Askari walinda Amani wa JWTZ wauawa Darfur

Inno laka

JF-Expert Member
Mar 24, 2012
1,616
583
Habari wana JF,

Habari zilizonifikia hivi punde kutoka kwa mpiganaji mmoja aliyeko Sudani ni kuwa wanajeshi takribani 7 wa JWTZ wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa pamoja na Askari mmoja kujeruhiwa vibaya. Hii imetokea baada ya waasi kuwalia Ambushi..

RIP Soldierz
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vilivyoko Sudan vinadai kuwa Kulfi kuwa na mapigano makubwa yameyosababisha Askari Saba wa JWTZ kupoteza maisha leo.


========
Ieleweke kuwa:
Askari wetu kule ni peacekeepers na si peace enforcers. Peace keepers huwa wanakuwa hatarini zaidi kwani hawaruhusiwi kushambulia mpaka watakapoanzwa. Kutokana na hilo mara nyingi huwa wanakuwa victims wa ambush attacks.

Hawa ni tofauti na walioenda Kongo kwani wa Kongo ni peace enforcers na wameruhusiwa kushambulia targets hata kama hawajachokozwa mradi objective yao itimie.
attachment.php


***********
Gazeti la Mwananchi - Julai 14, 2013
Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.

Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.

Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.

Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji.

Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.

Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.

Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur.

Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC.

Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanzania imepeleka wanajeshi 850.

“Tanzania imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na ushauri kwa nchi nyingi,” alinukuliwa Kanali Mgawe, na kueleza kuwa majeshi ya Tanzania yamekuweko katika vikosi vya kulinda amani huko Lebanon, Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya Comoro na Liberia. Liberia waliuawa wanajeshi wa Tanzania 11.

“Tanzania daima haiendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa,” alisema.
 

Attachments

  • IMG_2206.JPG
    IMG_2206.JPG
    70.7 KB · Views: 42,385
Futa kauli au jipange kutupa habari za uhakika. Iweje unaskia alafu iwe News Alert. Toka nje; shuwaiin"!

Kwa nini umekuwa na jazba kiasi hicho kwa Inno laka? Jukwaa hili ni sehemu ya kupeana taarifa mbalimbali. Amefanya kosa gani kutupatia taarifa aliyoipokea kutoka kwa mtu aliyeko Sudan? Hakuna kosa kusema News Alert, kwa sababu habari yenyewe alikuwa amepewa na mtu, bado hajapata jinsi ya kuithibitisha kutoka vyanzo vingine. Kazi yetu wanajamvi ni kuipokea, halafu kuichunguza uhakika wake kutoka kwenye vyanzo vingine. Wahenga walisema subira yavuta heri!

R.I.P. Askari wetu!
 
Hii ni habari nzito inayobeba hisia ya nchi ya inaweza pia kuvuruga amani ya nchi maana watu wana ndugu zao na watoto huko sudani kwaiyo si kila tetesi ambayo unaonma inabeba tension ya taifa kwa ujumla uipunch huku.mods futa hii thread till the relevant authourity proves the fact or more supporting evidence is brought hereby.
 
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vilivyoko Sudan vinadai kuwa Kulfi kuwa na mapigano makubwa yameyosababisha Askari Saba wa JWTZ kupoteza maisha leo.

Taarifa zaidi nitawaletea nitakavyozithibisha
 
Inasemekana ni askari mmoja amekufa baada ya logistic base kuwa ambushed na kushambuliwa. Hao 8 sijasikia. Source: New York Times.
 
Hii ni habari nzito inayobeba hisia ya nchi ya inaweza pia kuvuruga amani ya nchi maana watu wana ndugu zao na watoto huko sudani kwaiyo si kila tetesi ambayo unaonma inabeba tension ya taifa kwa ujumla uipunch huku.mods futa hii thread till the relevant authourity proves the fact or more supporting evidence is brought hereby.

The relevant authority they normally reverse the truth...especially taarifa zenye kugusa taifa
 
These boys are executing their legal mandate...when it comes to falling down, we all should feel sad and sorry for the fallen heroes. I hope the number is not that big. But in any war, there should be casualties, unfortunately.
 
kweli hizi habari sio za kuandika kwa furaha maana tuna ndugu zetu wanaiwakilisha Nchi na Afrika kwa ujumla.
Kwa mtu asiyejua kazi ya Mwanajeshi na wanaapa nini ndio anaweza kushangilia
Mimi naamini ni habari ya UONGO kabisa laba huyo mmoja na ni lazima maiti yake iletwe na aagwe kiheshima
Tufuatilie hilo New York Time
 
Wanajeshi wetu wamevamiwa na waasi huko Sudan.

Askari mmoja kapoteza maisha!

New york times!
 
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vilivyoko Sudan vinadai kuwa kulfi kuwa na mapigano makubwa yameyosababisha Askari Saba wa JWTZ kupoteza maisha leo,taarifa zaidi nitawaletea ,nitakavyozithibisha,

If that's the case inaonyesha tuna wanajeshi wengi sana walioko Darfur.
 
Ukishaamua kuwa mwanajeshi, kifo sio suala la kushangaza maana wapo wengine wanaofariki mafunzoni hata kabla ya kugika viwanja vya mapambano...
 
Kazi za Majeshi ni kugangamara...,nakumbuka kipindi kile nipo j.k.t.....hii nyimbo tulikuwa tukiimba Sana..
 
Bado M 23, bado Kagame! Kisa kutaka umaarufu kwa waume wa magharibi. R. I. P
 
Back
Top Bottom