Arusha - polisi aliyehusika wizi $ 50,000 atoroshwa!

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Mpwapwa(1).jpg

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa

Polisi atoweka, akwepa tuhuma

ASKARI Polisi anayedaiwa kuhusika na wizi wa dola za Marekani 50,000 za kidhibiti katika kituo kikuu cha Polisi jijini hapa, ametoroka na familia yake. Askari huyo (jina limehifadhiwa) anadaiwa kutoroka usiku wa manane wakati Tume maalumu ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema, ikiwa inaendelea kuhoji polisi na raia juu ya upotevu wa fedha hizo. Awali askari huyo, aliwekwa rumande na mwenzake, lakini walipewa dhamana baada ya kuandika maelezo kwa viongozi hao wa juu wa Polisi mkoani hapa juu ya wizi huo.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alipoulizwa alikiri kuwekwa ndani kwa askari hao, lakini alikataa kutaja majina yao kwa sababu za kichunguzi juu ya suala hilo. Mbali ya askari huyo kutoweka, askari kanzu mwingine mwenye cheo cha Konstebo (jina tunalo), alikamatwa juzi jioni na anashikiliwa katika kituo kikuu cha Polisi kwa madai ya kufahamu mtandao mkubwa wa wizi jijini hapa na kuhusika na wizi wa fedha hizo.

Mpwapwa alipoulizwa jana kwa njia ya simu juu ya kutoweka kwa askari huyo na familia yake, na mwingine kukamatwa, alisema yeye yuko nje ya mji, labda inawezekana ikawa kweli au la, lakini kwa kuwa yuko nje ya ofisi hilo hatalizungumzia. ''Mimi niko Karatu kikazi labda huyo askari alitoroka wakati nikiwa huku na kama kuna mwingine, nikirudi kesho (leo) nitapata taarifa kwa ukaribu zaidi na kupata ukweli wake,'' alisema Mpwapwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kukamatwa kwa askari kanzu huyo kulitokana na taarifa kutoka kwa raia wema kuwa askari huyo alihusika moja kwa moja na upotevu wa dola hizo. Habari zilisema kuwa konstebo huyo piaanadaiwa kumiliki magari ya kisasa jijini Arusha, zaidi ya 10 yakiwamo yaliyokodishwa na mengine kubeba abiria - teksi.

Vyanzo vya habari vilisema kwamba baadhi ya askari kanzu ambao wanafanya kazi karibu na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Arusha (RCO) ambao walikuwa zamu siku ya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa nao tayari wamehojiwa na Tume hiyo ya IGP.

Fedha hizo za kigeni sawa na Sh milioni 90 zinazodaiwa kuwa sehemu ya dola za Marekani
200,000 zilizoporwa zilioneshwa mahali ziliko na mmoja wa watu watatu wanaosadikiwa
kuhusika na ujambazi wa kutumia usafiri aina ya pikipiki maarufu jijini Arusha kwa jina la
Toyo ama Bodaboda.

Fedha hizo dola 50,000 ziliyeyukia mikononi mwa polisi katika mazingira ya kutatanisha.

Watuhumiwa hao wa ujambazi walifanya uhalifu huo hivi karibuni kwa kumpora dereva wa gari la hoteli maarufu ya kitalii ya jijini hapa ya Kibo Palace, Onesmo Joseph (28), dola
200,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 340.

Habari Leo
 
Sasa ametoroka,au ametoroshwa?
Ni uzembe wa hao AL SHABAB wa tz,mabingwa wa kupiga mabom wanafunzi,ulinzi 'F'
 
Sasa ametoroka,au ametoroshwa?
Ni uzembe wa hao AL SHABAB wa tz,mabingwa wa kupiga mabom wanafunzi,ulinzi 'F'

Kuna dalili za kutoroshwa kwa kuwa alikuwa mahabusu, kisha wakubwa wake wakamtoa na kumwacha huru, kwa hali ilivyo ni mchezo fulani uliofanywa na wakubwa wake kumtorosha ili kuvuruga ushahidi baada ya boss wao kuunda tume.

Cha kushangaza atoroke na familia yake, ni jambo lisilo rahisi kufanya hivyo isipokuwa kwa utaratibu wa mipangilio iliyowahusisha zaidi ya familia yake na kabisa wakubwa wake, usafiri alipata wapi hadi atoroke na familia yake yote?
 
Kama kweli ametoroka basi hapa kuwa watu wa kuwajibika tena bila subra!
 
polisi wa kituo cha kati Arusha ni ''genge'' yaani wao ndio wacheza mishe... Wanaweza wakashika mirungi yote afu usiku baadhi ya askari wanasambaza kwa wauzaji wao, afu wengi wao ni matajiri sijui ni mshahara tu? yaani polisi wa cenral Arusha ni hela ! Watu wametumwa hela kwa hiyo haramu yeyote wanapiga hawaangalii.. Ndio aina polisi tulionao
 
Ni kawaida sana kutoroshwa au kufichwa kukwepa kesi.

Kumbuka wale wa January 5, wamepiga waandamanaji risasi na hawaonekani waliko
 
Huyo askari bure kabisa! Dola 50,000 ndo zinamsababisha akimbie? Zitamsaidia nini hizo? Khaaaaaa....!!!
 
Huyo askari bure kabisa! Dola 50,000 ndo zinamsababisha akimbie? Zitamsaidia nini hizo? Khaaaaaa....!!!

Mkubwa!

Kwa kweli kwa hili si amekimbia kwa sababu tajwa hapo juu,Mi nahisi amebeba shilingi ya kutosha. Na kwa kuwa tupo hapa mjini hakika tutasikia mengi juu ya tukio hili.
 
Huyo askari bure kabisa! Dola 50,000 ndo zinamsababisha akimbie? Zitamsaidia nini hizo? Khaaaaaa....!!!

Sishabikii wizi wa huyo askari. Lakini kama unafikiri hiyo ni pesa ndogo kwa askari wa cheo kidogo, fuatilia ujue Prof Shivji alilipwa kiinua mgongo dola elfu ngapi baada ya miaka mingi ya utumishi uliotukuka. Inawezekana huko uliko hiyo ni pesa ndogo sana, lakini kwa askari wa kawaida Tanzania, hiyo ni pesa iliyo nje ya ndoto zake.
 
Hivi yule askari anayedaiwa aliamriwa na Zombe kuua wale wafanyabiashara wa madini kutoka mahenge alishapatikana?..polisi ya Tz ni zaidi ya tunavyoijua!
 
Kuna dalili za kutoroshwa kwa kuwa alikuwa mahabusu, kisha wakubwa wake wakamtoa na kumwacha huru, kwa hali ilivyo ni mchezo fulani uliofanywa na wakubwa wake kumtorosha ili kuvuruga ushahidi baada ya boss wao kuunda tume.

Cha kushangaza atoroke na familia yake, ni jambo lisilo rahisi kufanya hivyo isipokuwa kwa utaratibu wa mipangilio iliyowahusisha zaidi ya familia yake na kabisa wakubwa wake, usafiri alipata wapi hadi atoroke na familia yake yote?

Nilipo kuwa shule,nilidhani hadithi ya nchi ya kusadikika si halis lakini TZ inaelekea huko kwa kasi!
 
Sishabikii wizi wa huyo askari. Lakini kama unafikiri hiyo ni pesa ndogo kwa askari wa cheo kidogo, fuatilia ujue Prof Shivji alilipwa kiinua mgongo dola elfu ngapi baada ya miaka mingi ya utumishi uliotukuka. Inawezekana huko uliko hiyo ni pesa ndogo sana, lakini kwa askari wa kawaida Tanzania, hiyo ni pesa iliyo nje ya ndoto zake.

Hebu tujuze Mkuu, Professor Shivji alilipwa chini ya hiyo $50,000? Na kama chini ya hapo, ni asilimia ngapi ya hiyo amount? My God!
 
Huyo askari bure kabisa! Dola 50,000 ndo zinamsababisha akimbie? Zitamsaidia nini hizo? Khaaaaaa....!!!

Hata angeendelea kufanya kazi usikute hz pesa asingezipata kwny maisha yake!?
 
Wakuu wana JF hapo Arusah, tujuzeni majina ya huyo polisi.......Ngongo, PJ mpo hapo?
 
Nilipo kuwa shule,nilidhani hadithi ya nchi ya kusadikika si halis lakini TZ inaelekea huko kwa kasi!
Kwa Arusha hayo mambo ni kawaida kuna rafiki zangu Wa kwaya fulani ya kanisa waliibiwa kinanda cha kwaya ya kanisa kilikamatwa mahali kikapelekwa hapo Polisi Arusha baada ya siku moja kiliyeyuka hadi Leo hakijulikani kilipo mimi mwenyewe nilishaingiliwa na majambazi walibeba TV 2 computer 1 music sistem tulikamata Tv 1 kamera 1 viliyeyukia hapo Polisi,katika kufuatilia hivo vitu mara jamaa wakwambie wananjaa uwalishe mara tax baadaye niliona nazidi kuishiwa hela na nimepoteza nikaamua kuacha kila kitu, hiyo ndiyo Polisi ya TZ hasa Arusha wanajua tu kuzuia maandamano na mikutano ya siasa tu
 
Back
Top Bottom