Kukosoa wanasiasa haiwezi kuwa ‘UDINI’

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,503
86,053
Katika pita pita zangu nimekutana na ka' makala kadogo hivi, kazuri kameandikwa na Buyobe wa Twitter. Nikaona si dhambi kukaweka hapa Ili wale wanaotetea "upumbavu" wa CCM Kwa minajili ya "UDINI" wakumbuke hili nalo.

Tarehe 25 December 2017, Askofu Zakaria Kakobe akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, alinukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu"

Baada ya kauli hii, Askofu Kakobe alipokonywa passport yake, alihojiwa uraia wake na aliandamwa na TRA kwa madai ya kodi.

Huyu alikuwa ni kiongozi wa dini ya Kikistro na alimkosoa Mkristo Magufuri

Huu ulikuwa udini? Wa dini gani?

Askofu wa Catholic Jimbo la Rulenge (Severine Niwemugizi) alimkosoa mkatoliki mwenzake Magufuri juu ya haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano.

Aliishia kupokonywa passport na kuhojiwa uraia wake.

Alikuwa mdini? Akishabikia dini gani?

Nachukizwa sana na yeyote ambaye atataka kutugawa kwa misingi ya kidini.

Kukosoa haiwezi hata mara moja kuwa udini.

Kuwa kiongozi wa dini hakumnyimi haki kiongozi huyo kupata haki zake za kikatiba kutoa maoni juu ya mambo ya nchi yake kama anavyoweza kufanya Mwalimu, daktari, mkulima au mfugaji.

Tukemee wale wote wanaotaka kujificha kwenye udini pale tu wanapokosolewa kwa makosa waliyoyafanya wenyewe.

Mungu Ibariki Tanzania na watu wote.

Uhuru, Umoja na Amani

From your commander of the hand to mouth battalion

A dull, Colorless and Clueless old man now chewing Mugombero the turbo charger.

Hii ni copy and paste

View: https://twitter.com/fbuyobe/status/1693344546560630858?t=7iwxWIHRnifJmbr1Oh8RyQ&s=19
 
Tarehe 25 December 2017, Askofu Zakaria Kakobe akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, alinukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".
Nayakumbuka mahubiri yake hayo Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko?
P
 
Upande wa pili kwa maana ya Waislam, wao huwezi kuwasikia wakimsema Muislam mwenzao hata kama kakosea. Mfano halisi ni hili suala la Mkataba wa hovyo kati ya nchi yetu na kampuni ya DP World. Hakuna hata mmoja uyamsikia kwenye vyombo vya habari akikosoa, pamoja na kwamba wanajua ni mkataba mbovu kabisa kuwahi kutokea duniani!

Upande wa pili, mtu wao ni malaika, hakosei!

Ndo maana hata siku moja, huwezi kuwakuta kama kundi (ukiachilia mbali wanasiasa kama Prof. Lipumba), wakikosoa mambo ya hovyo yanayofanywa kwenye serikali ya ndugu yao s100.
 
Wengi wanaoleta habari za udini huku wanafanya makusudi tu Ila ukweli wanaijua,hata kipindi cha Magufuli kanisa halikukaa kimya. Tena bakwata ndiyo ilikua nae bega kwa bega,kuna shehe wa zamani wa mkoa wa Dar mpaka alimfananisha Magufuli na Mungu.
 
Upande wa pili kwa maana ya Waislam, wao huwezi kuwasikia wakimsema Muislam mwenzao hata kama kakosea. Mfano halisi ni hili suala la Mkataba wa hovyo kati ya nchi yetu na kampuni ya DP World. Hakuna hata mmoja uyamsikia kwenye vyombo vya habari akikosoa, pamoja na kwamba wanajua ni mkataba mbovu kabisa kuwahi kutokea duniani!
View attachment 2723459
Asili ya wanafiki ndio ilivyo, hawaambiani ukweli
 
Halafu mbona haya masuala ya udini huwa yanaibuka zaidi pale Muislam anapokuwa Rais?

Halafu waanzilishi wa haya mara nyingi ni wao wenyewe?!

Mbona kipindi cha Hayati Mwl. JKN, Hayati BWM na Hayati Dk.JPM haya mambo ya kipu,mbavu ya udini hayakuwepo?!
 
Inferiority complex tu
 
Wanasiasa watatumia mbinu zozote kuendelea kubaki madarakani na kuendelea kuramba asali. Hili la udini ni moja ya mbinu yao chafu lakini effective sana. Bahati mbaya hali ikifika hapa huwa huko mbele inazidi kuwa mbaya badala ya kuboreka.
 
Ndugu yangu Wakili wa Shetani, shetani anasemaje kuhusu hili?
 
Upande wa pili kwa maana ya Waislam, wao huwezi kuwasikia wakimsema Muislam mwenzao hata kama kakosea. Mfano halisi ni hili suala la Mkataba wa hovyo kati ya nchi yetu na kampuni ya DP World. Hakuna hata mmoja uyamsikia kwenye vyombo vya habari akikosoa, pamoja na kwamba wanajua ni mkataba mbovu kabisa kuwahi kutokea duniani!
View attachment 2723459
mfano halisi ni Zito, now yupo kimyaa
 
CCM waliwaita viongozi wa dini kuwaelezea mambo ya mkataba wao wa kubumba wa DP WORLD huku wakijua kuwa kuwashirikisha viongozi wa dini ktk mambo yao ni kuchannganya Dini na Siasa.

Viongozi hao hao walio alikwa na CCM katika mambo ya siasa wametoa waraka kwamba hajaelewa mkataba wa kimangungo ccm wanalalamika kuwa viongozi wa dini wasifanye siasa na dini.

Hivi hao viongozi wa Dini wangeandika waraka kwa waumini wao kuukubali huo Mkataba wa ki Mangungo haya mafisadi ya CCM wangenuna?

Mbona Wakati wa Magufuli KKKT walitoa waraka wa pasaka kupinga mauaji na uonevu pia TEC walitoa waraka hakuna aliye simama kusema kuwa Magufuli anakosolewa kwa sababu ya Ukristu wake?

Askofu Niwemugizi, Askofu Shoo, Askofu Bagonza, na Kakobe walimkosoa vikali Magufuli mpaka kupelekea kuhojiwa uraia wao Askofu Kakobe alipekewa hadi TRA kwa nini hamkumtetea dini ya Magufuli?

Magufuli alijenga hadi msikiti mkubwa kwa waisilamu hapakuwa na kelele zozote kwa nini anawajengea waislamu msikiti au anachanganya dini na siasa.

Askofu Gwajima ana kanisa lake nchi nzima na nje ya nchi pia ni kiongozi wa ccm hata mama Lwakatare alikukuwa na kanisa lake. Hawa wanaitumikia CCM na pia Mungu kwa wakati mmoja hakuna anayesema wanachanganya dini na siasa.

Na hoja ya udini CCM wanaitumia pindi hasa Rais akiwa muislamu na wamekosa hoja zenye mashiko,mbona Magufuli alipokuwa anapingwa hadi akawa anatumia Bunduki kuzima upinzani kwa nini hakutetewa kuwa anapingwa kwa sababu ni Mkristo?

Maendeleo hayana vyamaa.
 
Back
Top Bottom