Askofu moses kulola kada wa ccm?

Zaidi miaka 20 iliyopita nilikuwa mwanafunzi mjini Arusha. Siku moja rafiki yangu alinishawishi tukamsikilize mzee Kulola viwanja vya Reli (au kitu cha kufanana hivyo). Mahubiri yalifanywa na yeye na mwanaye aitwaye Dan. Well, sikuamini nilichosikia.

Ilipofika mida fulani (yapata saa kumi na mbili jioni) watu wengi hasa wanafunzi walianza kuondoka kuwahi usafiri kurudi vyuoni/majumbani.....nimnukuu maneno aliyosema "Mlaaniwe wote mnaoondoka kabla sijamaliza....magari na mabaiskel yaingie mitaroni....mpatwe na ajali, magonjwa, msilale kwa amani nk nk nk..."

Basi mie nilichora mstari toka siku ile kutomsikiliza wala kutaka kusika chochote chenye kumhusu huyu mzee. Inaonekana ana ubnifsi, hasira na chuki. Bila shaka hawezi kutoka nje ya wigo huo. Hivyo nasikitika sana kusoma jambo lolote linalomhusu huyu mzee kama ilivyo leo
 
EATG iungane na TAG kama zamani ndio tutaelewa anapenda sana umoja na amani. Kujitenga kwake ni kiashiria tosha kwamba yeye naye ni adui wa umoja na amani. Kwa magomvi yake na mpinzani wake Zakayo??? alisababisha watu wengi kupwaya imani zao. Anaonekana yupo kibiashara zaidi, ingawa kweli Mungu amemtumia sana kuvuna watu, lakini shetani naye kamtumia sana kuangusha wengi. Ni rahisi kukiona kibanzi ndani ya jicho la mwenzio lakini ni vigumu sana kuliona boriti ndani ya jicho lako mwenyewe.

Mkuu Lukanjobe inatisha sana mtu anapohubiri amani na uvunjifu wa amani wakati yeye mwenyewe anajua alikoanzia mpaka kufungiana milango ya kanisa na waliokuwa wanampinga na hadi anaanzisha hilo la kwake ni mangapi yametokea. Amani bila shibe hakuna, amani wakati wananchi wanaona raslimali zao zinaibiwa mchana kweupe sidhani kama hiyo ni amani, amani wakati wananchi wanafukuzwa kama mbwa kwenye maeneo yenye migodi kupisha wawekezaji hiyo sidhani kama ni amani, amani wakati watoto wa walalahoi wanakaa chini hawana madawati wala vitabu wala walimu sidhani kama hiyo ni amani
 
Back
Top Bottom