Askofu Zakaria Kakobe: Tanzania siyo nchi ya chama kimoja! Amtaka Rais Magufuli atubu

Askofu Zakaria Kakobe leo akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, amenukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu" amenukuliwa akisema Kakobe.

Huwa sielewi ni kwa nini Hapa JF mtu anapewa likes nyiiingi bila kujali kudadavua maelezo yaliyoko mbele yetu. Maelezo kama haya yanayoitwa ya Kakobe yana nini hadi useme 'like' Yaonekana maisha yametulamba tunatafuta wanaotusaidia kulia.

Ni vizuri kutoa ushauri lakini lazima ujue unatoa ushauri kwa nani. Kakobe anatoa ushauri kwa Rais wa nchi kama mtu anayetoa ushauri kwa muumini wake, maana wahubiri wa aina hii humiliki watu. Bado hajapata funzo la makosa yake ya tangu enzi zile za kukosana na umoja wa vijana wa CCM, kukosana na serikali juu ya umeme na redio yake, utabili wake wa kutangaza mteule wa Mungu, nk. sasa anakuja na matusi kwa Rais. Mi nayaita matusi maana suala la kutubu ni kutangazia umma kwamba rais ni muovu.

Yeye Kakobe ni msafi kiasi gani hadi atangaze kutubu kwa rais. Baadhi mutaunga mkono kwa kero zenu lakini nionavyo jamaa huyu anatafuta sababu ya kutaka ajulikane. Yeye si Nabii kama anavyotaka tujue. Ni mtu wa kawaida na huenda wa hovyo kama tulioko sokoni tukigusa mifuko ya watu.

Kwa akili yangu tu; Tangu Kakobe ameanza kuhubiri, faida gani imeingia hapa nchini zaidi ya kupumbaza watu. Ni kama yule mwingine wa Kimara. Hajajenga shule, hajajenga hospitali, hana lolote la kusaidia umma. Yapo madhehebu yenye nguvu hizi kwa jinsi yalivyosaidia umma wa TZ. Ngoja tusubili atangazwe shujaa.
 
Ukimwangalia huyu DC Happy kila kitu kinaonesha ni jikedume.....!!Ndo maana alimwandama Halima Mdee, si unajua jinsia za kike ambavyo huwa wanawekeana mikwara...??Kwa Kakobe hana ubavu huo maana huyo ni mwanamme wa shoka....!!
Cyo jikedume...yule ni jike
 
Duh we patriot kwa hiyo unasema ukishakuwa rais we ni mtakatifuna wasiwasi na maharage uliyokula
 
Askofu Zakaria Kakobe leo akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, amenukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu" amenukuliwa akisema Kakobe.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu
 
Kanisa hili la FGBF pamoja na muasisi wake lilianza vizuri sana. Lilionesha dhahiri kuwa tengenezo kwa makanisa mengine ya Kipentekoste hivyo likajidhihisha kuwa ndiyo haiyumkiniki Kanisa lililo mpango wa wazi wa Mungu. Usingemsikia muasisi wake au wasaidizi wake wakijiingiza kwenye suala lolote lililo nje na kuwahubiri watu waje kwa Bwana Yesu kristo. Aidha, Kanisa liliwakataza kabisa washirika wao kujichanganya ktk siasa. Wao waliazimu Full Gospel tu. Kwa kweli wakati ule nakiri hakukuwa mtumishi wa Mungu mfano wa Bishop Kakobe. Kanisa likakua kama uyoga kwa kuwa na matawi Nchi nzima. Ilipendeza sana. Wakristo kwa waabudu mizimu wakampokea Bwana Yesu kristo huku wakiziacha imani na dini na madhehebu yao. Hakika nguvu za Bwana Yesu kristo zilijidhirisha bayana ktk FGBF. INASIKITISHA, kanisa hili sasa ni kama CHADEMA. lina kila dalili ya kupoteza vision yake. Ukitaka kuhakikisha juu ya hili Ninaloshuhudi njoo huku mikoani. Makanisa mengi yamebaki tupu. Washirika 'wamekimbia'. Moja ya sababu: wachungaji wa Kanisa hili kujihesabia haki na wanafikiri 'utaua ni njia ya kujipatia mali na heshima. Hawana mahusiano mazuri na watumishi wa Mungu wa makanisa mengine. Wanadhihaki na kubeza. Ndiyo ustaarabu wao. Ushauri wangu kwa kaka yangu na kiongozi wangu archbishop Kakobe: Rudia misimamo na mitazamo yako ya awali. Ungeendelea vile Huduma ya FGBF ingekuwa kubwa kuliko zote hapa Tz. Mimi binafsi nakukubali sana Ila hii misimamo uliyoanza kuonesha, mh! naingiwa na shaka kidogo. Achana na Serikali za Dunia hii. Achana na siasa kaka yangu. Nu bhileke ni bhulandage! Hubiri fundisha. Nakumbuka mpaka madhehebu na dini nyingine walikuwa wanafundishia masomo yako. Ulikuwa unatisha mzee! Yatengeneze upya makanisa yaliyopo mikoani. Yanakuchafua image yako nzuri. Mojawapo ya hatua za kuchukuwa ni kuwabadilishia vituo wachungaji. Wamekaa sana sehemu moja kwa muda mrefu. Jambo hili linaathiri utendaji wao. Haya, huu ni ushauri tu kama Yethro alivyomshauri mkwewe Musa. Najua wapo washirika watabeza kama CDM ambavyo wamekuwa wakibeza shauri wanazopewa na wenye hekima. Matokeo yake Chama kinasambaratika na badala ya kuchukuwa hatua stahiki wanalaumu vyama vingine vya siasa.
 
Labda kwenye hifadhi ya barabara watampatiaa .lakini uraia itakuwa ngumu maana mwenyewe Kakobe alikuwa afisa uhamiaji kabla aje kuwa muhubiri
Hata kwenye hifadhi ya barabara hawatamuweza kwani ili kung'oa jengo la kanisa lake itabidi pia ile maternity dispensary ya kanisa katoliki ing'olewe! Bishop Kakobe songa mbele babaa!! Haki huinua taifa!!!
 
Huwa sielewi ni kwa nini Hapa JF mtu anapewa likes nyiiingi bila kujali kudadavua maelezo yaliyoko mbele yetu. Maelezo kama haya yanayoitwa ya Kakobe yana nini hadi useme 'like' Yaonekana maisha yametulamba tunatafuta wanaotusaidia kulia.

Ni vizuri kutoa ushauri lakini lazima ujue unatoa ushauri kwa nani. Kakobe anatoa ushauri kwa Rais wa nchi kama mtu anayetoa ushauri kwa muumini wake, maana wahubiri wa aina hii humiliki watu. Bado hajapata funzo la makosa yake ya tangu enzi zile za kukosana na umoja wa vijana wa CCM, kukosana na serikali juu ya umeme na redio yake, utabili wake wa kutangaza mteule wa Mungu, nk. sasa anakuja na matusi kwa Rais. Mi nayaita matusi maana suala la kutubu ni kutangazia umma kwamba rais ni muovu.

Yeye Kakobe ni msafi kiasi gani hadi atangaze kutubu kwa rais. Baadhi mutaunga mkono kwa kero zenu lakini nionavyo jamaa huyu anatafuta sababu ya kutaka ajulikane. Yeye si Nabii kama anavyotaka tujue. Ni mtu wa kawaida na huenda wa hovyo kama tulioko sokoni tukigusa mifuko ya watu.

Kwa akili yangu tu; Tangu Kakobe ameanza kuhubiri, faida gani imeingia hapa nchini zaidi ya kupumbaza watu. Ni kama yule mwingine wa Kimara. Hajajenga shule, hajajenga hospitali, hana lolote la kusaidia umma. Yapo madhehebu yenye nguvu hizi kwa jinsi yalivyosaidia umma wa TZ. Ngoja tusubili atangazwe shujaa.
Povu
 
Nitakapo wasikia bakwata ndio nitaamini magufuri raisi wa ovyo lakini Hawa maaskofu matumbo sina imani nayo kabisa
Ulishasikia magufuri kaenda kusali FG kwa kakobe?
Kwa nini hajaenda?

Ukikosa majibu hebu ulizia kwa wachochezi watakupa majibu sahihi
 
Kaongea rubbish kama wapinzani wanavyoongea aongee kama kiongozi wa kiroho ...asitumie jukwaa LA dini vibaya eti magufuli atubu yeye ni nani mazambi yake hayaoni !? maana keshamuhukumu Rais wakati yeye mwenye anamadhambi tena mengi penhine kuliko ya Rais ...imeandikwa usihukumu ili na wewe usihukumiwe..kwa nn unaona kibanzi cha mwenzio angali jichoni mwako kuna boliti na hujioni?!
Angesifia wala haya yote yasingekuwepo.ametimiza wajibu wajibu wake kama mtanzania mzalendo,pili kama kiongozi wa kiroho niwajibu wake kukemea maovu kuonya/kukanya jamii yake.ameepuka unafiki.amethubutu,maana nchi nzima imepigwa ganzi.wanaona jahaz letu linaenda mrama hawastuki.wote wanaogopa kusema ysliyo moyoni wote wamejaa unafiki.hata mfalme akikosea wanamsifia tu maana ndicho kirevi akipendacho mfalme.Historia itamkumbuka.
Wakati Hitra anaanza wengi waliagukia kwenye mahaba nae ya kinafki kiasi hata kuwapiga ganzi viongozi wa dini.kanisa halikuwai kumkosoa hata siku moja.kanisa likapata aibu kuu kwa kumnyamazia kiongozi huyo wa Nazi.papa John II alipotembelea moja ya kambi zilizokuwa za mateso uko poland katika hotuba yake akauliza kwa nini kanisa lilinyamaza?mwisho akaomba radhi kwa niaba ya kanisa.ni suala la muda tu.
 
Back
Top Bottom