Askofu Dallu: Marufuku shule za kanisa katoliki wanafunzi kuendelea na masomo baada ya kupata mimba

Wewe siyo Mkristu au akili yako ina walakeen. Unataka wasichana 770 wazae mara saba saba? If you kill once, you cannot kill him again. Kuua watu 7 mara 70 so mtu mmoja ni watu 500. Biblia haikusema hivyo.
Mkuu shida huyo padri anaongelea maadili ndio nkuulize na wwe mtetezi je kma ni maadili kwanni msitimue wasio bikra????

Kma katoliki wako serious na maadili mbona wanfungisha ndoa hata ya asiye bikra??? Aliyezaa????

Nijibu hayo mawili
 
Dah mkuu mie naona basi uendelee na msimamo wako tu maana inaonekana hutaki kuamini tofauti mfano unasema akishazaa asirudi shule eti sababu sheria inasema hivo !!! Kwahyo ina maana hata wakati tunaibiwa madini magufuli angekaa kimya tu kisa sheria ndo zinataka tuibiwe hivyo???? Mbona sikuelewi

Pia kuhusu imani na kiserikali nmeshakubali mimba na zinaa ni kosa kubwa sana ila nmeshasema adhabu ndio napingana nayo ssa hujibu kitu umekalia udini tu basi nshakubali kuwa ni kosa ila je we unaona hyo adhabu ni sawa na kma ni sawa kwanni basi mnaacha wanaotoa mimba wanaofanya kinyume na maumbile, wanaotumia condom n.k kwanni msiwatimue hao wote if at all mnadai mnafanya hivo kwa ajili ya kupinga zinaaa

Kma unataka kujifunza basi jibu hizo hoja usizunguke na usibadilishe mada
Nimekuuliza swali unataka majibu ya kidini au serikali?
Mambo ya makinikia yanakujaje? Mtoto wako akipata mimba unafanyaje?
 
Mapadri wanatakiwa kusoma alama za nyakati pia watu sasa hivi wana uelewa sana kupita kiasi na vyongozi wa dini hawatakiwi kuunga hoja zinazokuwa zinatolewa na watawala maana unaweza kuwaudhii waumini wasiofungamana na huyo mtawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi Wa dini kuwa puppet Wa watawala haipendeziii.alikuwa wapi siku zote asizuie hilo aje kusema sasa hivi badala ya mkulu kusema
 
Nimekuuliza swali unataka majibu ya kidini au serikali?
Mambo ya makinikia yanakujaje? Mtoto wako akipata mimba unafanyaje?
Makinikia nimeingiza maana unasema eti oooh mwanafunzi si sawa arudi shule kisa sheria inasema hivo???? Ndio nkakupa mfano mbona kwenye makinikia magufuli alibadilisha sheria na hakusema tunaibiwa kisa sheria????

We jibu hoja kwa maoni yako sio unajificha eti sheria sheria kwani sheria haiwezi badilishwa bungeni!!!!

Ni hayo tu
 
Jibu basi zote maana unazunguka majibu hunipi
1.kidini
2.kiserikali

Haya anza
Kidini kwa maana ya kanisa katoliki lina mahakama zake ikithibitika Pasi na shaka lolote muamini atazuiwa kupata Huduma mpaka atakapo ungama na kukiri dhambi zake.
Kiserikali endapo mahakama itajiridhisha mkosaji atafungwa jela
 
Makinikia nimeingiza maana unasema eti oooh mwanafunzi si sawa arudi shule kisa sheria inasema hivo???? Ndio nkakupa mfano mbona kwenye makinikia magufuli alibadilisha sheria na hakusema tunaibiwa kisa sheria????

We jibu hoja kwa maoni yako sio unajificha eti sheria sheria kwani sheria haiwezi badilishwa bungeni!!!!

Ni hayo tu
Jibu ni jepesi kwa yote sheria ya madini imebadilishwa lkn itawahusu wale watakaokuja sio waliopo.sasa na ww zishauri shule zibadili sheria ili wanafunzi wapya wakipata mimba waendelee kusoma
 
Kidini kwa maana ya kanisa katoliki lina mahakama zake ikithibitika Pasi na shaka lolote muamini atazuiwa kupata Huduma mpaka atakapo ungama na kukiri dhambi zake.
Kiserikali endapo mahakama itajiridhisha mkosaji atafungwa jela
Mkuu hoja si kuhusu mimba na shule ama???

Tunachojadili hapa hizo adhabu kidini ni sawa??? Hakuna kitabu kwenye biblia yenu wakristu inayosema mwanamke akizaa nje ya ndoa basi atengwe au asipewe maarifa hakuna na hakitowahu kuwepo ndio maana hat Yesu alisocialise na kahaba na hta kumsamehe dhambi zake hadi akamuosha miguuu sasa kitabu gani kinakataza asipewe maarifa/elimu????

Haya baai tuseme kweli hafai je kwanni mnabagua dhambi??? Mbona saskofu haisemi kuhusu mashoga?? Mbona askofu haisemi kuhusu wanawake wanaoingiliwa kinyme ili wasipate mimba?? Wanaotumia condom??? Wasio mabikra?? Hivi maadili ni kuzia mimba tu sio uzinzi ama zinaa??? JIBU HILI

Kama pia kanisa katoliki linapinga mimba wasirudi shuleni je kwanni wao hawajawahi kataza mwanamke aliyewahi kuzaa asifungishwe ndoa ??? (Kumbuka shule hata akiungama dhambi zake bado haruhusiwi kusoma ila akiungama anaruhusiwa kuolewa) je hakuna double standards hapa

2. KISERIKALI
kma serikali inazuia mimba kwa kigezo cha maadili mbona haitimui wasio bikra???? JIBU HILI PIA
 
Jibu ni jepesi kwa yote sheria ya madini imebadilishwa lkn itawahusu wale watakaokuja sio waliopo.sasa na ww zishauri shule zibadili sheria ili wanafunzi wapya wakipata mimba waendelee kusoma
Ndio hapo wanakataa eti maadili??? Sasa maadili hawalalamiki wanaotolewa bikra hawalalamiki wanaotoa mimba hawalalmiki wananaotumia condom ila MAADILI ni kupinga mimba tu

Hii ncii hii sijui nani katulaani
 
Unafiki ni kwa kila Mwanadamu, namuunga mkono askofu kwa maana ametoa tamko kwa niaba ya kanisa jimboni mwake ambao yy ni mtawala.
Ni sawasawa Hata mm ndani ya utawala wa NYUMBA ni kwangu binti zangu ntawaambia hivyohivo Hata nyingi watoto wenu, wadogo zenu na majirani zenu mtawaambia hivyo hivyo tuache unafiki .
Plan B baada ya binti kutiwa mimba hayo ni mengine. Yaani kanisa lishabikie mimba zitokanazo na zinaa au kanisa lishabikie matumizi ya kondom hapana kila kitu na wakati wake watoto wasubiri wakati utafika.
mwanao akipewa mimba je
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea Mhashamu Damian Dallu amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo, na kusema kuwa shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki hazitaruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

Amesema hayo katika Ibada ya Misa Takatifu ya Upadrisho wa Shemasi Jerome Mtatifikolo, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Afya ya wagonjwa Ilole jimboni Iringa ambapo amebainisha kuwa wanaoshabikia wanaopata mimba kurudi shule wanaharibu utamaduni wa kiafrika na kuchafua heshima ya Taifa.

“Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu. Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?.

Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?” Amehoji Askofu Dallu.

Katika hatua nyingine Askofu Dallu amewaasa waamini kufanya maandalizi ya kutosha hasa ya kiroho wanapojiandaa kuingia katika Sakramenti ya Ndoa ili ndoa zao ziwe na mwelekeo wa kiimani zaidi. Amesema kuwa kabla ya kupewa upadri, Shemasi Jerome alihudhuria mafungo ya kiroho ya siku 5 jambo ambalo linapaswa kuigwa na wale wanaojiandaa kupokea Sakramenti ya ndoa badala ya kujikita katika kufanya maandalizi ya kimwili.

“Watu wa familia mnatumia siku ngapi kufanya mafungo kabla ya kufunga ndoa? Au ndiyo ile kufanya maandalizi mengine ya kimwili marefu. Mkumbuke kuwa hata sisi mapadri tunatoka kwenu, matokeo ya kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya ndoa ndiyo haya tunayoshuhudia sasa hivi ambapo wanaoishi ndoa kama Sakramenti ni wachache,” ameeleza.

Aidha amesema kuwa watu wanaoishi maisha ya pamoja kwa muda mrefu hadi kuwa na watoto hawastahili kuitwa wachumba kwa kuwa uchumba kielelezo chake ni Maria na Yosefu, na kuwataka kuacha kutumia jina hilo na badala yake wajiite wachumba sugu.

“Ulisikia wapi watu wanaishi uchumba mpaka wanakuwa na wajukuu? Tafuteni jina jingine kuanzia sasa labda mjiite wachumba sugu. Tutapata mapadri na masista wa namna gani? Kielelezo cha uchumba ni Yesu na Maria,” Ameeleza.

Pia amesema kuwa kazi ya karama ni kujenga umoja wa Kanisa na siyo kuligawa, na kumtaka kila mmoja kutumia wito wake kumtajirisha mwingine.
View attachment 547182

Chanzo:Gazeti la Kiongozi..
Lakini pia marufuku hiyo iwahusu masista na watawa wanaopata ujauzito wasiendelee kuishi kwenye makazi ya kanisa baada ya kujifungua.
 
Hii iambatane na sera ya kitaifa na elimu kwa watoto wa kike wale wanaokumbana na ubakaji watoe taarifa haraka mara baada ya tukio wapewe zile dawa za kuzuia mimba isitunge na wahusika wakamatwe watakaopata mimba kwa namna ingine zaidi watakuwa wamejitakia na ndiyo wale waliokuwa wanaendekeza ngono
 
Kwani Hio dini anayoiongoza ni utamaduni wetu sisi WaAfrica?? Bangi sio chai
 
Back
Top Bottom