real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,287
Kutoka jijini Arusha AyoTV imezipata taarifa za diwani wa kata ya Daraja Mbili Arusha Prosper Msofe katika jimbo la Arusha Mjini amejiuzulu nafasi yake nakuhamia CCM kwa madai ya kumuunga mkono Raisi Magufuli.
Pamoja na mambo mengine Prosper Msofe amesema CHADEMA kimekuwa chama kinachoongozwa na Mbunge Lema katika mkoa wa Arusha na ameadai kuwa meya amekuwa akikataa kuambiwa ukweli.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia amekiri kupokea barua hiyo na zikiwemo barua za madiwani wengine wa CHADEMA kujiuzulu nafazi zao hizo kwa madai wa kuhamia CCM.
Chanzo: Millard Ayo
-------------
Madiwani wawili wa Chadema kutoka Arusha Mjini wamehamia CCM muda huu.
Diwani wa kata ya Daraja Mbili Ndg. Prosper Msofe na Diwani wa kata ya Terrat Ndg.Obeid Meng’oriki (Chadema) wamejiuzulu uanachama na udiwani leo hii na kutangaza kujiunga na ccm kwa kile walichoeleza kuwa wamefanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Mh Rais Magufuli.
Diwani mmoja amesema; "Hakuna maisha magumu kisiasa kama kuishi kwenye Ukoo wa kambale ambao Baba, Mama na watoto wote wana Ndevu. Agenda hakuna, kila Mtu mropokaji na kulazimishana kufanya siasa za kuhujumu maendeleo kama njia ya kuijenga Chadema badala ya Nchi. Tukiendelea na siasa za namna hii, itafika wakati tutaambiwa tukabomoe Madaraja na kuiba pampu za miradi ya maji?
Tumekataa siasa hizi za kishetani na tunawaomba Watanzania wazikatae pia."