Askofu Dallu: Marufuku shule za kanisa katoliki wanafunzi kuendelea na masomo baada ya kupata mimba

Mimi ni mkatoliki na hivyo sikubaliani kabisa na matamko ya huyu askofu kwa sababu anapotosha watu sabb ya kiherehere cha mtafuta kiki kwa piki2 ukisoma kitabu cha maandiko matakatifu cha mathayo 18; 21-35 inaelekeza wazi ni jinsi gani wanadamu wanavyopaswa kusamehana na kumwachia mungu atoe hukumu kwa matendo mabaya.
Mi mwenyewe napinga hili.Mbona kule Ulaya na Marekani kuna maPadre walikuwa wanawapumulia vijana wadogo,wengi wakiwa wanakondoo na misamaha ikatolewa kwa hao wahalifu??? Yaani ni kujipendekeza tu kwa utawala bila kuangalia athari zake kwa jamii.Afadhali kukaa kimya hata kama ndo msimamo wa kanisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Utamaduni wetu wa africa ni upi?maana haka kamsemo me huwa sikaelewagi...

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapi huyu padri kajitoa ufahamu tuu kujipendekeza .Ukiwa mkristo ni pamoja na kufuata desturi na tamaduni za kikristo na utamaduni wako utakao bakia nao ni ule unaolandana na tamaduni za kikristo na zaidi inakuwaga lugha tuu ndio inabaki kama tamaduni yako ndani ya ukristo na kadhalika dini karibu zote .ndio maana ataa yeye huyo padri kavaa joho badala ya rubega ya ngozi ,sasa Sijui yeye padri anaongelea utamaduni gani hapo ,maana kama ni ukristo Yesu anasema kwa asie na dhambi awe wakwanza anyanyue jiwe amuadhibu mwanamke huyu aliezini .matokeo hakuna aliesubutu .Kwa Mungu napo anasema samehe Mara saba sabini ataa ikibidi ni kwa siku moja,sasa huyu anatoa wapi ujasiri Wa hii kauli yake yakutosamehe ,au mchawi huyu maana .wachawi ukivunja mwiko ndio basi kama ni kufa unakufa .Hawa ni wakuwaombea tuu nao sio wazima .duh Mungu anisamehe lakini ukweli inakatisha tamaa
 
Mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 hana utashi wa kusema anafanya mapenzi bali anabakwa.

Sasa binti anayebakwa na kupata mimba kwanini tena anapewa adhabu ya kunyimwa haki yake ya kuendelea na masomo??
Mkuu Mchambuzi nakuelewa na kukubaliana na wewe kuwa ni mtoto mdogo na kwamba ana haki ya elimu. Ila ninachosimamia mimi ni umuhimu wa kujadili njia nyingine ya kumsaidia huyu mtoto nje ya mfumo uliopo ili kuzuia kuhalalisha mimba mashuleni. Kuruhusu waendelee kwenye mfumo uliopo kwaweza "kuhalalisha". Pia tujadili njia ya kuzuia hizi mimba. Inauma mtoto kukosa elimu, lakini ni vizuri kuifundisha jamii kuwa sio jambo jema.
 
...ina maana kabla mtukufu kabisa kutema cheche kupiga marufuku wanafunzi na mimba mashuleni ina maana kanisa katoliki lilikuwa likiruhusu wanafunzi wazazi kuendelea na masomo..?
nauliza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa makini ungejua kwamba anayemjaza mwaafunzi mimba anafungwa miaka mingi tu.

Wazazi wanaojua uchungu wa kujaziwa mimba watoto,hii kauli wataifikisha kwa mabinti zao bila kutoa/kuongeza neno,maana hata wao binti akipata mimba wanafukuza nyumbani.

Ndoto binaadamu anakuwa nazo nyingi sana,tatizo ni sisi kudhani ndoto ni shule au inatimizwa na shule tu.
Ifike kipindi watu mtumie vichwa vyenu kufikiria badala ya kufuata kila kitu wanacho zungumza hawa wavaa kanzu na skapulali.
Hivi inakuaje mtu unashindwa kuelewa kwenye situation kama hii anae umia zaidi ni mtoto wa kike hapo.
Hata hivyo vitabu vyenu vya imani vimesisitiza sana kuhusu elimu.
Hao wazazi wanao fukuza watoto kisa wamepewa mimba ni arrogance inawasumbua, ukimfukuza nyumbani inasaidia nini!?!?
zaidi ya kuzalisha malaya,watoto wa mitaani etc
 
Vipi kuhusu muumini mwenye mimba kabla ya ndoa hamtachukua sadaka yake?

Plus waumini wenye ndoa waliozaa nje ya ndoa. Hakuna anayeshabikia uovu lakini sote tu wanadamu tu tuna mapungufu yetu kama wanadamu. So tunapokosea ni vizuri kukawa na 2nd chance kama ambavyo Mungu anavyotoa hiyo nafasi ili kurekebisha pale tulipokosea.
 
Hata wewe ni mtuhumiwa wa uzinzi na mtu Fulani,Ila kithibitisha ndio tatizo.
Ujasikia kanisa katoliki America lilitangaza kufilisika ili kukwepa kulipa fidia kwa watoto walio lawitiwa na kudhalilishwa kwa tuhuma zilizo dhibitishwa mahakamani !!?? Google for more details .
 
Askofu yuko sahihi. Je watoto wanaopata mimba kwani wako kwenye ndoa?kusema waendelee na masomo ni kusema waendelee na uzinzi japo kuna wazinzi sugu ambao hawapati mimba .
Inawezekana mimba hizo ni tunda la uzinzi, ambayo ni dhambi. Je na wale wanaobakwa je? Wanaorubuniwa na ndugu ili watimiziwe mahitaji ya msingi, ikiwemo elimu? Na wao tunawahukumu? Hata Yesu, alituasa tusamehe saba mara sabini. Hata Yesu yule mwanamke mzinifu alipotaka kupigwa mawe na umati (kitu ambacho ni utamaduni wao) aliwaambia "mwenye dhambi na anyanyue jiwe awe wakwanza kumpiga"... Leo hii, Kanisa lilojengwa kwenye msingi wa mafundisho na maisha ya Yesu Kristo, linawanyanyapaa watoto wa Kanisa, watoto wa Yesu. Hatuwasaidii, tunawazidishia mzigo..wakimbilie wapi kwenye faraja na mafunzo ya kweli kama sio "Kanisani"?
 
Je ni kweli kuwa kama jamii hatuna mifano ya wototo waliojiendeleza kielimu baada ya kujirudi na kujutia makosa yao na sasa ni watu muhimu kwa familia na jamii? Je kwa kuwanyima elimu haiwezekani tukawa tunawanyima uwezo wa kutunza watoto wao na hivyo kuzalisha vibaka watakaozaliwa na hawa wajawazito tunaowanyima fursa za elimu? Ni imani yangu kuwa baba Askofu hana hata mstari mmoja wa kutoka biblia kusupport hoja yake hiyo
Yesu alitumia mfano wa mbegu kwamba mbegu haiwezi kuzaa bila kufa kwanza (sijui kwenye biblia ni sehemu gani). Hivyo kumfukuza mmoja itasaidia kuzuia au kupunguza kwa kiasi wengine wasifanye makosa yanayofanana. Kufukuza ni sehemu ya kuboresha nidhamu kwa wengine watakao baki. Tusichukue mifano michache kuangamiza wengi. Na ujue kuna kumsaidia mtu huku ukiwa unaonesha kutoridhika na makosa yake. Naamini kwa asilimia kubwa ikitokea mwanafunzi mmoja katika kundi akipata mimba na akiruhusiwa wengine kupata mimba kuko nje nje. Hivyo kumyima kuendelea hapo inaonesha kabisa kumpa nafasi nzuri ya kujirekebisha kuliko kumuuacha hapo. Mm nina mifano mingi ya watu ambao wanafuata waliowatangulia wakifanya tu uzembe wengine wanaofuata kufuata tabia hiyo.
(Methali 23:13)Proverbs 23:13. Withhold not correction from the child: for if thou beatest him with the rod, he shall not die
 
KUMBE!!!
Mimi ningemuelewa zaidi huyu mtumishi wa Mungu kama angesema, ni "marufuku mwanafunzi kujiingiza kwenye mambo ya ngono, pia ni marufuku kuvunja amri ya kuzini hata kwa wasio wanafunzi" sasa kauli yake imeacha mpenyo wa wanafunzi wafanye ngono ila OLE wao wakikamatwa hasa hawa wasichana, shule basi. Hapa naona anaikuza biashara ya kondom.
Unafiki ni kwa kila Mwanadamu, namuunga mkono askofu kwa maana ametoa tamko kwa niaba ya kanisa jimboni mwake ambao yy ni mtawala.
Ni sawasawa Hata mm ndani ya utawala wa NYUMBA ni kwangu binti zangu ntawaambia hivyohivo Hata nyingi watoto wenu, wadogo zenu na majirani zenu mtawaambia hivyo hivyo tuache unafiki .
Plan B baada ya binti kutiwa mimba hayo ni mengine. Yaani kanisa lishabikie mimba zitokanazo na zinaa au kanisa lishabikie matumizi ya kondom hapana kila kitu na wakati wake watoto wasubiri wakati utafika.
Hapo kwenye red, huoni kama kanisa limeshabikia matumizi ya kondom kupitia kauli yake. Fafanua kama sio kweli alimaanisha nini kwamba wasichana wakipata mimba hakuna kurudi shuleni! Maana yake ili usipate mimba tumia kondom#$!? Logic ya kawaida tu hii
 
Back
Top Bottom