Askofu moses kulola kada wa ccm?

kamanzi

Senior Member
Oct 28, 2007
100
23
Nianze kwa kusema namuheshimu Askofu Kulola kama mtumishi kamili wa MUNGU. Kama utumishi Tanzania, ameufanya na hakuna swali katika hilo.

Lakini lazima niseme kuwa u-CCM wake unatia kinyaa sasa maana amezidi. Wakati wa uchaguzi alikemea kila mtu aliyeonekana kama anashabikia CHADEMA. Akaweka mkutano mkubwa sana pale Biafra Kinondoni akielezea kwanini bila CCM nchi itaingiwa na vita. Hata pale Askofu mwenzie, Kakobe aliposhauri washirika wake waende ibada jumamosi ili jumapili waitoe kwa ajili ya kupiga kura, Kulola alimtusi vibaya sana. Namnukuu maneno yake akisema, "wanaosema washirika waende kupiga kura jumapili wamelaaniwa". Hapo hapo akatangaza kwa wachungaji wa kanisa lake la EAGT (mimi nilidhani linatakiwa kuwa la Mungu) kuwa yeyote atakayefuata wazo la Askofu Kakobe ambaye alimuita "pepo" atashughulikiwa. Mimi najiuliza hivi huyu mzee haoni aibu? Waliposema JK ni chaguo la Mungu tuliwakubalia matokeo yake JK kaua nchi. Leo hii hatudanganyiki tena maana inaelekea wengi wanafikiri kwa kutumia matumbo kama Mrisho Gumbo alivyosema.

Kwa yeyote ambaye hajasoma utumbo huu, tafadhali soma habari hapo chini iliyotokea katika gazeti la Habari Leo.

Askofu: Muombeeni Kikwete, msimwandame

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT), Moses Kulola, amewataka Watanzania kumwombea Rais Jakaya Kikwete katika kazi zake na waache kumwandama kwani ana mzigo mkubwa wa kufikiria wananchi.

Aidha, amewataka Watanzania kutokubali kushawishika na mtu yeyote, ili kujiepusha kusababisha uvunjifu wa amani huku akisisitiza kuwa nchini hakuna maisha magumu ikilinganishwa na nchi jirani.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam , Askofu huyo alisema umefika wakati wa Watanzania kuweka pembeni ushabiki wa kisiasa na kuungana kumwombea Kikwete ili nchi ibarikiwe na Mungu, kwani utawala unaruhusiwa na Mungu anayeuweka na kuuondoa.

Amesema, ameamua kutoa rai hiyo kwa Watanzania akiwa ni kiongozi wa dini kutokana na jinsi anavyoona uvunjifu wa amani unavyotokea katika nchi nyingine, hivyo Watanzania waepuke kushawishiwa na kujiingiza katika vurugu zitakazosababisha kuvunjika kwa amani.

Amesema, Kanisa lake lina wanachama wa vyama tofauti, lakini katika kuhakikisha amani iliyopo inalindwa kwa maslahi ya Watanzania wote, inapaswa kuwa kitu kimoja katika kumwomba Mungu.

Amesema, hali hiyo inatokana na kuwa Mkuu huyo wa Nchi halali na usiku kucha roho yake inatapatapa nchi nzima kuangalia sehemu yenye matatizo, ili kuhakikisha wanapata ufumbuzi.

"Roho ya Rais wetu haitulii kwani kukiwa na magonjwa ni lazima atafute njia ya kuwa salama, hivyo tumwombee kwa Mungu ili awe pamoja naye, ili nchi iongozwe na Mungu, kwani tusipowapenda viongozi, wananchi tunamchukiza Mungu," amesema Kulola leo .

Amesema, kinachotakiwa ni kumwombea hadi amalize muda wake wa uongozi na kupata mtawala mwingine wa nchi; uchochezi utakaosababisha vurugu na uvunjifu wa amani usikubaliwe hata kidogo, kwani kuna nchi zilikuwa na amani mtu au kundi la watu likasababisha amani kutoweka.

"Sisi hatuna maisha magumu kama nchi zingine, watu wasilaumu tu wafanye utafiti na kuhakikisha kile wanachosema, mimi nimezunguka nchi nyingi kuna zenye maisha magumu ya kukosa hata chakula," amesema.

Angalia historia yake na munishi....hapo ndio utaelewa somo.
 
Ni muda sasa Watanzania tutambue kwamba matatizo yetu hayata tatuliwa kwa kupiga magoti na kusujudu tu. Jamani hard work is prayer in action. Hii mentality ya kudhani kila kitu kita kuwa sawa tu kwa kufumba macho na kukunja mikoni ndiyo ina tuponza.
 
EATG iungane na TAG kama zamani ndio tutaelewa anapenda sana umoja na amani. Kujitenga kwake ni kiashiria tosha kwamba yeye naye ni adui wa umoja na amani. Kwa magomvi yake na mpinzani wake Zakayo??? alisababisha watu wengi kupwaya imani zao. Anaonekana yupo kibiashara zaidi, ingawa kweli Mungu amemtumia sana kuvuna watu, lakini shetani naye kamtumia sana kuangusha wengi. Ni rahisi kukiona kibanzi ndani ya jicho la mwenzio lakini ni vigumu sana kuliona boriti ndani ya jicho lako mwenyewe.
 
Nimemshangaa mara nyingi sana huyu Mzee ambaye nilikua namheshimu sana but tangu aanze kushabikia mambo ambayo hayana msingi nimempuuzia! juzi katumia airtime kibao kuponda CDM na Babu wa Loliondo tena kwa kumuita mchawi na mshirikina, kwa kweli amenikinai ila baada ya hapo nilifuatilia his educational background....mmmhh kumbe hana tofauti na akina fulani
 
Hivi Eli hujui kama huyu mzee kashapewa PhD ya theology? Yeye pamoja na wachungaji kadhaa wa dhehebu lake wamepewa PhD kama ile aliyopewa mchungaji Getruda Lwakatare, mama Mkapa na ile ya JK. Tanzania ni vichekesho vitupu kwenye kila sector. Hata kwenye dini watu wanachakachua kama kawa.
 
Anashabikia umoja huku akitukuza ubinafsi, alitofautiana na mch. maboya wakatimuana na leo anakuja kutuhubiria umoja! labda kama umoja una maana nyingine, nieleweshwe
 
Tumuombee, hivi anamdanganya nani kwama JK anawatanzania katika kichwa chake? imekula kwako mzee bahati mbaya hasomi jamii forums
 
Kumbe bado tuna safari ndefu. Eeh mungu wa mababu wape upofu wote wanaotetea mafisadi
 
EATG iungane na TAG kama zamani ndio tutaelewa anapenda sana umoja na amani. Kujitenga kwake ni kiashiria tosha kwamba yeye naye ni adui wa umoja na amani. Kwa magomvi yake na mpinzani wake Zakayo??? alisababisha watu wengi kupwaya imani zao. Anaonekana yupo kibiashara zaidi, ingawa kweli Mungu amemtumia sana kuvuna watu, lakini shetani naye kamtumia sana kuangusha wengi. Ni rahisi kukiona kibanzi ndani ya jicho la mwenzio lakini ni vigumu sana kuliona boriti ndani ya jicho lako mwenyewe.

Si TAG tu, hata haya yote yametoka humo ndani ya EAGT baada ya kujitoa TAG - Full Gospel Fellowship -Kakobe, Calvary Assemblies -Maboya, Philadelphia Assemblies-Masinga, Bethel Assemblies of God - Chidundo plus many other. Huo umoja anaousema ilhali yeye mwenyewe hapendi kuwa na umoja ni upi?
 
Ndugu zangu
Askofu Kulola si suala la uzee. Ni kazi ya UWT.
Wana mkakati wa kuwatumia baadhi ya maaskofu na mashehe ili kuwagawa
watanzania na kuwachanganya ili wasiungane kuona nini kinalisumbua taifa.

Nimedokezwa na watu walio karibu sana na Askofu Kulola, kuwa juzi alipelekewa tiketi ya ndege na UWT ili aje DSM kuongea na wana habari hasa baada ya kusikia kuwa CDM inaweza kuitisha maandamano nchi nzima kupinga muswada wa mchakato wa katiba. Mzee anapewa hata maneno ya kusema.

Haiingia akilini kuona Kulola anamsakama Kakobe wakati Kakobe mwaka jana alimkaribisha na kumwandalia nafasi ya wiki nzima kanisani kwake kuhubiri mbele ya televisheni. Katika mahubiri yake ya wiki nzima, Kulola akatamka kuwa "Askofu Kakobe ni nabii wa kweli katika taifa letu". Akaendelea kusema kuwa ameonyeshwa hivyo na Mungu kuwa Kakobe ni mtu wa Mungu.

Amefikia hatua mbaya ya kusema lolote kwa kupewa chochote.

Si kila uzee una hekima.
 
sadka zimepungua nini kanisani?lazima jk atakuwa amemfadhili...hivi inawezekana shetani anawatumiA BAADHI YA WACHUNGAJI?mmh hizi dini sasa noma
 
Nimemshangaa mara nyingi sana huyu Mzee ambaye nilikua namheshimu sana but tangu aanze kushabikia mambo ambayo hayana msingi nimempuuzia! juzi katumia airtime kibao kuponda CDM na Babu wa Loliondo tena kwa kumuita mchawi na mshirikina, kwa kweli amenikinai ila baada ya hapo nilifuatilia his educational background....mmmhh kumbe hana tofauti na akina fulani

Hata mimi nampuuza kwani inaonekana shida za watanzania sio ajenda yake muhimu ila kutumikia tumbo na umaarufu, hatukubali kuyumbishwana viongozi wanaojali matumbo tu!!
 
Ndugu zangu
Askofu Kulola si suala la uzee. Ni kazi ya UWT.
Wana mkakati wa kuwatumia baadhi ya maaskofu na mashehe ili kuwagawa
watanzania na kuwachanganya ili wasiungane kuona nini kinalisumbua taifa.

Nimedokezwa na watu walio karibu sana na Askofu Kulola, kuwa juzi alipelekewa tiketi ya ndege na UWT ili aje DSM kuongea na wana habari hasa baada ya kusikia kuwa CDM inaweza kuitisha maandamano nchi nzima kupinga muswada wa mchakato wa katiba. Mzee anapewa hata maneno ya kusema.

Haiingia akilini kuona Kulola anamsakama Kakobe wakati Kakobe mwaka jana alimkaribisha na kumwandalia nafasi ya wiki nzima kanisani kwake kuhubiri mbele ya televisheni. Katika mahubiri yake ya wiki nzima, Kulola akatamka kuwa "Askofu Kakobe ni nabii wa kweli katika taifa letu". Akaendelea kusema kuwa ameonyeshwa hivyo na Mungu kuwa Kakobe ni mtu wa Mungu.

Amefikia hatua mbaya ya kusema lolote kwa kupewa chochote.

Si kila uzee una hekima.
Siku hizi unabii wa mtu unatolewa na watu sio Mungu na hapa hutegemea ni kiasi gani cha pesa umempa mtu mwenye mamlaka au umaarufu fulani!! ndiyo maana mzee naakwenda akifuata upepo au mdondo wa pesa kakobe alipomwalika lazima alimuandalia fungu na alitakiwa amtawaze Kakobe kuwa nabii, na hapa Kikwete nae Katoafungu unabii umebadilika!!
 
Si TAG tu, hata haya yote yametoka humo ndani ya EAGT baada ya kujitoa TAG - Full Gospel Fellowship -Kakobe, Calvary Assemblies -Maboya, Philadelphia Assemblies-Masinga, Bethel Assemblies of God - Chidundo plus many other. Huo umoja anaousema ilhali yeye mwenyewe hapendi kuwa na umoja ni upi?

Funua tujue maana wengi tunajua huyu mzee hayuko hivi hata kiimani.
 
Back
Top Bottom