chumbani.......nilichukua vitu vyangu na kuondoka pale


Tufanyeni kazi lakini watu sio wazuri pata matatizo ndo utajua Nani ni Mchumba/mke Wa kweli....


View attachment 402317

MAMBO GANI YA KUWEKA MKE WANGU HAPA
NTAKUCHUKULIA HATU
 
KILA NIKIWAZA NIANDIKE NINI HAPANA NASITA INAUMA ........................................... KAMA NDIO UJU HAPPY BIRTHDAY KWAKE Olala aaaa hawa viumbe bana kama cake vile
 
Acha bana!!

Namuonea huruma kumuacha nitamuumiza tena
https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/Namuonea-huruma-kumuacha-nitamuumiza-tena.868074/

e8e6f59299e2741571a49070d81639a3.jpg
Hii kitu ni kweli na wala sio hadithi...kama wewe unavyofikiria
 
Mkuu pole sana ila inauma, wanajamvi wamekupa pole, kumbe wanajamvi tunapendana, ila, mkuu, kwa picha niliyo iona hapo juu siyo ya kuoa na haina sifa ya uvumilivu, pili mkuu binti huyu, ni vigumu akusubilie mkuu, kwa miaka mitano na uzuri wake huu, si dhana mkuu zilikuwa ni ndoto za abunuasi, na hata aliye mchukua fatilia Maisha yake itakuwa ni vurughu tu siku zote huenda mungu amekuepushia shida hii ww akamwambia mshikaji mkuu ushauri wangu naomba, umusahau kabisa tafuta mwingine uoe wana wake ni wengi ila usitegemee mwanamke huyu angekusubilia within five years, please try again later.
 
Pole sana Mkuu, labda binti aliona hawezi kusubiri miaka mitano baada ya kusikia hukumu yako.
 
Nimekaa Gerezani kama miaka miwili tu....
Hivi ingekua ndo dada kakaa gerezani kwa muda kama huo wewe ungevumilia kweli? Au mnaongeaga tu mbaya zaidi hukua umemwoa.
Ndio ulimpa kila kitu ila umesahau kua kitu kimoja bahati mbaya ulikua nacho wewe gerezani.
 
Habari wana JF,

Ni siku nyingine tulivu namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiona siku hii ya Leo maana wengi walitamani lakini hawajafanikiwa kuiona na wengine wapo mahospitalini eeh Mungu wasaidie wapone.

Katika maisha wanawake si wa kuwaamini kwa asilimia 100 zote hapana kabisa. Mwaka 2009 niliajiriwa baada ya kuanza kazi mwaka huo 2009 nilijikita zaidi katika kujiendeleza kielimu nilijiunga na Chuo Kikuu huria na hatimaye mwaka 2012 nilihitimu Degree yangu.

Mwaka huo waliajiriwa wafanyakazi wengine walikuwepo ma binti kadhaa pamoja na wanaume kadhaa kama ilivyo wafanyakazi wanapoajiriwa kidogo mambo yao huwa yanakuwa hayajakaa sawa sawa. Nilitokea kumpenda binti mmoja kati ya wale wageni nikasema huyu ndiye na lazima atakuwa mke wangu.

Kiukweli nilimpenda na hata yeye pia alinipenda uhusiano wetu ulikuwa imara baadae mimi na yeye tukawa tunatembeleana kwa kuwa naye alikuwa amepanga nikawa naenda kwake nalala au yeye anakuja analala kwangu.

Mwaka 2013 mwezi wa 11 nilipatwa na matatizo kazini na kupelekea kufikishwa mahakamani kwa kosa la MAUAJI, wakati nikiwa gerezani nikisubiria vikao vya jaji kwa sababu mimi nipo pembezoni mwa Tanzania.

Nilikaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa ndio jaji alikuja na kuanza kusikiliza kesi yangu katika kipindi chote hicho huyo mchumba wangu alikuwa akija na kuanza kunifariji sana Mara nyingi alikuwa akija siku za Jumapili pale Gerezani aliniahidi atanivumilia.

Kwa kuwa mshahara ulikuwa ukiendelea kusoma nilimkabidhi kadi yangu ya bank na vitu vyangu vyote nilimkabidhi yeye, mwaka 2015 mwanzoni ndipo nilipatikana na HATIA YA KUUA BILA KUKUSUDIA na nikahukumiwa kwenda Jela miaka 5, alilia sana huyo mchumba wangu nilimsihi asilie maana hii yote ni mipango ya Mungu nilimuambia asijali mimi nitatoka tu maana HAKI YA MTU HUWA HAIPOTEI.

Wakati nipo Gerezani baada ya hukumu ile akaanza kubadilika nilikaa mwezi mzima bila kumuona nikaanza kusikia kwa watu kuwa mchumba wako yule Fred ambaye ni mdogo wako kikazi nasikia wanatoka niliumia sana kusikia vile niliamua kukata Rufaa na bahati nzuri niliachiwa huru mwaka Jana.

Niliwakuta tayari wamwashaoana na wanaishi kama mke na mume nilimfuata nikamuambia anipe vitu vyangu kwa aibu yule dogo alijificha chumbani, nilichukua vitu vyangu na kuondoka pale.

Tufanyeni kazi lakini watu sio wazuri pata matatizo ndo utajua nani ni mchumba/mke wa kweli.
ulihukumiwa miaka mitano na sasa upo uraiani,.What happened?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom