AZAM MEDIA hakikisheni watangazaji wenu (Baraka mpenja,Patrick Nyembera n.k) wanapata elimu ya msingi kuhusiana na michezo wanayoitangaza mubashara

ToniXrated

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
1,135
2,976
Amani iwe nanyi.

Nikiwa kama mdau wa michezo, napenda kuishauri kampuni ya habari ya AZAM kuhakikisha kuwa uwekezaji wao wanaoufanya katika tasnia ya michezo unaendana sambamba na kuwapa elimu ya msingi (basic education) watangazaji na wachambuzi wao.

Niipongeze kampuni ya Azam Media katika juhudi zake za kufufua michezo ya mpira,ndondi n.k ila inatakiwa ishirikiane na vyama vya michezo husika katika kuwapa elimu hawa watangazaji wao kina Baraka Mpenja,pascal kabombe,iddi salum,hashim ibwe,patrick Nyembera n.k kuhusiana na michezo wanayoitangaza.

Kama mtangazaji anatangaza kuhusu masuala ya mpira mathalani mechi basi awe na elimu ya awali kuhusiana na mpira na si kutangaza tu fulani kachukua boli kampa yule, mayele katetema, sakho kanyunyiza n.k

MaJuzi kuna tukio lilitokea kwenye boxing katika mechi ya Mandonga dhidi ya Salum Abeid, Mandonga aliangishwa chini ,Refa akawa anamtoa mpinzani wa mandonga asiendelee kumshambulia mandonga akiwa chini.Huku watangazaji wakawa wanapayuka kuwa refa hafai ,afungiwe n.k kwanza katika ethics za utangazaji huwezi kusema refa afungiwe kwasababu huna mamlaka hayo. Tunaona blunders zikifanywa na marefa wa Epl ila huwezi kumsikia mtangazaji kama Peter Drury akipayuka kuwa marefa wafungiwe n.k.

Hivyo basi kampuni ya Azam Media ihakikishe watangazaji wake wanapatiwa elimu juu ya michezo wanayoitangaza kabla hawajashika microphone au wahakikishe kuwa wanaweka mtangazaji namba mbili ambaye atakuwa akisaidiana na hawa watangazaji kuchambua aspects of the game kama sheria, masuala ya kimbinu n.k. kama wanavyofanya katika mataifa yaliyoendelea kimichezo huko ulaya na America.

Mechi za ulaya hutangazwa na watangazaji wawili , wa kwanza huwa ni mtangazaji wa kawaida ila mtangazaji wa pili ni lazima awe alicheza soka la kulipwa au ana taaluma ya ukocha mfano mzuri ni Andy Townsend anayefanya uchambuzi wakati mechi inaendelea. Ina maana ana uwezo wa kuelezea mabadiliko ya kimbinu yanayofanywa na makocha n.k

Hata katika boxing/basketball lazima wawepo watangazaji ambao walikuwa ni wachezaji hapo kabla au makocha. Mfano mzuri ni combination ya Jesse john na marehemu Mwalimu Kashasha.

Ni hayo tu.
 
Baraka mpenja huwa anahama kwenye tukio husika pale camera ikimwonyesha mwanamke siku hizi mnaita pisi Kali

utamsikia " waooooo tazama mauaa,mtoto mzuri kabisa naye anafatilia kabumbu" mwenzie Gharibu mzinga anaconcentrate na mpira tu
Very unprofessional kwa kweli . Inatakiwa wapewe elimu juu ya michezo wanayoitangaza. Nashangaa sana kuona kila mchezo wanatangaza ..mtangazaji wa mpira unamkuta anatangaza ngumi,mara anatangaza basketball n.k kwa wenzetu huwezi kukuta mtangazaji wa mpira akatangaza ngumi ,tennis,cricket,basketball hata siku moja.
 
Broadcast journalism ni kozi kabisa inayotolewa katika vyuo vikuu huko ulaya na america. Watu wana specialize katika sports commentary...mtangazaji anatakiwa aufahamu mchezo wenyewe hususani elimu ya msingi ,sheria na kanuni za mchezo na pia awe na maadili ,ajue do and don'ts za utangazaji sio kupayuka payuka tu.
 
The best commentator kwa kizazi cha sasa ni Ghalib Mzinga

Anajua taarifa nyng sana kuhusiana na kila mchezaji atakaecheza, historia ya makocha wa hizo timu, historia ya refarii na records zake, historia ya nchi na ukanda wa klabu zinapotokea nk nk

Kwa kifupi jamaa huwa anajiandaa vya kutosha, huwa anachimba taarifa za kutosha za washiriki ktk gemu husika

Much appreciation kwake, huwa naburudika sana nikimsikia akitangaza
 
Aisee hili swala bila shaka limenikera San na leo niliikutana na Patrick nyembera maeneo ya oceans road anatembetembe fukweni kidgo nimzabe makofi yaani almanusura

Jana yule refa aliyechezesha pambano la mandonga na abed bwan mkarafuu alililielezA ktk kipindi Cha wasafi areana jamaa aliweza kutoa ufafanuz juu ya tukio lile namm nikabaki mdmo wasi jmaaa Ni mtaalamu haswa haswa kwanza ndio mwenyekit wa waamuzi wa ngumi za kulipwa nchini hvyo huo mchezo anaujuwa vzr mnoo na kujuwa sheria zake Ila mazuzu kina nyembera hawajui kitu

Alieleza tukio zima na kusema kuwa hana makosa yoyote katk lile Jambo kwani maboxer ndio walikuwa hawajui sheria za ngumi hvyo kumpeleka yey kuanza kufundisha sheria wakt huohuo afanye maamuzi hvyo aliwalaumu Sana wachambuzi kina nyambera kuwa hawaujui mchezo huo na Wala hawajui sheriaaa yoyote

Jmaaa yule mkarafuu nimependa mno kwanza Ni msomi mzuri wa sheria na language inapanda mbaya

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Yule refa wa pambano la mandonga alipuyanga na tayari ameshafungiwa
Haiwezekani mandonga aangushwe chini na clear punch halafu anamuacha aamke bila kumhesabia
Mandonga alimsukuma mpinzani wake akaanguka chini huyo refa akaenda kumhesabia
Inawezekana jamaa ni mtaalamu ila aliamua makusudi kufanya yale madudu
 
Back
Top Bottom