Baada ya Azam TV Kuingia mkataba na TFF Wa Miaka 10, naona wamepandisha Bei za vifurushi vyao

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,238
Wakuu Chief Hangaya Anaupiga Mwingi.

Sasa Azam Tv Baada ya Kuona Wenzao Dstv wamepandisha vifurushi vyake mwezi Uliopita(Wa September) basi na wao AzamTv wamepandisha vifurushi vyake.

Kile kifurushi tulichokuwa tunalipia elfu20 Kwa ajili ya Kuona Mpira Wa Ligi Kuu sasa ni elfu25!

Kile cha Azam play tulichokua tunalipia elfu 28 Sasa ni elfu 35..

Je Shida ni Kodi na Tozo au shida Ni Nini?

All in All Tutafika tuu, Maana Hakuna tena mtetezi wa walaji wa mwisho.

R.I.P Mjuba Magu
 
Sasa hayo mambo mengine ni starehe, mkisema kila kitu serikali iingilie itakuwa tabu, hizo ni biashara za watu, unafikiria alipoamua kuweka bilioni 250, ni mchezo?

Na yeye anategemea sana mipira hii ligi kuu.tumeshindwa kusikilizwa kwenye huduma za msingi kama mawasiliano , utegemee huko kwenye starehe?!!kama huwezi huko kuwakomoa usilipie tu.
 
Ukishindwa kulipia unaacha, wakiacha kulipia watu wengi wao wenyewe watashusha bei...

Kuna mambo mengine si lazima serikali iyapambanie, hulka tu za wananchi zinatosha kushape baadhi ya mifumo haswa hii ya huduma zitolewazo kwa kutegemea pesa za wananchi...
 
Ukishindwa kulipia unaacha, wakiacha kulipia watu wengi wao wenyewe watashusha bei...

Kuna mambo mengine si lazima serikali iyapambanie, hulka tu za wananchi zinatosha kushape baadhi ya mifumo haswa hii ya huduma zitolewazo kwa kutegemea pesa za wananchi...
Watu wanalia hata kwenye mambo ya starehe. Hawajui starehe gharama. Mbona K Vant imepanda bei lakini walipa kodi hatujalalamika?
 
Sasa hayo mambo mengine ni starehe, mkisema kila kitu serikali iingilie itakuwa tabu, hizo ni biashara za watu, unafikiria alipoamua kuweka bilioni 250, ni mchezo, ?na yeye anategemea sana mipira hii ligi kuu.tumeshindwa kusikilizwa kwenye huduma za msingi kama mawasiliano , utegemee huko kwenye starehe?!!kama huwezi huko kuwakomoa usilipie tu.
So Kisa ni bizinezi za Watu basi wasiwe regulated? Sasa ni Wakati upi mlaji anakuwa secured na Serikali?
 
Kama vipi unaacha kulipia, unaangalia bure TBC ili unufaike kuangalia mema aliyofanya "mungu" wako aliyededi, bwana mwendazake
 
Back
Top Bottom