Askof Malasusa acha kujifanya wewe si muuaji.

Mmh huyo mtoa 'mada' atakuwa graduate wa sheria UDSM kweli? mbona unaidhalilisha UDSM na fani ya sheria? Wanasheria wanajua kujieleza na mwanasheria hawezi kutuhumu mtu kwa kesi ya mauaji kwa kisingizio cha ada ya Chuo. Ada kubwa ya Chuo Vs. Kuua (Murder) kwa mujibu wa Sheria vina uhusiano wowote?

Any way, mimi ni mmoja wa wadau waliosoma Chuo cha Tumaini hapa Dsm. Hakuna hata siku moja ambapo chuo kilitangaza mchango wa ujenzi wa kiasi chochote kile. Inashangaza hiyo Shilingi milioni moja yeye ameitoa wapi! Kwa kifupi ada wakati ule (mpaka 2008/09) ilikuwa 1,460,000, 1,560,000, na 1,660,000 kwa mwaka wa 1, mwaka wa 2 na mwaka wa 3 respectively. Bodi ya Chuo ikaamua kupandisha ada kutoka hiyo iliyotajwa mpaka shilingi 2,300,000 kwa wote ili kukidhi gharama ya uendeshaji. Ada mpya ilianza mwaka wa masomo wa 2009/10.

Ikumbukwe pia Tumaini ni Chuo Kikuu Binafsi ambacho kinajiendesha kwa ada ya wanafunzi na hakina ruzuku ya aina yoyote kutoka serikalini. Kama ungekaa chini kuchanganua hali halisi ya uendeshaji ungeweza kuelewa ninachokizungumza hapa. Kama vyuo ambavyo mishahara ya wafanyakazi, majengo, na gharama zingine zote za uendeshaji zinagharamiwa na serikali (Vyuo vya serikali) vinatoza ada mpaka 1,800,000.00 (ikiwemo sheria) Chuo Kikuu binafsi kitatoza ngapi ili kumudu gharama zote za uendeshaji??? Mbona kuna vyuo ada zake ni zaidi ya zile za Tumaini Dsm! mfano ni Sebastian Kolowa Memorial University - Lushoto ambao ada ni 2.7 milioni, Bagamoyo University 3.0 milioni, hapo huhitaji kutaja IMTU na vinginevyo!! Natambua, hata hivyo kuwa kuna Vyuo vichache vya binafsi vyenye ada ndogo kama St. Augustine, lakini each case on its own merits.

Inabidi tufike hatua kutofautisha hali halisi ya kipato cha mtanzania na gharama za uendeshaji katika kuwapatia elimu watanzania! Kama hilo lingejulikana basi hata serikali ingekuwa inachangia gharama za uendeshaji kwenye vyuo binafsi ili ada iweze kupungua.

Nisiwachoshe wasomoji, niseme tu kuwa nimesikitishwa na mtoa 'mada' kwa kiwango chake kidogo cha uelewa wa mambo hasa anapojipambanua kama mwanasheria halafu anatoa hoja ambazo mwanasheria hatarajiwi kuzitoa. Zaidi ya yote Askofu Malasusa ni mmoja wa viongozi wa dini ambao wamekuwa mstari wa mbele kukemea mambo yasipokwenda sawa katika jamii ikiwemo serikali... na kwa kauli aliyoitoa ya mauaji ya mwandishi wa habari anastahili kuungwa mkono unless mtoa mada ndo polisi aliyemuua Mwandishi wa Habari kwa hiyo anataka ku-divert attention ya watu.

Asante
 
Kanisa limejenga vyuo, shule, vitega uchumi, mahospitali kwa wingi sana
inawezekana hiyo hela yako uliyokatwa iliingia kwenye kazi nyingine.

Ni lazima roho ukuume kwa kuwa haujaona kilichofanyika kutokana na makato yako. Lakini usipende sana
kuwatuhumu watu wa Mungu namna hiyo, na inawezekana pia ni watu wa chini ya Askofu ndio wanaofanya kanisa lipate lawama.

Malasusa ninayemfahamu (japo siyo sana) ni mtu mwadilifu kabisa.
 
Siku zote jamii huchagua kiongozi mwadilifu. But inapotokea uongozi wa chini yake ukavuruga lazima tumseme Kiongozi tuliyemweka madarakani, ili aangalie kulikoni. Pia ujue kuwa hakuna mtu wa shetani sote tumeumbwa na Eloi aliye mmoja. "Mtu na akitataka kuwa askofu na a..." Tafuta mtume Paulo anasema nini juu ya mwenye kuuhitaji u-askofu.

Bajeti ni kitu muhimu sana. Na kila pesa huenda kule ilikopigiwa bajeti kwa hili, "Kanisa limejenga vyuo, shule, vitega uchumi, mahospitali kwa wingi sana inawezekana hiyo hela yako uliyokatwa iliingia kwenye kazi nyingine." nakataa na inaonyesha umenionyesha ufinyu. Bora ungeliusoma uzi huu na kunyamaza tu.
 
Mmh huyo mtoa 'mada' atakuwa graduate wa sheria UDSM kweli? mbona unaidhalilisha UDSM na fani ya sheria? ...

Any way, mimi ni mmoja wa wadau waliosoma Chuo cha Tumaini hapa Dsm. Hakuna hata siku moja ambapo chuo kilitangaza mchango wa ujenzi wa kiasi chochote kile. Inashangaza hiyo Shilingi milioni moja yeye ameitoa wapi! Kwa kifupi ada wakati ule (mpaka 2008/09) ilikuwa 1,460,000, 1,560,000, na 1,660,000 kwa mwaka wa 1, mwaka wa 2 na mwaka wa 3 respectively. Bodi ya Chuo ikaamua kupandisha ada kutoka hiyo iliyotajwa mpaka shilingi 2,300,000 kwa wote ili kukidhi gharama ya uendeshaji. Ada mpya ilianza mwaka wa masomo wa 2009/10.

Ikumbukwe pia Tumaini ni Chuo Kikuu Binafsi ambacho kinajiendesha kwa ada ya wanafunzi na hakina ruzuku ya aina ... Mbona kuna vyuo ada zake ni zaidi ya zile za Tumaini Dsm! mfano ni Sebastian Kolowa Memorial University - Lushoto ambao ada ni 2.7 milioni, Bagamoyo University 3.0 milioni, hapo huhitaji kutaja IMTU na vinginevyo!! Natambua, hata hivyo kuwa kuna Vyuo vichache vya binafsi vyenye ada ndogo kama St. Augustine, lakini each case on its own merits.

Inabidi tufike hatua kutofautisha hali halisi ya kipato cha mtanzania na gharama za uendeshaji katika kuwapatia elimu watanzania! Kama hilo lingejulikana basi hata serikali ingekuwa inachangia gharama za uendeshaji kwenye vyuo binafsi ili ada iweze kupungua.

Nisiwachoshe wasomoji, niseme tu kuwa nimesikitishwa na mtoa 'mada' kwa kiwango chake kidogo cha uelewa wa mambo hasa anapojipambanua kama mwanasheria halafu anatoa hoja ambazo mwanasheria hatarajiwi kuzitoa. Zaidi ya yote Askofu Malasusa ni mmoja wa viongozi wa dini ambao wamekuwa mstari wa mbele kukemea mambo yasipokwenda sawa katika jamii ikiwemo serikali... na kwa kauli aliyoitoa ya mauaji ya mwandishi wa habari anastahili kuungwa mkono unless mtoa mada ndo polisi aliyemuua Mwandishi wa Habari kwa hiyo anataka ku-divert attention ya watu.

Asante

Hii ni Ngoma kweli Umekalia u-UDSM, u-UDOM, huna lolote. Nchi sasa iko mikononi mwa Wachina hata kuchomelea grill tu sasa mpaka wawa ajiri degree zenu sasa zimegeukia kwenye marumbano yasiyo tija , marumbano ya u-,u-,u-. Hivi mtu akisema "unaniua" kwa mjanja kama wewe unajua its a total tansformation of soul to spirit!!!

Halafu unaongelea mambo ya wakati ule.Cheki hiyo red. Asante kwa takwimu zinayo support thi sthread. "kukidhi gharama ya uendeshaji." Sema jingine, uendeshaji upi wa jengo moja tu la ghorofa pale Kurasini. Huku ofisi ni makontena yaliyobebana? Serikali ituambie hii ni gharama kuliko ile ya kuendesha SAUTI na vyuo vingine vinavyoendeshwa na dini? hata kile Chuo cha Iringa Chini ya waluteli? Akha!!

Sebastian Kolowa Memorial University - Lushoto ambao ada ni 2.7 ( According to TCU's 2012/2013 guidebook pg 95.Kwa taarifa yako kozi ya juu niTsh. 1.6M/=) milioni, Bagamoyo University 3.0 milioni, hapo huhitaji kutaja IMTU ()na vinginevyo!! (Upo sawa, tunaomba serikali itupe sababu za ada hizi.) Iwapo leo chuo kinakubaliwa kumtoza Daktari, Mwanasheria ada maradufu tunafuga nini in future kama si rushwa?

...hasa anapojipambanua kama mwanasheria... nakushukuru sana kwa uelewa wako mpana wa kunipamba fani ya sheria nami sijatamka mahali popote kuwa mimi ni mwanasheria
 
kwa kifupi ni kwamba, kile chuo mimi ni mmoja wapo wa watu tuliochangia kukijenga, kipindi hicho bado nilikuwa nasali lutheran. nilihama lutheran lakini hadi leo hii bado nampongeza sana askofu mdegella wa iringa kwa kujenga chuo kile na shule zingine nyingi sana kule iringa na mikoa meingine. tulichanga kabisa, na sadaka zilitolewa ndo maana wewe ulienda kusoma pale, hukujua chuo kile kilitoka wapi, ila kwa kifupi ni kwamba hadi masikini wa vijijini walichanga kwaajili ya kile chuo tena kwa moyo bila kulazimishwa na sadaka zetu nyingi zilienda kujenga chuo kile ambacho wanaasoma walutheran, waislam, walokole,wakatoliki etc...pamoja na kwamba waliochangishwa mara ya kwanza na kukijenga chuo kile walikuwa walutheran peke yao...ndo maana tunasema wakristo tunao uwezo wa kujiendesha sisi wenyewe kwasababu tumefundishwa kutoa kwa moyo kujenga shule au hata kusaidia masikini sio kama watu wengine ambao wanaomba majengo ya tanesco ambayo yako tayari waingie kuanzisha chuo...kulialia hadi lini?kama wewe ulifeli vyuo vingine ukalazimika kwenda Tumaini, nani alikwambia ufeli? si ungeenda udsm kama una ubavu? hapo kwenda tumaini ulikuwa unasaidiwa tu kusoma chuo ambacho hukuchangia hata senti moja kukijenga ukijua kuwa pale kile chuo hakina mfadhili yeyote zaidi ya ada hizo na sadaka za walutheran ndo zinalipa malecturer wenu wanaofundisha watu wa dini zote. majengo mapya yatatoka wapi? unafikiri watabaki kulalama tuuu kuomba msaada wasaidiwe na selikali kama watu wengine? noooo, cha muhimu ni kujifunza kuwa na moyo wa kuchangia kujenga kitu kwenye jamii yetu kwasababu kitasaidia watu wetu...acha mkono wa birika, utakufa masikini.hutabarikiwa kwasababu ya kuwa mchoyo kutoa kwa watu wengine au kutoa kwaajili ya ujenzi wa jamii yako.[/uta]

sio bure unatafuta bwana,,,,,,,,,nyeg* zimekushika

Nilidhani nawakilisha mawazo yangu kwa watu wanaoweza kunielimisha nami nikawa na mtazamo chana kumbe kuna takataka kama hizi "sio bure unatafuta bwana,,,,,,,,,nyeg* zimekushika'. Usichangie uzi wangu kama huna jambo la
kujenga nchi hii. kwa taarifa yako ujenzi wote huwa na mwisho. pia kiwango na si huu wa TurDACo.

MALASUSA AKATAZA IBADA ZA KUSIFU NA KUABUDU

Wakuu,naomba hii ipostiwe kama separate thread nimeshindwa post

kwa masikitiko makubwa mkuu wa KKKT amekataza ibada za kusifu na kuabudu kuwa huo sio utaratibu wa KKKT na kanisa halitamvumilia mchungaji yoyote atakayekwenda kinyume na utaratibu huo atakayekiuka ataondolewa

Hii imetangazwa jumapili usharika wa Wazo wakati wa ufunguzi wa kanisa je tunaelekea wapi! Nawasilisha
 
Tungempata mdau mmoja ama mtu mwenye uelewe pengine angetufafanulia.Watanzania wengi ni wapuuzi,wanapenda kupuuza mambo ya msingi.Huu uzi una mantiki,kama mtu anaona kuna mazingira hayamfurahishi ana haki ya kuhoji na aelezewe kiufasaha bila matusi wala kejeli.
 
mtoa mada jieleze vzr tukuelewe, inawezekana una hoja ya msingi ila punguza hasira na panga maneno yako vzr utaeleweka.

Kama kwa ufahamu huo umeweza kuvuka mpaka kiwango cha chuo kikuu basi kuna kazi!!!! wewe chuki yako ni zaidi ya Askofu Malasusa, unakitu nadhani ni muendelezo wa hoja za sensa!!!! mtashangaaaaa
 
Kama kwa ufahamu huo umeweza kuvuka mpaka kiwango cha chuo kikuu basi kuna kazi!!!! wewe chuki yako ni zaidi ya Askofu Malasusa, unakitu nadhani ni muendelezo wa hoja za sensa!!!! mtashangaaaaa

Mkuu nani kakwambi ninachuki?
Mbona sijaona nilipokosea?
Hebu soma huyu, utasema nae anachuki?

MALASUSA AKATAZA IBADA ZA KUSIFU NA KUABUDU

Wakuu,naomba hii ipostiwe kama separate thread nimeshindwa post

kwa masikitiko makubwa mkuu wa KKKT amekataza ibada za kusifu na kuabudu kuwa huo sio utaratibu wa KKKT na kanisa halitamvumilia mchungaji yoyote atakayekwenda kinyume na utaratibu huo atakayekiuka ataondolewa

Hii imetangazwa jumapili usharika wa Wazo wakati wa ufunguzi wa kanisa je tunaelekea wapi! Nawasilisha
 
Japo jamaa ametoka nje ya mada ameeleweka sema mtu mwenyewe aliyemjadili ndo inasababisha wadau wajifanye hawakuelewa ila angeongelewa mtu anayevaa kanzu ungeona reaction. tehe! tehe! tehe!
 
mtoa mada jieleze vzr tukuelewe, inawezekana una hoja ya msingi ila punguza hasira na panga maneno yako vzr utaeleweka.

Sasa hapo juu mnashabikia nn!! Yaan watu wengine bana ! Mtoa mada alichokieleza ni ukweli mtupu ila ameshindwa kudisign kichwa cha habari....pili nyie vijana siwaelewi kwan chuo huwa unachagua mwenyewe au unachaguliwa!? Nin maana ya CAS!!!? Kila kitu mbona kinajieleza ndan ya hicho kitabu? ,FEES za kila chuo .itakuwaje uchague chuo unachoona kuwa kuna ada ndefu? Wakati kuna vyuo kama SAUT=950000,MUM=1200000.WHY TUMAIN =2500000?WEZI WAKUBWA HAOOOOOO...!
 
Pumbavu kabisa! Hiki ni nini?

1Tim 3:1-7, mtu akitaka kazi ya askofu... v.3 ...asiwe mwenye kupenda fedha. Tito 3:7 ...asiyependa mapato ya aibu. naamini haya ni mapato ya aibu, kwani haiwezekani kuunganisha ada na fedha za michango ya majengo kisha iitwe kuwa ni ada. kwani serikali ni wajinga kuweka kiwango cha ada ya 1.5M/= kwa kozi kama zinazotolewa na Tumaini University kwa vyuo vingine. Mf. SAUTI, na vyuo vingine vya kiroho.

Jambo hili liko dhahiri lakini serikali na Askofu (anaonekana ameridhia mapato haya ya aibu) wako kimya. Sioni chochote pale Kurasini. Mapato ni makubwa kuliko huduma za kichuo. Library is full of newspapers too small to accomodate more than 50 students at once!!, tena wote ni day scholars. This means huwezi kuitegemea maktaba wakati ukisubiri kuingia darasani mchana kama uko everning session.
 
Tunaiomba wizara husika isifanye masiala, warudi na kukikagua chuo hiki kama kina mazingira ya kishule au mazingira ya kimaslahi zaidi. Binafsi napenda kiwepo, lakini si ktk mazingira hayo, pia nashauri kuwa watoze michango yao kwa mwaka wa kwanza tu. Pia, watuonyeshe kuwa kweli michango hiyo inafanya kazi. Eloi wa Israel naye atawabaria nao watazidi kuongezeka.
 
Mwisho kabisa samahani sana wote mliokwazwa na heading yangu. Lengo langu lilikuwa ni kuwavutia ili msome yanayoniudhi juu ya mapato haya ya aibu kwa kanisa, chini ya kisingizio cha elimu.

Kuua ni msemo wa kawaida ktk mitaa yetu, kukiwa na maana ya kuangushana, "unaniua mshikaji wangu kwa bei hiyo hapana.." Unyonge wetu usiwe ni chanzo cha kutuumiza. Ikumbukwe kuwa elimu ya nchi hii imechangiwa sana na mashirika ya dini. Lakini hatukusoma kwa bei za ajabu kama hizi. Tuende kwa RCs tujifunze wakifanyacho. Wao huduma za kijamii ni za kijamii kweli kweli at an affordable prices. Si kama nishuhudiavyo sasa kwa mfano wa Tumain University-Kurasini kampasi. Askofu nimekusema kwani wewe ndiye uliyeshika hatamu hii. Sitaacha kukumbusha wajibu wako pale uongozi wako utakapolikoroga. Kama ambavyo marais wote wanavyokosolewa.
 
MALASUSA AKATAZA IBADA ZA KUSIFU NA KUABUDU

Wakuu,naomba hii ipostiwe kama separate thread nimeshindwa post

kwa masikitiko makubwa mkuu wa KKKT amekataza ibada za kusifu na kuabudu kuwa huo sio utaratibu wa KKKT na kanisa halitamvumilia mchungaji yoyote atakayekwenda kinyume na utaratibu huo atakayekiuka ataondolewa

Hii imetangazwa jumapili usharika wa Wazo wakati wa ufunguzi wa kanisa je tunaelekea wapi! Nawasilisha

Mimi si Mlutheri wala mu Anglikana; lakini naamini zipo sababu za msingi za kutoa zuio hilo. Kila jumuia inajipambanua kwa taratibu, mila, desturi na utamaduni wake, hivi ndivyo vinavyopambanua imani moja hadi nyingine. Kwa mfano huwezi kuabudu kikatoliki katika ibada ya kiluteri, au kipentekoste katika ibada Katoliki. Moja ya majukumu ya "Askofu" ni kuhakikisha hivyo vinazingatiwa na kudumishwa katika dhehebu analoliongoza; sasa ulitaka aache kila mtu afanye anavyojisikia? Hapana, akifanya hivyo atakuwa amekiuka sababu za uwepo kwake na atasababisha kanisa kutekwa nyara na madhehebu ambayo kanisa lake linajipambanua dhidi yao. At the end hakutakuwa tena na mantiki ya uwepo wa dhehebu analoliongoza. Yuko sahihi.
 
MALASUSA AKATAZA IBADA ZA KUSIFU NA KUABUDU

Wakuu,naomba hii ipostiwe kama separate thread nimeshindwa post

kwa masikitiko makubwa mkuu wa KKKT amekataza ibada za kusifu na kuabudu kuwa huo sio utaratibu wa KKKT na kanisa halitamvumilia mchungaji yoyote atakayekwenda kinyume na utaratibu huo atakayekiuka ataondolewa

Hii imetangazwa jumapili usharika wa Wazo wakati wa ufunguzi wa kanisa je tunaelekea wapi! Nawasilisha

Ni kweli Ibada za kusifu na kuabudu ni nje ya utaratibu wa kilutheri, ilikua ni mbinu tu iliyotumiwa na wachungaji kutaka washarika wao wasihamie makanisa mengine hasa ya pentekoste ambayo hizi ibada zimekuwa ni kivutio cha wengi. Sisi lutherans(walutheri) tuna utaratibu wa kuendesha ibada kwa kufuata liturgia (liturgy)na muongozo huo unafanana na makanisa yote ya kilutheri Tanzania na ulimwenguni, si kwamba nazipinga hizi ibada, lakini zilikua zinatoa makanisa mengi ya kilutheri nje ya utaratibu.
 
Nafurahi kukujulisha kuwa hapa sijaongelea hivyo vyeo vyenu na madaraka. Point yangu hapa ni tozo la Tsh.1M/= per year per student in all his/her years life at Tumaini University-Kurasini campus. (e.g 3M/= for 3 years, 2M/= per2 years and 1M/= if he/she will spend a year only in the University pending annual tuition fee of 1.5M/=).

Umezoea kubishanania vyama nini? Make hata pale penye ukweli ulisha zoea Chama..., basi huona serikali haijafanya kitu. Masuala ya dini (ya Kaisari) hayanihusu. Nikitaka dini nitakuuliza swali moja tu, je, Askofu anajua kuwa kila mtu anayehesabiwa (Sensa) torati inamtaka ailipe serikali? Basi.
.... Muheshimiwa raisi, ile bodi ya udhibiti wa karo na michango mashuleni na vyuoni UTAIANZISHA LINI manake haya pia yanachangia "INFLESHENI"
 
Back
Top Bottom