Askofu moses kulola kada wa ccm?

kachoka huyo mzee.. wenye hela wamecapitalize! nadhani sadaka hazitoshi kwa sasa
 
Ni muda sasa Watanzania tutambue kwamba matatizo yetu hayata tatuliwa kwa kupiga magoti na kusujudu tu. Jamani hard work is prayer in action. Hii mentality ya kudhani kila kitu kita kuwa sawa tu kwa kufumba macho na kukunja mikoni ndiyo ina tuponza.
Kweli kaka tunatakiwa tufungue macho, yaani kuomba na kufanya uchunguzi wa nini kingine zaidi ya maombi tunachotakiwa kukifanya kwa faida ya nci yetu sio kukaa kama mzuzu na kusubiri kiuambiwa cha kufanya na hawa mafisani wa makamnisani
 
Haya ni mambo ya conficts of iterest. Huwezi kuwa kiongozi wa dini halafu ukawa mwana siasa, kwani ndani ya kanisa au msikiti kuna wafuasi wa vyama mbalimbali. Hii ni either njaa, au kutijiamini, au kukosa muelekeo.

Ukiona mchungaji kagombea ubunge amekwisha katika uchungaji.

Niachie hapo, haya ni mambo ya nafsini hasa.:hug:
 
CCM tangu wakati wa Nyerere, ilimpatia Kulola walinzi wanaolipwa na serikali, ili akipigie debe chama hicho. Kulola alikaidi uongozi wa TAG ikazuka vita kati yake na Askofu Emanuel Lazaro. Serikali ilimpendelea kulola kwani alidai misaada mingi kutoka Marekani ilikuwa na lengo la kupenyeza CIA Tanzania kwa kutumia TAG. Nyerere aliinunua hiyo jumla kwani sera zake za ujamaa zilizoshindwa zilikuwa zikihofu sana Marekani wasijeleta ubepari Tanzania. Kulola alionekana malaika wakati Lazaro serikali ilimuona shetani. Lazaro alikwamishwa mpaka alipoachia ngazi ya uaskofu. Kulola mpaka leo anafaidi uongo wake wa kuidanganya serikali kwamba CIA walimtumia Lazaro. Ukiyasikiliza mahubiri ya kulola kwa makini, utakuta anawalisha waumini siasa za CCM bila wao kujua. Kulola ndiye mhubiri wa DOLA Tanzania. Mikutano yake inalindwa na kikosi maalum, Yeye mwenyewe analindwa kila aendako, Ni kipenzi cha CCM. Tuombe iwe hata mbinguni Mungu atampa heshima anayopewa na CCM. Vinginevyo atakuwa ameshavuna duniani. Nchini Kenya Kitonga aliipamba sana KANU na alikuwa mhubiri wa dola Kenya. Tangu KANU waachie ngazi Kitonga yuko nje ya duara la madaraka.

source
 
Karibu viongozi wote wa dini wana ushirika na serikali ziliizo madarakani hivyo mkuu sitoshangaa na ujumbe huo.
 
Wakuu,

Nimesikia kwenye kipindi cha RFA cha 'watanzania tuongee magazeti' kwamba Askofu kulola amewaasa watanzania waache kumsumbua kikwete kwa maelezo kuwa rais anatumia muda mwingi kufikiria namna ya kuwaletea maendeleo wananchi. Vipi imekaaje hii?
 
IMEKAA KAMA ILIVYOKAA......tunasumbua mno pasipo kuhangahika kwa kutafuta maendeleo
 
Hata mimi nahangaikia sana familia yangu inanishinda lakini nimegundua ni kwa sababu uwezo wangu wa kufikiri,kifedha na seriousness ni mdogo lakini wameshindwa kuniwajibisha.
 
** Nimesoma kwenye vyombo vya habar Gazeti la nyakati toleo namba 139 la 29-05-2011 * kuwa Askofu kulola wakati wa sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake kuliongoza kanisa la EAGT,shrehe hiyo ilifanyika katika kanisa la EAGT-Siloam Ipagala Dodoma aliwataka wa-Tanzania kuacha kumlalamikia Rais kikwete pamoja na wasaidizi wake kutokana na maisha kuwa magumu badala yake tumgeukie Mungu.
** Jambo jingine aliwaasa viongozi wa madhehebu na viongozi wa vyama vya siasa waache kuwatumia wanavyuo katika migomo maana watatengeneza kizazi kitakachoichukia nchi na viongozi wake
** Kwa maoni yangu kauli yake hiyo haiwezi kupita bila kupingwa sababu Jk pamoja na serikali yake ndio waliotufikisha hapa Ufisadi,mikataba mibovu dhuruma kwa wananchi kuuawa wananchi na polisi wanaolipwa na kodi za wananchi kwa visingizio mbali-mbalina mambo mengine mengi tu.
** Kuhusu migomo vyuoni wakulaumiwa ni serikali ya Jk urasimu mpaka wanafunzi wanakosa haki zao za msingi kwa haya machache serikali lazima ilaumiwe Kama ni kumwomba Mungu yeye tayari alishatubariki na vitega uchumi vingi sana tatizo ni kwa Rais wetu na wasaidizi wake wameshindwa kusimamia raslimali za nchi yetu na kusababisha nchi yetu kuwa shamba la BIBI kwa wawekezaji.
 
Code:
aliwataka wa-Tanzania kuacha kumlalamikia Rais kikwete pamoja na wasaidizi wake kutokana na maisha kuwa magumu badala yake tumgeukie Mungu
.
Lakini kama yeye ni chaguo la Mungu kwanini kuwe na maisha magumu kwa raia wake, na yeye akiishi raha mustarehe?
 
Wamepoteza maana ya injiri hao wanafiki...
Wamelewa sadaka za waumini wao hata hawafahamu tena umasikini wa hao waumini.
Wanachofanya ni kutengezneza mazingira ili "ministry" zao zisibugudhiwe na watawala.
Ndio maana utawasikia "Kikwete chaguo la Mungu"
Unafiki tu kwa matumbo yao........ MTZ hana pa kukimbilia hakiyanani
 
** Nimesoma kwenye vyombo vya habar Gazeti la nyakati toleo namba 139 la 29-05-2011 * kuwa Askofu kulola wakati wa sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake kuliongoza kanisa la EAGT,shrehe hiyo ilifanyika katika kanisa la EAGT-Siloam Ipagala Dodoma aliwataka wa-Tanzania kuacha kumlalamikia Rais kikwete pamoja na wasaidizi wake kutokana na maisha kuwa magumu badala yake tumgeukie Mungu.
** Jambo jingine aliwaasa viongozi wa madhehebu na viongozi wa vyama vya siasa waache kuwatumia wanavyuo katika migomo maana watatengeneza kizazi kitakachoichukia nchi na viongozi wake
** Kwa maoni yangu kauli yake hiyo haiwezi kupita bila kupingwa sababu Jk pamoja na serikali yake ndio waliotufikisha hapa Ufisadi,mikataba mibovu dhuruma kwa wananchi kuuawa wananchi na polisi wanaolipwa na kodi za wananchi kwa visingizio mbali-mbalina mambo mengine mengi tu.
** Kuhusu migomo vyuoni wakulaumiwa ni serikali ya Jk urasimu mpaka wanafunzi wanakosa haki zao za msingi kwa haya machache serikali lazima ilaumiwe Kama ni kumwomba Mungu yeye tayari alishatubariki na vitega uchumi vingi sana tatizo ni kwa Rais wetu na wasaidizi wake wameshindwa kusimamia raslimali za nchi yetu na kusababisha nchi yetu kuwa shamba la BIBI kwa wawekezaji.

Kwenye red: ama huyu Babu anasumbuliwa na dementia au katumwa. Kama ni dementia sawa maana huo ni ugonjwa lakini kama katumwa kutueleza huu upuuzi na anajuwa ni upuuzi basi yeye ni mpuuzi. Kwa nini nasema ni mpuuzi? Yaani tukose umeme kwa sababu ya makampuni hewa badala ya kudai haki anasema tumwombe mungu? polisi wauwe watu badala ya wananchi kudai utawala wa sheria anasema tumuombe mungu? 80% ya wanafunzi form IV wapate zero badala ya kuuliza ni kwa nini anasema tuombe mungu?

Askofu matonya huyu, kazoea kuishi kwa sadaka na misaada, na kwake yeye anaona ni mungu ndio ameleta. Sasa kwa nini mungu anaonekana kujitenga na watawala wetu wanaotunyang'anya kila kitu badala ya kutuletea neema? Ni kwa kwa sababu tumekuwa hatudai haki yetu. Nasema tupishe tudai haki yetu Askofu, na kama wewe unavyopayuka kwenye ibada kuhusu fungu la kumi basi na sisi tunataka fungu la letu. Not even Babu Askofu Kulola can stop us!
 
Back
Top Bottom