CHADEMA wakiwa kwenye ubora wao walihamasisha hadi Joh Makini na wenzake kutunga wimbo wa kiharakati uitwao Bye Bye

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
703
1,757
Wakuu tukiacha masikhara na tukiwa wakweli lazima tukiri kuna miaka CHADEMA ilikuwa ya moto mno kisiasa. Ilikuwa haishikiki. Jijini Arusha na wilaya za jirani walikuwa hawaambiwi kitu kuhusu CHADEMA. Jamaa walikiwasha sana. Mwaka 2005 - 2015 zilikuwa ni zama za dhahabu kwa CHADEMA. Ilikuwa imekamilika kuanzia BAVICHA hadi taasisi nyingine zote chini ya CHADEMA. Kwa Arusha walikuwa wakipata sapoti kubwa kwa siri kutoka kwa wanaCCM baadhi. Ninakumbuka miaka ya 2011 hadi 15 ilikuwa kuona mtu kavaa mavazi ya CCM ni hadi uende CCM Mkoa au kwa mzee mmoja muuza magazeti kona Ilboru. Sapoti ilikuwa kubwa.

Baada ya tukio la Januari 5, 2011... CHADEMA walipata kiki kubwa mno ya kisiasa hadi kupelekea Joh Makini na wenzake kutunga wimbo wa kiharakati kuhusu kilichotokea. Bahati mbaya 2015 mwenyekiti na genge lake wakacheza kamari iliyokipoteza mazima CHADEMA hadi kesho. Itachukua miaka mingi sana kuja kupata chama cha upinzani kama CHADEMA ya 2005 - 2015. Hii ya sasa ni ya hovyo mno. Imejaza waropokaji wasioweza kujenga hoja yoyote. Zamani kiongozi mwandamizi wa CHADEMA akisimama atatema madini hadi nchi inatetemeka ila kwa sasa kiongozi mwandamizi anasimama na kuropoka "BODABODA NI KAZI YA LAANA". CHADEMA ya hovyo mno kuwahi kuwepo.

Nimekuwekea wimbo usikilize.
 

Attachments

  • Joh_Makini_ft_G_Nako_-_Bye_Bye.mp3
    3.9 MB
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom