Baada ya kukatika nchi nzima; umeme warejea!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Habari zilizothibitishwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Ngeleja zinasema kuwa tatizo la umeme lililoikumba nchi muda mfupi uliopita linatokana na matatizo ya kiufndi kwenye gridi ya taifa na juhudi zinaendelea wakati huu kuhakikisha kuwa hali inatengemaa kabla ya kupambazuka.

Akizungumza nami muda mfupi uliopita Waziri Ngeleja amesema kuwa matatizo kama haya huwa yanaweza kutokea na kwa vile ni ya kiufundi zaidi basi yanahitaji umakini wa hali ya juu kuyatatua na amewahakikishia wananchi kuwa juhudi zote zinafanywa ili kurejesha hali katika hali ya kawaida.

"Siyo tatizo la sehemu sehemu tu, ni tatizo la system nzima ya gridi yetu na mafundi wetu wako kazini sasa hivi kurejesha hali katika hali ya kawaida" amesema Bw. Ngeleja.

Wakati huo huo nilitumia muda huo kumpa pongezi kwa jinsi alivyosimamia suala la Kakobe na Nguzo za umeme na hatimaye kuifanya serikali ichukue msimamo badala ya kuyumbishwa kirahisi. Nilimhakikishia kuwa Watanzania wanataka kuona serikali yao inachukua maamuzi badala ya vikao visivyoisha hasa kwenye mambo ambayo uamuzi unahitajika haraka.
 
asante mwanakijiji......Mungu atusaidie isije ikawa kama Zanzibar
 
Uchaguzi umekaribia kina R.Aziz na EL hawana uhakika wa kurudi Bungeni kwani wamebanwa majimboni mwao sasa wanataka kutumia muda huu kumalizia mambo yao kama vile kuuza hii mitambo mapema ili hata wasiporudi basi Serikali ijayo isiizuie au kuitaifisha hii mitambo iliyokwishajifia.
 
Huo ni mgao hawataki tu kusema ukweli wao walishaona hamna mtakachofanya laleni gizani mapaema kesho muwahi kazini hao ndio wabongo
 
Kweli aisee,imenibidi nichungulie nje ni giza tupu,duuuuh bahati nzuri hapa nilipo waliwasha jenereta chapchap,hivyo sikunotice kuwa umeme umekatika .asante....naona huko nje sehemu sehemu kabali njenje.
 
Mwaka wa 2010 hakuna umeme! Hii kweli ni ari mpya na nguvu mpya ya kumaliza nchi.

Upepo tunao, kwanini wasitumie wind turbine generators. Halafu mnadai eti mna viongozi na wana taaluma. lol.

Wapige simu siemens ujerumani watawasaidia hawa. Kama hawana number wanipigie simu, nitawasaidia.
 
hapa nilikuwa nataka kuwapigia simu nilidhani ni mtaa wetu tu! Ngoja nitulie kumbe ni janga la kitaifa
 
Mwenye taarifa alete habari hapa nini kinaendelea na giza hili

tatizo linakuwa ni kwamba kila mtu anajua ni maeneo yake tu...sisi tuna bahati Mwanakijiji ametufumbua macho...so tusubiri alete data
 
Max.. wakitatua tatizo la nishati wao watakula wapi?

Kwahiyo hawa jamaa hawapendi wanachi wao.

Waarabu wa Dubai walienda Munchen Ujerumani, wakapewa utalaam wa production ya umeme kupitia wind. Sisi bado tupo tuaendelza ufisadi kupitia kampuni ya kuchapa vitabu ya Richmond na kutumia maji ya kunywa.

Mungu saidia watanzania.
 
Yanatengenezwa mazingira ya 'dharura' hapo...Hivi ni lini kutakuwa na umeme wa uhakika Tanzania??Maana watumiaji ni proportion chache tu ya raia wote,ile kuwakidhi hao tu nalo limekuwa shida.Where is da vision mr president?Ngeleja?Rashid(if u r stil there)?
 
Mkjj hakuna tena cha kustaajabisha kuhusu swala la umeme Tanzania. Tatizo la umeme lilianza rasmi mwaka 1992 na hadi hii leo miaka 18 baadaye na Marais watatu tofauti, hali ya umeme bado ni mbaya na hakuna dalili zozote za kupata uvumbuzi wa kudumu kuhusu swala hili na kwa maoni yangu hali siku za usoni itazidi kuwa mbaya sana. Kama unajiweza sasa ni wakati muafaka wa kujizatiti ili kuanza kutumia umeme wa jua na kuachana na matatizo chungu nzima ya TANESCO.
 
Kwahiyo hawa jamaa hawapendi wanachi wao.

Waarabu wa Dubai walienda Munchen Ujerumani, wakapewa utalaam wa production ya umeme kupitia wind. Sisi bado tupo tuaendelza ufisadi kupitia kampuni ya kuchapa vitabu ya Richmond na kutumia maji ya kunywa.

Mungu saidia watanzania.

Mkuu tulishaambiwa kwamba Kikwete katika awamu yake ya kwanza katimiza yale yote yaliyokuwemo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005. Nadhani asilimia kubwa ya yaliyokuwemo kwenye ilani hiyo ni kuwakingia kifua mafisadi wote kuanzia Mkapa, Rostam, Karamagi, Iddrisa Rashid, Mzee wa Vijisenti na wengineo wengi. Ingekuwa nchi nyingine uchaguzi wa mwaka huu CCM ingekiona cha mtema kuni kilimchotoa kanga manyoya kwa kuwadharau kabisa wapiga kura, lakini kwa nchi yetu watashinda tena kwa kishindo kikubwa na kurudi tena madarakani kiulaini kabisa. Mungu inusuru nchi yetu.
 
Back
Top Bottom