Arusha yarindima kwa risasi! Jambazi laua polisi

Jesuit - Hao sio wapiga kura wa Lema, ni Jimbo la Arumeru Mashariki bila shaka, ila Arusha kunajulikana kwa kuhifadhi majambazi, eneo hilo la barabara mpya ndiko ile barabara iliyochongwa mya kupandisha mlimani kulekea kunakosemekana kwa mh EL! Na ni mojawapo vilivyoibua hija ya kama EL ni mmasai au MMeru. Kwenye ambush kama hii hakuna wa kulaumiwa, ni vita na askari anaweza kupoteza maisha kwani vifaa vyao havifuniki mwili mzima, ninawapa pole askari polisi kwa kazi hii ngumu sana ya ulinzi na usala wetu (pampoja na madhaifu yenu).
 
Great thinker,
Unadhani kujua english ndo kuelimika?

English: the language used in britain, the US, Australia and other countries, other example of languages are Nyaturu, chagga, digo and zanaki!

Education: process of being taught a particular subject theoritical and practical!

Nawasilisha![/QUOTE]

UMEWASILISHA JAMBO LA MAANA MKUU_NINE NGWITIKA,......KIND OF MENTAL SALVE
 
Hawa polisi sijui kwanini hawajifunzi kuwa makini wanapoenda kufanya 'raid'. Mimi nakumbuka nilishawahi kumtishia polisi mmoja na bastola ya toy, yaani alitoka nduki huyo utasema mwanamke anakimbia wabakaji.
Mwita 25, katika bandiko lako nanusa harufu ya udhalilishaji wa kijinsia! Wanawake hawawakimbii wabakaji ila wanapambana na wabakaji.
 
P1031272.JPG

KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA BW THOBIAS ANDENGENYE AKIZIPANGA RISASI
AMBAZO ZILITUMIKA KATIKA TUKIO LA KUUA ASKARI KATIKA ENEO LA SHANGARAI

KATIKA hali isioyokuwa ya kawaida askari polisi F 228 Constebo Kijanda Mwandru amefariki dunia, pamoja na mkuu wa upelezi wilaya Faustine Mwafele kujeruliwa vibaya na jambazi sugu mkoani hapa ambaye amejulikana kwa jina la Hendry Samson Kaunda. Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Andengenye Thobias alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saakumi za alfajiri.

Kamanda Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo lilitokea mara baada ya askari hao kwe nda kwa ajili ya upekuzi katika nyumba ya Bi Agness Silas ambayo ilikuwa ikitumika kwa ajili ya makazui ya majambazi mjini hapa. Alibainisha kuwa mara baada ya askari hao kufika katika eneo la tukio kwa bahati mbaya jambazi hendry aliwavamia askari hao na kisha kuwapiga kwa risasi mfulululizo hali ambayo ilimsabbishia kifo askari huyo pamoja na kumjerui Mrakibu huyo wa wilaya ya Arusha vijijini.

Pia alisema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo polisi waliendelea na msako mkali katika nyumba hiyo ya Bi Agness ambayo ilikuwa inasadikiwa kuwaficha na kuwatunza majambazi na kisha kukuta vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vinatumika kwa ajili ya shuguli za ujambazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Alitaja Vifaa hivyo kuwa ni pamoja na risasi 36,risasi 12 aina ya Short gun ,kitako kimoja cha bunduki aina ya Shortgun,pamoja na soksi za kuvaa usoni ambazo walikuwa wakizitumia majambazi hayo katika shuguli mbalimbali za uhalifu.

Bw Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo watoto wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi ambapo watoto hao ni DainessMsawe(9) pamoja na Alex Paramina (13) ambaye ndiye aliyefumfungulia mlango Jambazi aliyeuwa na kujerui askari polisi. Aidha mrakibu wa jeshi la polisi bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Selian wakati polisi ikiendelea na msako dhidi ya majmbazi hayo yaliyokimbia.
 
Nimewahi shuhudia siku polisi nchi fulani waliposhtukia jambazi ameingia kuiba sehemu, polisi wako waangalifu, nyumba ilizungukwa na makamandoo wa kipolisi huku kila mmoja ameshika bunduki kwa mikoni miwili kuilenga nyumba alimo jambazi mfano kama tuonavyo michezo ya movie za ulinzi au kigaidi vile, magari 18 yakiwa na askari wasiozidi 24 yalimiminika ndani ya eneo within 5 minutes baada tu ya emergence call. Wakinyata kwa uangalifu huku wakisubiri kikosi maalum ambacho baada ya kuwasili muda mfupi dakika 7 za emergence call tangu waarifiwe kilikuwa na mbwa wasiopungua wanne.

Barabara na vipenyo vyote ambavyo ni rahisi kupata upenyo wa kukimbia zililindwa na baadhi ya magari yaliyofika huku mawasiliano mtindo mmoja na haku gari lililoruhusiwa kuingia wala kutoka eneo la tukio. Baada ya kuizingira nyumba walikata umeme na kuruhusu mbwa waingie kumsaka jambazi huku nje wakiwa makini na kusikiliza kinachoendelea ndani na trigger tayari zimeshikiliwa kwa mikono miwili wameilenga nyumba ile wakiwa wamevaa zile vulana za kuzuia risasi. Mbwa walifanikiwa kulinasa jambazi na kuanza kumchanachana kwa meno ndipo polisi walipotinga ndani kumchukua jambazi kiulani na kisha kumpeleka hospitali kutibiwa chini ya uangalizi wao akiwa na zile scuff mkononi na baadaye kupelekwa kituoni.

Baada ya shughuli ile nzito nilienda kuwapa mikono na kuwapongeza, nao walikuwa na mifano mingi sana tu ya kunisimulia yatokeayo katika kazi zao na waliniambia wanajitahidi kushika mtu salama si kuua, na wanatumia kila njia ya kuhakikisha mtu anashikwa mzima huo ndio ufundi na maelekezo ya kazi yetu unaotakiwa tufanye vinginevyo tukiua tutakuwa tumeharibu kesi na mengi yaliyofichika hayatafichuka. Polisi wetu wanaenda kuvamia jambazi kama wanavyovamia maandamano ya amani yanayofanywa. Polisi wetu kuna dalili nyingi za kutotumia ujuzi na mbinu zao za kikazi, vinginevyo kwa mwendo huu wanaweza kuwashika wachovu tu na waandamaji wanaoandamana kwa amani.

Kisa hiki si cha kusimuliwa, bali nilishuhudia live na nilikiri utendaji wao uliotukuka, na katika nafasi ile walivyozingira hakuna pakutokea, nashangaa wao walizingira na kisha mtu mmoja kuwazidi kwa kuua, kujeruhi na kisha kutoroka, hii ni aibu sana kwa askari walijipanga kumzingira mhalifu halafu jambazi ambaye hakujipanga awashinde nguvu na kutoroka. Sina maana nafurahia kuuawa na kujeruhiwa polisi, ila inaonyesha udhaifu mkubwa uliopo ndani ya jeshi la polisi, na sasa naelewa kwa nini wakiitwa kwenye tukio hufika masaa kadhaa wakati mhusika alishafanya uhalifu na kukimbia. Iweje wananchi wenye hasira wasijichukulie sheria
 
watoto wameingizwa kwenye system mapema hivi. hii ni hatari

Kosa si la askari wadogo, ila ni la wakubwa kwa maana kwamba askari hufanya kazi kwa maelekezo kutoka mkuu wao kiongozi ambaye naye huelekezwa na wakuu wke wa juu. Hapa naona kama ule mtindo wa kupeana vyeo kwa kujuana madhara ndio haya. Makosa kama haya kwenzetu ni somo la kutorudia kosa kama hilo next time.
 
Mkuu CandidScope, hii picha mbona imenikumbusha mbali sana!! Kama huyo jamaa kulia nilidhani ni Mzee Mahita enzi zile za KAFU Ngangari na IGP Kada wa CCM Ngunguri.

Poleni sana IGP Mwema pamoja na familia za wafiwa na mliojeruhiwa mkitutumikia umma wa Tanzania.

P1031272.JPG

KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA BW THOBIAS ANDENGENYE AKIZIPANGA RISASI
AMBAZO ZILITUMIKA KATIKA TUKIO LA KUUA ASKARI KATIKA ENEO LA SHANGARAI

Bw Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo watoto wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi ambapo watoto hao ni DainessMsawe(9) pamoja na Alex Paramina (13) ambaye ndiye aliyefumfungulia mlango Jambazi aliyeuwa na kujerui askari polisi. Aidha mrakibu wa jeshi la polisi bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Selian wakati polisi ikiendelea na msako dhidi ya majmbazi hayo yaliyokimbia.
RIP askari aliyefariki, amekufa kishujaa!. Concern yangu ni kwa hao watoto under 14, innocent victims of circumstances, vyama vya haki za binaadam, vifuatilie treatment ya hawa watoto.

Japo sishabikii ujambazi, wala siungi mkono mauaji yaliyofanyika, lakini nafsi yangu imefarijika hilo jambazi lilivyofanikiwa kuwatoroka polisi na kutokomea!. Kwa sababu, lingepatikana, lingekuwa tortured to death na taarifa ya polisi ingesema limeuwawa katika kurushiana risasi, na Arusha ni very notorious kwa ujambazi na polisi wauawaji!.

Nimesema nimefarijika kwa sababu bado niko na kumbukumbu jinsi washukiwa wanne wa ujambazi ambao walichukuliwa wakiwa wazima na afya zao, wakapelekwa kituo cha polisi cha Arusha Ijumaa moja mwaka juzi. Kesho yake jumamosi na jumapili ndugu na jamaa zao walitaka kuwaona ndugu zao, walikataliwa kata kata. Jumatatu asubuhi wale ndugu wakaambiwa wafuatilie ndugu zao Hospitali ya Mt. Meru. Kufika hospitali, wakaambiwa polisi wameleta miili ya watu wanne waliowaokota mitaani baada ya kuuliwa na wananchi wenye hasira!.

Walipokabidhiwa miili ya ndugu zao kwa maziko, walishuhudia dilapidated bodies due to torture!. Kumbe polisi waliwauwa watuhumiwa hao siku ile ile ya Ijumaa walipowachukua, miili wakaipeleka polisi Jumapili usiku kujustfiy they know nothing. The story ended up there. Hakuna inquery, hakuna maelezo yoyote ya ziada, na wala no any complain was filed anywhere to anybody!. Ndio maana nimesema, afadhali jambazi katoroka!
 
Do you really mean it Pasco?
 
Do you really mean it Pasco?
Kengemumaji, I really mean it!, from the bottom of my heart!. Nimefarijika, jambazi kaua polisi wazembne na kusepa, kuliko angelikamatwa, angeliuawa kwa mateso! torture!.

Tena sio hivyo tuu, pia sikufurahishwa Kasusura alipokamatwa, wala siungi mkono hata kidogo, kila siku mwizi wa kuku anapouwawa kwa kuchomwa moto huku mijizi ya EPA ikiambiwa irudishe ilichokwiba na hakuna kesi!.

Kwa kifupi sipendi kabisa kuona damu, hata ya panya!, kama kuna namna yoyote ya kumuua panya kwa sumu, naiunga mkono, sipendi abamizwe na kutoka damu!. Ndio maana nimehadharisha, siungi mkono ujambazi, wala siungu mkono polisi wazembe kuuliwa!
 
Kosa si la askari wadogo, ila ni la wakubwa kwa maana kwamba askari hufanya kazi kwa maelekezo kutoka mkuu wao kiongozi ambaye naye huelekezwa na wakuu wke wa juu. Hapa naona kama ule mtindo wa kupeana vyeo kwa kujuana madhara ndio haya. Makosa kama haya kwenzetu ni somo la kutorudia kosa kama hilo next time.
Nadhani hapa ana wazungumzia watoto waliolifungulia jambazi ambao watoto hao wamekamatwa...
 
Huenda si jambazi ni mtu wa TISS hajatekeleza maagizo ya wakuu hvyo njia ya kumwondoa ni kubambika kuwa ni jambazi
 
Nimestushwa na habari ya kifo cha rafiki yangu mpendwa Kijanda Mwandu(Danny). bado naona kama naota vile: Kijada nilimaliza naye Form Six kule Shinyanga, nitaendelea kukumbuka upole nauhaminifu wake aliokuwa nao. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
 
Back
Top Bottom