Arusha - polisi aliyehusika wizi $ 50,000 atoroshwa!

Jeshi la Polisi Arusha linatakiwa kufumuliwa lore kuanzia ngazi ya juu hadi chini, ndiyo maana akin Zuberi wanakiburi wanajua wanachokifanya
 
polisi wa kituo cha kati Arusha ni ''genge'' yaani wao ndio wacheza mishe... Wanaweza wakashika mirungi yote afu usiku baadhi ya askari wanasambaza kwa wauzaji wao, afu wengi wao ni matajiri sijui ni mshahara tu? yaani polisi wa cenral Arusha ni hela ! Watu wametumwa hela kwa hiyo haramu yeyote wanapiga hawaangalii.. Ndio aina polisi tulionao
Mimi polisi sinaga imani nao hata siku moja hata nikiwa na mawe ni kheri niombe washkaji wanisindikize Bank kuliko polisi, mimi ninawadharau sana hawa watu kama wapo tayari kuunga mkono makosa ya barabarani kwa Ths1000 tu sembuse kukuua ili wajipatie pesa zako ulizotaka zifike Bank salama.
 
Polisi atoweka, akwepa tuhuma


Mpwapwa alipoulizwa jana kwa njia ya simu juu ya kutoweka kwa askari huyo na familia yake, na mwingine kukamatwa, alisema yeye yuko nje ya mji, labda inawezekana ikawa kweli au la, lakini kwa kuwa yuko nje ya ofisi hilo hatalizungumzia. ‘’Mimi niko Karatu kikazi labda huyo askari alitoroka wakati nikiwa huku na kama kuna mwingine, nikirudi kesho (leo) nitapata taarifa kwa ukaribu zaidi na kupata ukweli wake,’’ alisema Mpwapwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kukamatwa kwa askari kanzu huyo kulitokana na taarifa kutoka kwa raia wema kuwa askari huyo alihusika moja kwa moja na upotevu wa dola hizo. Habari zilisema kuwa konstebo huyo piaanadaiwa kumiliki magari ya kisasa jijini Arusha, zaidi ya 10 yakiwamo yaliyokodishwa na mengine kubeba abiria - teksi.

Habari Leo
Kuwa nje ya kituo cha kazi hakuwezi kumfanya bwana Mpwapwa asipewe taarifa ya jambo tena kubwa kama hilo ambalo lipo hot kwa sasa limetokea katika himaya yake. Hapa naona anatudanganya.

Mara nyingi nimekuwa nikisema, ninavyoamini mimi, Nowadays there is a very thin line differentiating Polisi with Criminals kama vile ninavyoshindwa kumtofautisha Mganga wa kienyeji na Mchawi, maana ni mtu huyo huyo, akiroga anaitwa Mchawi, ukimkuta anaagua anaitwa Mganga. Si tumesikia wale waliowapora wafanya biashara wa Mahenge? Si kuhizi ni salama ukutane na Vibaka usiku kuliko ukutane na Polisi. Naogopa msije mkani-Kibanda/Mwigamba bure, I am just thinking loudly.

 
Kuna dalili za kutoroshwa kwa kuwa alikuwa mahabusu, kisha wakubwa wake wakamtoa na kumwacha huru, kwa hali ilivyo ni mchezo fulani uliofanywa na wakubwa wake kumtorosha ili kuvuruga ushahidi baada ya boss wao kuunda tume.

Cha kushangaza atoroke na familia yake, ni jambo lisilo rahisi kufanya hivyo isipokuwa kwa utaratibu wa mipangilio iliyowahusisha zaidi ya familia yake na kabisa wakubwa wake, usafiri alipata wapi hadi atoroke na familia yake yote?


Hivi yule askari aliyemuua Zombe yuko huru au bado yuko lupango? Jibu la swali hili linaweza likawa muongozo mzuri ktk mjadala wa uzi huu
 
Kwa Arusha hayo mambo ni kawaida kuna rafiki zangu Wa kwaya fulani ya kanisa waliibiwa kinanda cha kwaya ya kanisa kilikamatwa mahali kikapelekwa hapo Polisi Arusha baada ya siku moja kiliyeyuka hadi Leo hakijulikani kilipo mimi mwenyewe nilishaingiliwa na majambazi walibeba TV 2 computer 1 music sistem tulikamata Tv 1 kamera 1 viliyeyukia hapo Polisi,katika kufuatilia hivo vitu mara jamaa wakwambie wananjaa uwalishe mara tax baadaye niliona nazidi kuishiwa hela na nimepoteza nikaamua kuacha kila kitu, hiyo ndiyo Polisi ya TZ hasa Arusha wanajua tu kuzuia maandamano na mikutano ya siasa tu

Matatizo yameanzia pale vyombo vya uslama vinapofanya kazi ya kisias badala ya wajibu wao wa kulinda nchi na usalama wa raia. Kiwango cha chini cha mishahara kinafanya vyombo vya usalama kuwa na hali ngumu ya maisha na hivyo kujichukulia njia ya mkato kupata cho chote wawapo katika majukumu yao ya kila siku, na wanaoumia ni raia ambao wanajiweka rehani kwa vyombo vya usalama.
 
Hivi yule askari aliyemuua Zombe yuko huru au bado yuko lupango? Jibu la swali hili linaweza likawa muongozo mzuri ktk mjadala wa uzi huu

Sijakupata vizuri na comment yako, unaweza kutoa ufafanuzi zaidi nikuelewe?
 
Kuna dalili za kutoroshwa kwa kuwa alikuwa mahabusu, kisha wakubwa wake wakamtoa na kumwacha huru, kwa hali ilivyo ni mchezo fulani uliofanywa na wakubwa wake kumtorosha ili kuvuruga ushahidi baada ya boss wao kuunda tume.

Cha kushangaza atoroke na familia yake, ni jambo lisilo rahisi kufanya hivyo isipokuwa kwa utaratibu wa mipangilio iliyowahusisha zaidi ya familia yake na kabisa wakubwa wake, usafiri alipata wapi hadi atoroke na familia yake yote?

hiyo ni syndicate mkuu. you can not be a succesfull gangster without having close ties with the law enforcers. huu mchezo since day one ulikuwa very organized.
 
Back
Top Bottom