Matumbwela
Senior Member
- Oct 23, 2010
- 124
- 88
Mmh huyo mtoa 'mada' atakuwa graduate wa sheria UDSM kweli? mbona unaidhalilisha UDSM na fani ya sheria? Wanasheria wanajua kujieleza na mwanasheria hawezi kutuhumu mtu kwa kesi ya mauaji kwa kisingizio cha ada ya Chuo. Ada kubwa ya Chuo Vs. Kuua (Murder) kwa mujibu wa Sheria vina uhusiano wowote?
Any way, mimi ni mmoja wa wadau waliosoma Chuo cha Tumaini hapa Dsm. Hakuna hata siku moja ambapo chuo kilitangaza mchango wa ujenzi wa kiasi chochote kile. Inashangaza hiyo Shilingi milioni moja yeye ameitoa wapi! Kwa kifupi ada wakati ule (mpaka 2008/09) ilikuwa 1,460,000, 1,560,000, na 1,660,000 kwa mwaka wa 1, mwaka wa 2 na mwaka wa 3 respectively. Bodi ya Chuo ikaamua kupandisha ada kutoka hiyo iliyotajwa mpaka shilingi 2,300,000 kwa wote ili kukidhi gharama ya uendeshaji. Ada mpya ilianza mwaka wa masomo wa 2009/10.
Ikumbukwe pia Tumaini ni Chuo Kikuu Binafsi ambacho kinajiendesha kwa ada ya wanafunzi na hakina ruzuku ya aina yoyote kutoka serikalini. Kama ungekaa chini kuchanganua hali halisi ya uendeshaji ungeweza kuelewa ninachokizungumza hapa. Kama vyuo ambavyo mishahara ya wafanyakazi, majengo, na gharama zingine zote za uendeshaji zinagharamiwa na serikali (Vyuo vya serikali) vinatoza ada mpaka 1,800,000.00 (ikiwemo sheria) Chuo Kikuu binafsi kitatoza ngapi ili kumudu gharama zote za uendeshaji??? Mbona kuna vyuo ada zake ni zaidi ya zile za Tumaini Dsm! mfano ni Sebastian Kolowa Memorial University - Lushoto ambao ada ni 2.7 milioni, Bagamoyo University 3.0 milioni, hapo huhitaji kutaja IMTU na vinginevyo!! Natambua, hata hivyo kuwa kuna Vyuo vichache vya binafsi vyenye ada ndogo kama St. Augustine, lakini each case on its own merits.
Inabidi tufike hatua kutofautisha hali halisi ya kipato cha mtanzania na gharama za uendeshaji katika kuwapatia elimu watanzania! Kama hilo lingejulikana basi hata serikali ingekuwa inachangia gharama za uendeshaji kwenye vyuo binafsi ili ada iweze kupungua.
Nisiwachoshe wasomoji, niseme tu kuwa nimesikitishwa na mtoa 'mada' kwa kiwango chake kidogo cha uelewa wa mambo hasa anapojipambanua kama mwanasheria halafu anatoa hoja ambazo mwanasheria hatarajiwi kuzitoa. Zaidi ya yote Askofu Malasusa ni mmoja wa viongozi wa dini ambao wamekuwa mstari wa mbele kukemea mambo yasipokwenda sawa katika jamii ikiwemo serikali... na kwa kauli aliyoitoa ya mauaji ya mwandishi wa habari anastahili kuungwa mkono unless mtoa mada ndo polisi aliyemuua Mwandishi wa Habari kwa hiyo anataka ku-divert attention ya watu.
Asante