Azam tv sio burudani kwa wote ni burudani kwa waturuki. Mnaboa sasa

Nyanzige30

Member
Mar 18, 2024
91
224
Kwa sisi wapenzi watazamaji wa Azam Tv wapenzi wa tamthiliya hasa pale Azam Two hakuna tena burudani kwa wote bali burudani kwa Waturuki. Tamthiliya zinazorushwa na Azam Tv zinachosha mana zinajirudia rudia tu kuanzia visa mpk wahusika.

Hv kuna tofauti gani Kati ya Ertugurul, The Othoman, Barabarosa na Alpasaran? Zote ni mapanga na mishale, zote wahusika wakuu wanaua wahusika 1000 wakati wao wako watatu, Zote wahusika wakuu hata wapigwe risasi hawafi lkn wengne mlio wa risasi tu wanakata kauli, Zote wanawake wa wasioamini (Kwa mujibu wao) wanabadili dini kuolewa na wahusika wakuu, Zote zinapigania haki na kuushinda Ukristu, Zote lengo ni moja.

Twende kwa wahusika.. Achana na kujirudia kwa Ertugurul mpk Baba Oruc kuna kale katoto mara Kaitwe Melisa kwenye Melisa,Pelin kwny Husband Family,Okyu kwny Kizim.. Yani muhusika mmoja ikiisha tamthiliya hii inakuja nyinge yy ndo mhusika mkuu kla sku. INACHOSHA SIO BURUDANI TENA

Saa moja tamthiliya ya Kituruki, Saa 3 ya Kituruki, Saa 4 ya kituruki kwani hakuna mataifa mengne yenye tamthiliya za maana mkafasili mkatuwekea tuburudike km ilivyokuwa kwa Ruby Ring? (Nadhani ndo tamthiliya pekee isiyo ya Kituruki kuruka pale Azam Two sa 3 Usiku.

Wakuu km mmeingia ubia na Uturuki semeni tutafute ving’amuzi vingine! Uturuki tushaijua na dini tushaijua pia.

OVER.
 
Mkuu umechafukwa, mnatoa wapi muda wa kuangalia madudu hayo, na huku mnaishi chini ya dola moja
GK5MZLBXYAAhfwb.jpeg
 
Back
Top Bottom