Baada ya kukatika nchi nzima; umeme warejea!

Yanatengenezwa mazingira ya 'dharura' hapo...Hivi ni lini kutakuwa na umeme wa uhakika Tanzania??Maana watumiaji ni proportion chache tu ya raia wote,ile kuwakidhi hao tu nalo limekuwa shida.Where is da vision mr president?Ngeleja?Rashid(if u r stil there)?

Sasa unafikiri zile generator 'zetu' tutazipeleka wapi???
 
Mh! Isije kuwa ni Mungu wa Kakobe ameanza kujibu maombi yake kiawamu.
 
Mkuu tulishaambiwa kwamba Kikwete katika awamu yake ya kwanza katimiza yale yote yaliyokuwemo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005. Nadhani asilimia kubwa ya yaliyokuwemo kwenye ilani hiyo ni kuwakingia kifua mafisadi wote kuanzia Mkapa, Rostam, Karamagi, Iddrisa Rashid, Mzee wa Vijisenti na wengineo wengi. Ingekuwa nchi nyingi uchaguzi wa mwaka huu CCM ingekiona cha mtema kuni kilimchotoa kanga manyoya kwa kuwadharau kabisa wapiga kura, lakni kwa nchi yetu watashinda tena kwa kishindi kikubwa na kurudi tena madarakani kiulaini kabisa. Mungu inusuru nchi yetu.
Huwa inauma sana Mkuu.

Hawa jamaa hawana mapenzi kabisa na nchi zaidi ya kuendeleza wizi.

Serikali lazima ielewe kuwa, Wananchi sasa wanafahamu kuwa CCM ni chama kilicho kosa dira, mwelekeo, na upendo kwa wananchi wake. Na mwaka huu lazima atolewe mtu nishai, wapende au wasipende.

Habari za kukosa maji mtera ni upuuzi mtupu usio na mwelekeo. Habari za Richmond ni utumbo mtupu usio na thamani.

Dunia ya leo, si tegemezi kama ile dunia ya ujima. Tungependa hawa CCM watueleze, ni kwanini umeme unakatika wakati nchi ina upepo?
 
Sasa unafikiri zile generator 'zetu' tutazipeleka wapi???
Pamoja na kuwa na mito yote inayotuzunguka na rasilimali nyingi tulizonazo bado hata hatuwezi tukaumiza vichwa japo kidogo tu tuone tutajikwamua vipi na tatizo la nishati.Inabidi tufike mahala tukalitendea taifa letu haki ambapo ni pamoja na kuondoa kero kama hizi na hata tukafikiria kuwa mzee mwanakijiji kule aliko na wazee wenzake waache kukata magogo kwa ajili ya mkaa kwa kuwasambazia umeme vijiji.
 
Habari zinazotiririka sasa hivi zinadokeza kuwa umeme umekatika katika maeneo mbalimbali ya nchi na hadi hivi sasa bado chanzo hakijajulikana lakini siwezi kushangaa kutasababisha kununuliwa kwa haraka kwa mitambo ya Dowans (kitu ambacho hakitaondoa tatizolenyewe)..

Mikoa ambayo inaripoti kukatika kwa umeme ni maeneo kadha ya Jiji la Dar, Mwanza, Moro, Tanga, Arusha.. tunaendelea kufuatiliia..
Mimi niko Mbeya umeme ulikatikatika saa 1:00 jioni mkoa mzima wa Mbeya, nikajua sasa hapa ngoja tusubiri isije ikawa kama alivyosema Askofu KKB kuwa ataombea umeme usiwake,

Kama umeme umekatika Mbeya maana yake hata Iringa itakuwa hivyo.
 
Sasa unafikiri zile generator 'zetu' tutazipeleka wapi???

Naam watashuka tena ili kupigia tena debe ununuzi wa mitambo ya Richmonf ambayo iliingia nchini kifisadi. "Serikali imesema tena kuna umuhimu mkubwa wa kununua mitambo ya Richmond ili kupambana na hali mbaya ya umeme inayoikabili nchi. Serikali imesema mitambi hiyo ikinunuliwa basi itapunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo kubwa la umeme lililopo nchini." Halafu kwenye kauli kama hizi hukuti jina la mtu hata siku moja kama ni Kikwete au Ngeleja ambaye ametoa kauli hii siku zote itakuwa ni kauli ya lile jinamizi linaloitwa SERIKALI.
 
Mimi niko Mbeya umeme ulikatikatika saa 1:00 jioni mkoa mzima wa Mbeya, nikajua sasa hapa ngoja tusubiri isije ikawa kama alivyosema Askofu KKB kuwa ataombea umeme usiwake,

Kama umeme umekatika Mbeya maana yake hata Iringa itakuwa hivyo.


Mbona nilisikia alishakubali Tanesco wapitishe nyaya karibu na kanisa lake..au alibadili mawazo?

 
Heri yangu mimi basi, kwa mtaji huu. Hata nikirudi Bongo I will still be "running on solar cells"!

Kweli haiingii kichwani.
 
mikoa mbalimbali imeanza kuripoti kurudi kwa umeme.. nadhani hali itakuwa imetengemaa
 
Tungependa hawa CCM watueleze said:

Wewe sasa umechanganyikiwa, yaani waache kujiandaa na uchaguzi waje kukueleza habari za kukatika kwa umeme are you serious! Hivi watanzania mmelogwa?? Kwanza watakwambia watanzania wangapi wanaotumia umeme, sio zaidi ya asilimia kumi, katika hawa wanaopiga kura hawazidi asilimia 18% ya wapiga kura, so wa nini nyie? Imekula kwenu hadi limbwata la CCM litakapo-expire!!
 
Uchaguzi umekaribia kina R.Aziz na EL hawana uhakika wa kurudi Bungeni kwani wamebanwa majimboni mwao sasa wanataka kutumia muda huu kumalizia mambo yao kama vile kuuza hii mitambo mapema ili hata wasiporudi basi Serikali ijayo isiizuie au kuitaifisha hii mitambo iliyokwishajifia.

uwe unaongea mambo ya maana na wewe .sio unakuwa na chuki za kipumbavu na watu.Umeme ukatike unamhusisha Lowassa na Rostam...umaskini wa mawazo kitu kibaya sana
 
Mwaka wa 2010 hakuna umeme! Hii kweli ni ari mpya na nguvu mpya ya kumaliza nchi.

Upepo tunao, kwanini wasitumie wind turbine generators. Halafu mnadai eti mna viongozi na wana taaluma. lol.

Wapige simu siemens ujerumani watawasaidia hawa. Kama hawana number wanipigie simu, nitawasaidia.

Tatizo sio serikali haijui ifanye nini..ukiwapa siemens tender wataishia kufanya kazi coz ni kampuni inayojali reputation yake pia na huwa wanatoa hongo ndogo sana kwa viongozi na chama au no hongo kabisaaaa...kwaiyo inakuwa poa kuunda kampuni feki 100% owned by pesa za walipa kodi na kuilipa. Angalia TRL kwani serikali imeshindwa kuongea na national rail etc etc za uingereza au marekani..lakini waliona bora kuwapa wahndi ambao wakawabail out kwa hela ya walipa kodi...Tanzania umaskini wakujitakia!!
 
uwe unaongea mambo ya maana na wewe .sio unakuwa na chuki za kipumbavu na watu.Umeme ukatike unamhusisha Lowassa na Rostam...umaskini wa mawazo kitu kibaya sana

Unajifanya hujui ni nani katika nji hii anaegombania kwa udi na uvumba kuwa dalali kati ya tanesiko na walaji wa umeme? Ni hawa hawa kina RA na EL!!!
 
Habari zilizothibitishwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Ngeleja zinasema kuwa tatizo la umeme lililoikumba nchi muda mfupi ulipita linatokana na matatizo ya kiufndi kwenye gridi ya taifa na juhudi zinaendelea wakati huu kuhakikisha kuwa hali inatengemaa kabla ya kupambazuka.

Akizungumza nami muda mfupi uliopita Waziri Ngeleja amesema kuwa matatizo kama haya huwa yanaweza kutokea na kwa vile ni ya kiufundi zaidi basi yanahitaji umakini wa hali ya juu kuyatatua na amewahakikishia wananchi kuwa juhudi zote zinafanywa ili kurejesha hali katika hali ya kawaida.

.......

Swali la nyongeza mheshimiwa Ngeleja wakati akiperuzi hii thread, ni kwa nini hakuna backup generators au power station kuserve wakati wa emergencies kama hizi?
 
Lakini hivi kwa nini tuna gridi ya taifa? Kwa nini kila mkoa usiwe na chanzo chao cha umeme? Mimi sijui sana haya mambo ya umeme labda mnaojua mtanielewesha....maana kila kukiwa na tatizo kwenye hiyo gridi ya taifa basi sehemu kibao kunakuwa hakuna umeme...WTF?
 
Mambo ya Kakobe hayo yameanzaa alisema maajabu yatatokea, ndio hayo sasa. Alikuwa anazumzingia ule umeme wa pale Tanangozi leo Mchana
 
Habari zilizothibitishwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Ngeleja zinasema kuwa tatizo la umeme lililoikumba nchi muda mfupi uliopita linatokana na matatizo ya kiufndi kwenye gridi ya taifa na juhudi zinaendelea wakati huu kuhakikisha kuwa hali inatengemaa kabla ya kupambazuka.

Akizungumza nami muda mfupi uliopita Waziri Ngeleja amesema kuwa matatizo kama haya huwa yanaweza kutokea na kwa vile ni ya kiufundi zaidi basi yanahitaji umakini wa hali ya juu kuyatatua na amewahakikishia wananchi kuwa juhudi zote zinafanywa ili kurejesha hali katika hali ya kawaida.

"Siyo tatizo la sehemu sehemu tu, ni tatizo la system nzima ya gridi yetu na mafundi wetu wako kazini sasa hivi kurejesha hali katika hali ya kawaida" amesema Bw. Ngeleja.

Wakati huo huo nilitumia muda huo kumpa pongezi kwa jinsi alivyosimamia suala la Kakobe na Nguzo za umeme na hatimaye kuifanya serikali ichukue msimamo badala ya kuyumbishwa kirahisi. Nilimhakikishia kuwa Watanzania wanataka kuona serikali yao inachukua maamuzi badala ya vikao visivyoisha hasa kwenye mambo ambayo uamuzi unahitajika haraka.
MM Naomba Number ya Ngeleja
 
Back
Top Bottom