Arumeru Mashariki: Wanachama na viongozi UVCCM kuhamia CHADEMA

"Malaika hushangilia mbinguni mwenye dhambi mmoja anapotubu" tunayo sababu ya kufurahi pamoja, tuwakaribishe ili washike mwenendo mpya na mungu awasaidie.
 
Kweli Chadema mmeishiwa mmeamua kutunga habari halafu mnasingizia Gazeti la Mwananchi.

Ebu tusaidie mkuu Mwananchi ya lini imetoa hiyo habari, kama la leo hiyo habari ipo ukurasa wa ngapi?

Na bado kwa hiyo umeamua kuwafariji Chadema wenzako.
 
Mkuu hawa lazima waishie kwenye korido kwanza, ndo maana nikasema wastegemee posho ndani ya CHADEMA!!
Yale magamba yao lazima yakwanguliwe kwanza na yafanyiwe uhakiki(hii si chini ya 4yrs)!!
...mm! mkuu hivi ukimkwangua kobe lile-gamba lake anaweza kuendelea na maisha kweli?...
 
wanatoka ccm kwa dhati au kwa sababu wamekosa vyeo maana wasije wakaenda chadema wakaendeleza gamba lao ambalo haliwezi kuvulika.

cdm magamba yakishidikana kuvuliwa yanachunwa kama ngozi au kuwashwa moto bila kujali aliye nalo atakufa au anapona case study madiwani wa Arusha!!!
 
Mods,
Kuweni makini JF inataka kugeuzwa sehemu ya porojo mtu anatunga habari halafu analeta jamvini anasingizia gazeti la Mwananchi...tafuteni gazeti la Mwananchi hakuna hii habari.
 
Mods,
Kuweni makini JF inataka kugeuzwa sehemu ya porojo mtu anatunga habari halafu analeta jamvini anasingizia gazeti la Mwananchi...tafuteni gazeti la Mwananchi hakuna hii habari.

Arumeru kumekucha Send to a friend
Monday, 05 March 2012 20:50
0digg

Waandishi Wetu
WAGOMBEA wa vyama vitano vya upinzani, walijitokeza jana kuchukua fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki kimyakimya.

Wagombea hao, akiwamo mgombea wa Chadema, Joshua Nasari aliyesindikizwa na Meneja wa kampeni wa chama hicho, Vicent Nyerere ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Musoma mjini, walikabidhiwa fomu hizo jana na Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Trasias Kagenzi.

Baada ya kuchukua fomu mgombea huyo wa Chadema ambaye aliandamana pia na Mratibu wa chaguzi za Chadema, Basil Lema ambaye ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, walitembelea Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo,Mercy Silla na kumsalimia.

Wagombea wengine waliochukua fomu, Abraham Chipaka wa Chama cha TLP, Shabani Moyo Kirita wa Chama cha SAU , Charles Msuya kutoka Chama cha UPDP na Mohamed Abdalah Mohamed wa Chama cha DP mara baada ya kukabidhiwa waliondoka.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Kagenzi alisema wagombea wote hao, walifika katika ofisi za tume na barua za uteuzi wa vyama vyao kama ambavyo taratibu zinaruhusu.

"Tunatarajia wagombea zaidi wajitokeze leo na kesho(leo) kwani muda wa mwisho wa kuchukua fomu na kurejesha ni Mach 8,"alisema Kagenzi.

Habari kutoka ndani ya CCM zinaeleza mgombea wa chama hicho, ambaye alikuwa jijini Dar es Salaam, anatarajia leo kuchukua fomu saa 5:00 asubuhi.

Nasari atoa vipaumbele vyake.

Akizungumza mara baada ya kuchukua Fomu, Nasari alisema ana imani kubwa ya kushinda na akichaguliwa kipaumbele chake kitakuwa ni kuondoa migogoro ya ardhi, kero za afya, maji, elimu na miundombinu.

"Nimekuwa nikisema Meru tuna ardhi ya kutosha, hakuna sababu ya watu kuhamishwa, kwani kuna mashamba makubwa yanamilikiwa na watu wachache, pia tutasimamia sera za kuwa na zahanati kwa kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata," alisema Nasari.

Uchaguzi huo, unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge, Jeremiah Sumari na utafanyika Aprili mosi kwa kushirikisha wapigakura 127,000 wa tarafa tatu za jimbo hilo lenye kata 17.

Msimamizi uchaguzi anawajua Chadema

Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Meru, Trasias Kagenzi, anaweka historia ya kusimamia uchaguzi wa mdogo wa pili ndani ya mfumo wa vyama vingi kwani pia alikuwa msimamizi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime.

Katika uchaguzi huo uliotawaliwa na vurugu kubwa, Wagombea wa Chadema wa ubunge, Charles Mwera na Udiwani wa Kata ya Tarime mjini John Heche wote walishinda kujaza nafasi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Chacha Wangwe.

Akizungumzia uchaguzi wa Tarime na sasa Meru, Kagenzi alisema ana imani uchaguzi wa Meru utakuwa na usalama na hautakuwa na vurugu kama za Tarime.

"Sidhani kama huku kutakuwa na vurugu kama zile, nimewaona Wameru hawapendi vurugu", alisema Kagenzi.

Kwa upande wake mratibu wa Uchaguzi wa Chadema, Basil Lema ambaye pia alikuwa akiratibu uchaguzi wa Tarime, alisema wana imani kubwa na Kagenzi kwani sasa ni mzoefu wa chaguzi ndogo.

"Huyu Mkurugenzi tunabahati naye sana kwani kila eneo ambalo tumekuwa na uhakika wa ushindi tumemkuta," alisema Lema

CCM: hatutambui
tuhuma za rushwa

Wakati huohuo, Meneja Kampeni wa CCM katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Mwigulu Nchemba amesema chama hicho, hakitambui tuhuma za kusambaza rushwa ambazo zilikuwa zinamkabili Siyoi Sumari ambaye kateuliwa na chama hicho kugombea Jimbo la Arumeru Mashariki na hivyo ni msafi.

Akizungumza jana, Nchemba ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM na Katibu wa Uchumi na Fedha wa chama hicho, alisema CCM inaongozwa kwa kufuata misingi ya sheria hivyo hawajawahi kupata taarifa ya Sumari kutiwa hatiani.

"CCM tunaongozwa kwa kufuata sheria, hizi tuhuma za rushwa hazijachunguzwa na CCM kwani hatuna chombo hicho hivyo mgombea wetu ni safi," alisema Nchemba.

Meneja huyo, alisema kazi kubwa iliyokuwa inafanyika katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM, ilikuwa ni kumtafuta mgombea sahihi wa chama hicho na sasa amepatikana.

Wakati wa mchakato wa marejeo ya kura za maoni Makada watatu wa chama hicho, Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Wilaya ya Nyamagana ambaye aligombea pia jimbo hilo, Elirehema Kaaya, Katibu wa UVCCM Monduli Ezekiel Mollel na Diwani wa Kata ya Mbuguni, Thomas Mollel maarufu kama Askofu, walikamatwa kwa mahojiano kutokana na tuhuma za rushwa.

Makada hao wa CCM, walidaiwa kuwa katika kambi ya Siyoi hata hivyo baada ya mahojiano waliachiwa na wote walikanusha tuhuma hizo na kueleza ni sehemu ya siasa chafu za makundi zilizopangwa kuwachafua.

Azungumzia mpasuko ndani ya CCM Arusha

Akizungumzia mpasuko wa chama hicho, uliotokana na kura za maoni, alisema anatarajiwa kukutana na wagombea wote walioshiriki katika mchakato wa kura za maoni na wapambe wao ili kuweka mambo sawa.

"Tayari nimefika Arusha kwa kazi hii moja kwanza kuunganisha makundi haya na pili kuzungumza ili tuweze kuanza kampeni za kuhakikisha tunashinda katika uchaguzi huu," alisema Nchemba

Nchemba ambaye pia alikuwa meneja kampeni wa chama hicho Jimbo la Igunga, alisema CCM ina uhakika wa ushindi katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

Wakati huohuo baadhi ya Wanachama wa CCM katika Kata ya USA River ambao wagombea waliokuwa wanawaunga mkono walishindwa na Sumari katika kura za maoni leo wanatarajia kujiunga na Chadema.

Akizungumzia suala hilo, Anaeli Mungure alisema hawajaridhiwa na uamuzi ya Kamati Kuu ya CCM, kumpitisha Siyoi kwani wanaamini hakupata kihalali nafasi hiyo.

"Sisi tunapinga uteuzi kwani haikuwa halali Sumari kupita, juzi tumepeleka ushahidi wetu Takukuru kwani vitendo vya rushwa vilitawala", alisema Mungure.

Alisema leo baadhi yao, wakiwamo pia baadhi ya viongozi wa UVCCM katika jimbo hilo, wanatarajia kujiunga na Chadema.

Bendera zawa kivutio
BENDERA za vyama vya CCM na Chadema zimeonekana kuwa kivutio kikubwa katika hekaheka za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani ambapo kwa sasa bendera hizo zimeonekana zikining"inia katika miti, milingoti, magari pamoja na kwenye paa za nyumba mbalimbali za wakazi wilayani humo.

Wilayani Arumeru kwa sasa mgeni akipita katika maeneo mbalimbali hususani pembezoni mwa barabara ya Moshi /Arusha watakutana na bendera za vyama hivyo viwili zikipepea hali ambayo imekuwa ni kivutio kwa wageni na wenyeji wilayani humo.

Wakati bendera za CCM zikionekana kuzagaa kwa wingi katika maeneo ya Tengeru na Usa River bendera za Chadema zimeonekana kuzagaa katika maeneo ya Maji ya Chai na Leganga ambapo madereva wa bodaboda waliopo Kituo cha Leganga wameonekana kuhamasika kuzitumia bendera za chama hicho.

Hata hivyo, wakati bendera hizo zikipepea wilayani humo tayari vyama hivyo viwili vimeanza kuwapa masharti makada wake kusimamia vyema bendera hizo kikamilifu kwa lengo la kuzilinda huku vikiwataka wale wote waliozembea hadi kusababisha bendera hizo kushushwa bila sababu za msingi kujieleza mbele ya chama.

Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumza katika zoezi la kura za maoni ndani ya chama hicho zilizompatia ushindi Joshua Nassari alikaririwa akiwaamrisha makada wa chama hicho kuzining'iniza bendera za chama hicho kwenye nyumba zao na sio kwenye miti.

Dk Slaa alienda mbali zaidi na kuwaonya makada wote watakaozembea bendera zao kushushwa na wapinzani wao bila sababu za msingi wataitwa mbele ya vikao ili kujieleza ni kwa nini wameachia bendera hizo kushushwa.
Alisisitiza kwamba tayari uongozi wa chama hicho ngazi ya taifa unafanya jitihada za dhati kuhakikisha wanatuma bendera za kutosha ili ziletwe wilayani humo kwa lengo la kutumika.

Kwa upande wake, CCM mkoani Arusha kupitia kwa Katibu mwenezi wake, Loota Sanare alikataa kuzungumzia masuala ya bendera zao kwa madai kwamba masuala ya bendera ni mikakati ya siri ya chama chao na kamwe hawawezi kuitangaza hadharani mbele ya vyombo vya habari.

Habari hii imendaliwa na Moses Mashalla, Arumeru, Mussa Juma, Arusha
 
Kweli Chadema mmeishiwa mmeamua kutunga habari halafu mnasingizia Gazeti la Mwananchi.

Ebu tusaidie mkuu Mwananchi ya lini imetoa hiyo habari, kama la leo hiyo habari ipo ukurasa wa ngapi?

Na bado kwa hiyo umeamua kuwafariji Chadema wenzako.
Shule kitu muhimu sana ndugu, wacha kukurupuka kwa jambo ambalo huna ufahamu nalo.
 
Kweli Chadema mmeishiwa mmeamua kutunga habari halafu mnasingizia Gazeti la Mwananchi.

Ebu tusaidie mkuu Mwananchi ya lini imetoa hiyo habari, kama la leo hiyo habari ipo ukurasa wa ngapi?

Na bado kwa hiyo umeamua kuwafariji Chadema wenzako.
Unachamba sana...si kila kitu wewe lazima uwe unajua..

Monday, 05 March 2012 20:50
0diggsdigg

Waandishi Wetu
Azungumzia mpasuko ndani ya CCM Arusha

Akizungumzia mpasuko wa chama hicho, uliotokana na kura za maoni, alisema anatarajiwa kukutana na wagombea wote walioshiriki katika mchakato wa kura za maoni na wapambe wao ili kuweka mambo sawa.

"Tayari nimefika Arusha kwa kazi hii moja kwanza kuunganisha makundi haya na pili kuzungumza ili tuweze kuanza kampeni za kuhakikisha tunashinda katika uchaguzi huu," alisema Nchemba

Nchemba ambaye pia alikuwa meneja kampeni wa chama hicho Jimbo la Igunga, alisema CCM ina uhakika wa ushindi katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

Wakati huohuo baadhi ya Wanachama wa CCM katika Kata ya USA River ambao wagombea waliokuwa wanawaunga mkono walishindwa na Sumari katika kura za maoni leo wanatarajia kujiunga na Chadema.

Akizungumzia suala hilo, Anaeli Mungure alisema hawajaridhiwa na uamuzi ya Kamati Kuu ya CCM, kumpitisha Siyoi kwani wanaamini hakupata kihalali nafasi hiyo.

"Sisi tunapinga uteuzi kwani haikuwa halali Sumari kupita, juzi tumepeleka ushahidi wetu Takukuru kwani vitendo vya rushwa vilitawala", alisema Mungure.

Alisema leo baadhi yao, wakiwamo pia baadhi ya viongozi wa UVCCM katika jimbo hilo, wanatarajia kujiunga na Chadema.

Mashibuda hao, ina maana leo ndio wanaujuwa ubaya wa CCM? hawa ni malaya wa kisiasa.
JB Wiser unasema kweli, njaa kwenye siasa ni mbaya kweli!. Hawa jamaa ni njaa tuu ndizo zinazowasumbua, hawajajua ukweli wa Chadema, kule watajifia njaa bure na kutamani kurudi walikotoka!.

Ila pia kufuatia ruzuku ya haja, Chadema nako ni alihamdidulahi kuna chochote kitu na fungu nililosikia lililotengwa kwa Arumeru si haba!, angalau kuna chochote kidogo kitu!.
 
Hatupokei waadhirika wa siasa za ccm, inaonekana siyo wapganaji hao, wahakikishe kwanza wanapgania haki huko huko! itakuaje siku wakifanyiwa mbaya CDM watahamia chama ipi kama si kurudi CCM tena. CDM, please pay sensitive attention upon those ccm victims!
 
Narudia tena Source ya hiyo habari sio gazeti la Mwananchi, mie napinga hiyo Source yako kuweka Mwananchi...kwa yoyote mwenye gazeti la Mwananchi la leo atakubaliana na mie.
 
JB Wiser unasema kweli, njaa kwenye siasa ni mbaya kweli!. Hawa jamaa ni njaa tuu ndizo zinazowasumbua, hawajajua ukweli wa Chadema, kule watajifia njaa bure na kutamani kurudi walikotoka!.

Ila pia kufuatia ruzuku ya haja, Chadema nako ni alihamdidulahi kuna chochote kitu na fungu nililosikia lililotengwa kwa Arumeru si haba!, angalau kuna chochote kidogo kitu!.
Pasco usiniaibishe, 90% ya maandishi yako yanataja pesa, jaribu kuondoka huko fikiria ukombozi wa kifikra, wengine tumejitahidi hatutawaliwi na tamaa hizo, ndiyo maana mengi ya mabandiko yako bila kutaja bahasha hujakamilisha. Pasco don't be so cheap, kumbe unapom-support Lowassa ni kwa vile unajua endapo atafanikiwa atakufikiria?
 
Wasome kwanza sera na muongozo wa Chadema kabla ya kujiunga, hatuhitaji watu wa msimu na opportunists
 
Back
Top Bottom