April Fools

Status
Not open for further replies.
Hivi hii siku inaisha saa ngapi? Ni mpaka jioni au mchana.

Kwa wenzetu huko ambapo siku hii ilianzishwa inaisha saa6 kamili mchana.
Lakini hapa Bongo inaisha usiku wa manane ikiwezekana wiki nzima.
 
this is not funny, we shouldnt encouraging these kind of threads simply because its fools day, please you should put your thread in jokes forums you prick!
 
Jamani hebu naomba mnisaidie kumfahamu huyu MJINGA aliyeanzisha siku ya WAJINGA.. Na naomba mnisaidie kuna faida gani ya hii siku ya WAJINGA?? Na kama watu mnaisherehekea(Mimi siitambui) je nae ni MJINGA? Mi naona ni UJINGA mtupu.. Kwa nini tukubali siku wa WAJINGA? MJINGA ana faida gani katika jamii.. Huu ni UJINGA
 
Jamani naomba tusitumie April Fools' Day vibaya pamoja na kwamba nami bila kukusudia karibu nimeingie mkenge.Inasikitisha sna unapovutiwa na kichwa cha habari just to realise it is just a prank. Kuna jukwaa la Jokes tulitumie hilo.
Nawasilisha
 
binafsi simjui aliyeianzisha

nafikiri wanasaidia kidogo kufurahisha manake utakuta ujinga mwingie hadi mtu anatabasamu. naona baadhi ya post zinatoa changamoto ya watu kutafakri kabla ya kukubali kitu. nindhani kuwa kuwtokana na uangalifu unaochukuliwa katika habari siku hii ya wajinga inawezekana ndiyo siku wasomaji wa habari htafakari zaidi habari kuliko siku nyingine amabapo huzitrust habari zote kirahisi. na kama hilo ni kweli, inawezekana basi siku hii ndiyo siku pekee ya werevu na zilizobaki zote katika mwaka ndizo siku halisi za wajinga.

mfano habanri ya Tendwa kishukia CCJ/Mpendazoe, aikuwa na sifa yoyote ya kuitwa habari, na yoyote mwente tafakari hata ndogo tu angegundua ni a kutunga. sasa huoni kuwa imetoa changamoto kwa wale walioingia mkenge kuwa siku nyingine watafakari kila habari?

anagalia magazeti kaa ya udaku na hata baadhi ya magazeti yasiyo ya udaku. utagundua kuwa habari makini ni chache sana. sasa wale wanayoyaamin hayo magazeti huoni wanapaswa kuonywa watafakari kila habari?

ni maoni yangu ndugu
 
Tutajuaje wanaijua?

Yaani kila mtu anataka aanzishe thread ya april fool. hivi ukiihadhimisha hii sherere si unakuwa fool au?
 
Waingereza na makoloni yao walikuwa wanawalazimisha Wafaransa washerehekee mwaka mpya siku ya tarehe 1 January, lakini Wafaransa wakawa wanataka waendelee kusherehekea mwaka mpya tarehe 1 April. Kuona hivyo, Waingereza wakawa wanawatumia pongezi za kejeli Wafaransa kuwapa heri ya mwaka mpya kila inapofika April mosi.Basi kejeli na mizaha ikaendelea na hata wafaransa walipokubaliana na mfumo wa Gregorian calendar wa kusherehekea mwaka mpya tarehe Mosi January, ikawa imeendelea kutumiana pongezi za kejeli kejeli kila April Mosi na hadi ikawa siku ya wajinga.
 
this fools day thing is annoying yani hatutosoma kitu cha maana leo coz everyone is putting up a futile attempt to be funny..hahaha NOT!
 
Hata kama ni fool's day tujitoe tu. Kenya wamefanya kitu mbaya kufanya kampeni kali kuzuia tusiuze meno ya tembo tani nyingi zinaozea pale ivory room! Undugu gani huu usio wa kufaana?
 
Jamani hii siku mbona ina vituko namna hii na habari za kimzahamzaha! Kwa nini ikaitwa siku ya wajinga?

Hii siku ya wajinga duniani watu wameiharibu kabisa na sasa nafikiri isiitwe tena siku ya wajinga bali siku ya UONGO NA MIZAHA duniani.

Hebu fikiria uko na jamaa yako wote mmeingia kazini. Halafu baada ya muda jamaa yako anakuja kukwambia unaitwa na bosi ofisini, halafu unaenda kwa bosi anakwambia sijaita mtu yeyote hapa. halafu huyo jamaa yako anarudi kwako na kusema mbona hajaniita halafu unajibu leo ni siku ya wajinga. Hivi huyu aliyeitwa na bosi kwani ni mjinga?

Pia kuna ishu zingine ambazo tunasema hizi ndio haswa za wajinga. Mfano:
Kama hizi zilizotumwa leo kama Mrema, Mbatia wajiunga na CCJ lakini hata hii sio kwasababu ni kweli hawa jamaa wakiamua wanaweza kujiunga na chama hicho. Halafu kuna hii Osama bin Laden kuwasili nchini leo. Kwa hii mtu ambaye haelewi unaweza kusema hii ndio siku yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom