Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,482
- 24,592
Ukandarasi maana yake ni kufanya kazi kwa ajili ya mtu mwingine (sasa ni serikali), kimkataba.
Makandarasi ni kada iliyoenea nchi nzima, na kada hii imetumika sana katika kampeni Awamu ya Nne ili kuiingiza Awamu ya Tano madarakani.
Sasa hivi siyo siri makandarasi wanadhalilika na kudharauliwa.
Umoja wa makandarasi ulitoa masikitiko hivi karibuni juu ya mtizamo hasi unaoonyeshwa na viongozi wa Awamu ya Tano lakini muda mfupi baadaye tukaona ya Jaffo.
Waswahili walisema tenda wema usingojee shukrani na kwa makandarasi wajijue kuwa akili ni mukichwani mwao.