Arumeru Mashariki: Wanachama na viongozi UVCCM kuhamia CHADEMA

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Baadhi ya Wanachama wa CCM katika Kata ya USA River ambao wagombea waliokuwa wanawaunga mkono walishindwa na Sumari katika kura za maoni leo wanatarajia kujiunga na Chadema.

Akizungumzia suala hilo, Anaeli Mungure alisema hawajaridhiwa na uamuzi ya Kamati Kuu ya CCM, kumpitisha Siyoi kwani wanaamini hakupata kihalali nafasi hiyo.

"Sisi tunapinga uteuzi kwani haikuwa halali Sumari kupita, juzi tumepeleka ushahidi wetu Takukuru kwani vitendo vya rushwa vilitawala", alisema Mungure.

Alisema leo baadhi yao, wakiwamo pia baadhi ya viongozi wa UVCCM katika jimbo hilo, wanatarajia kujiunga na Chadema.

Source: Mwananchi
 
waje kwa ustaarabu, chadema ina utaratibu wake, lazima wauheshimu hatutaki mamluki.
 
pia kuna CCM makundi matatu. wao wapo kundi lipi! manake kama ni lile la waagizaji kama kina nape CDM mnakaribisha migogoro
Mkuu hawa lazima waishie kwenye korido kwanza, ndo maana nikasema wastegemee posho ndani ya CHADEMA!!
Yale magamba yao lazima yakwanguliwe kwanza na yafanyiwe uhakiki(hii si chini ya 4yrs)!!
 
wanatoka ccm kwa dhati au kwa sababu wamekosa vyeo maana wasije wakaenda chadema wakaendeleza gamba lao ambalo haliwezi kuvulika.
 
Isijekua ni kuambukizana ugonjwa,coz sijajua mpaka sasa ni yeye kumwaga pesa(rushwa) au sio mtu wao waliyemtaka?
 
Hawa lazima tuwafundishe kwanza uzalendo maana wametoka huko na magamba yao na ulafi wao wa madaraka huku tunawakwangua kwanza magamba yao kwa wembe halafu tunayachoma moto na mwili wao tunauosha kwa omo then wanajiunga na kuwa wanachama safi.
 
Tuwe makini na watu wa aina hii,tukumbuke hawaji cdm kwa sababu wanaipenda bali wanaenda cdm ili kukomoa wenzao,they are not good ppo,tuwakaribishe ila tuwe makini nao sana
 
KANU pia ilikufa haraka kwa sababu ya kuhamwa na wanachama! Huu ni uelekeo mzuri wa kuimaliza CCM! CHADEMA wapokeeni.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom