Ansbert Ngurumo: Tuwasikilize wahaini hawa wa CCM

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Tuwasikilize wahaini hawa wa CCM

Na Ansbert Ngurumo

SIKUSHTUSHWA na kauli ya ukali ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kwamba kuna watu ndani ya chama chao wanataka kumwondoa mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete, na kuweka mwenyekiti mwingine kabla ya 2015.

Katika kujibu mapigo ya vijana wenzake waliomkosoa yeye na wenzake wanaodai kwamba nchi hii ni ya CCM; na katika kuwatunishia misuli vijana hao na wote anaodai wako nyuma yao, Nape alisema wote wanaofikiria kumwondoa Rais Kikwete kwenye uenyekiti ni wasaliti na wahaini.

Kauli ya Nape inazusha maswali mengi. Kwanza, wapo wanaojiuliza kama alichosema ni chake au alitumwa na Rais Kikwete. Wanaojua hali ya mambo ndani ya CCM, wanajua fika kuwa alichokisema Nape si kipya ndani ya CCM.

Kumekuwa na fukuto ndani ya CCM, linalotokana na hisia kwamba chama kimedorora, kimekuwa legelege. Matokeo yake na serikali imekuwa legelege. Maana yake ni kwamba iwapo wataendelea na uongozi wa aina hii hadi 2015, ni vigumu CCM kushinda uchaguzi.

Kwa hiyo, makundi kadhaa ya wanaokitakia mema chama chao wanadhani wakati wa kufanya mageuzi ndani ya CCM ni sasa. Na wanataka kuanza na uongozi wa juu, ili kukisuka vema chama na kukipa mwelekeo.

Wanakiri kwamba uongozi wa sasa umepwaya. Ambacho hawajakubaliana ni nani azibe nafasi ya Rais Kikwete. Baadhi ya mapendekezo yanayotolewa yanawalenga wastahafu kadhaa wanaosikilizwa, ambao huko nyuma wameonyesha uwezo wa kuongoza.
Hata hivyo, kundi hili linakosa jambo moja – ujasiri wa kusema hayo kwenye vikao rasmi vya chama. Wanaogopa kusema kwa sababu wanajua mwenyekiti wao haoni kile wanachoona wao.

Hajakubali kwamba ameshindwa kuongoza chama. Hakubaliani nao kwamba CCM imekuwa legelege mikononi mwake. Hivyo, hayupo tayari kumpisha yeyote achukue nafasi yake kabla ya muda aliofikiria yeye kung’atuka.
Na kwa kuwa mwenyekiti wao ni rais, wanaogopa pia nguvu ya dola ambayo anaweza kuitumia kuwashughulikia wale wanaotamani aachie uenyekiti kabla ya 2015.

Nadhani mamlaka haya ya dola aliyonayo Rais Kikwete ndiyo yanampatia Nape jeuri ya kuwasema wanaotaka mabadiliko hayo, kwani anajua analindwa na yule anayemtetea. Na kwa hakika, wengi wanasema kwamba Nape ametumwa kuwatisha wanaotamani mageuzi hayo. Kauli ya Nape si yake hasa, ni ya Rais Kikwete.

Pili, wote wenye akili timamu hawakubaliani na Nape kwamba kutamani kubadilisha uongozi unaoonekana dhahiri kwamba umeshindwa ni uhaini. Si mapinduzi ya serikali; bali ni mwamko wa kutaka kufanya mabadiliko ya uongozi wa chama ili kukiimarisha kwa ajili ya ushindani makini siku za usoni.

Hawa wanatambua kwamba jamii pana ya Watanzania sasa inaliona hilo, na ndiyo maana, miongoni mwa sababu nyingi zilizopo, wananchi wanakiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Wanajua kuwa CCM hii ya Rais Kikwete, kama itaendelea kufa kila siku namna hii, haitaweza kufua dafu mbele ya nguvu ya umma. Kwa maneno mengine, wanataka kumsaidia Rais Kikwete kukivusha chama katika uchaguzi ujao.

Wengine wanadiriki kusema kwamba kukijenga upya chama hicho ndiyo maana halisi ya dhana ya kujivua gamba. Na ndiyo jinsi ya kukiondolea ombwe la uongozi linalokikabili. Maana niliwahi kuandika kwamba dhana ya kuvuana magamba ilichochewa na harakati za baadhi ya wanachama kupendekeza kwamba Rais Kikwete na Yusuph Makamba wapumzishwe majukumu ya uongozi waliyonayo.

Mwenyekiti akajiwahi, akayateka mapinduzi kwa kumpumzisha katibu mkuu ili kupoza hasira; na akaanzisha vuguvugu la kujivua gamba kwa kuwanyoshea vidole wengine.

Tatu, Nape amefanya lile alilopaswa kuzuia. Amewasaidia Watanzania wote kutambua kwamba ndani ya CCM mambo yameharibika kiasi hicho, kwamba hata wanawaza kumwondoa mwenyekiti wao.

Ingawa hali hii ilijulikana kwa baadhi yao ndani ya chama, kauli ya Nape imetangazia taifa zima kile ambacho yeye alitaka kiwe siri, na kiwe mwiko. Kwa maana nyingine, amewahamasisha hata wana CCM wengine kuanza kutafakari mustakabali wa chama chao. Amewasaidia kuanza kufikiria udhaifu wa mwenyekiti wao, na kuwaza nani anaweza kuziba nafasi hiyo.

Ingawa si lazima mabadiliko hayo yatokee sasa, kwa sababu Rais Kikwete naye anajaribu kwa nguvu zake zote kuyazuia, kauli ya Nape imeacha kovu. Hata kama kidonda kitapona, alama inabaki; kovu linaonekana.

Nape angeweza kumfichia Rais Kikwete udhaifu wake huu kwa njia mbili – ama kwa kutolizungumza kabisa hadharani, au kwa kuwasaidia wanaotaka kumwondoa mwenyekiti wafanye hivyo kistaarabu ili kuhakikisha chama hakimeguki, na anayeondoka hajihisi kudhalilika.

Nne, kauli ya Nape imezusha swali la msingi. Kumetokea kitu gani ndani ya CCM hadi baadhi ya wanachama na viongozi wawaze kumwondoa Rais Kikwete kwenye uenyekiti wake? Katika mazingira yasiyo na dosari kubwa, kwa chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambaye pia ni rais wa nchi, si rahisi kwa viongozi kuanzisha mchakato wa kumwondoa kiongozi mkuu katika nafasi yake.

Swali hili, pamoja na kwamba linawagusa wana CCM na wananchi wengine wanaofuatilia siasa za CCM, linamgusa mwenyekiti mwenyewe.
Angepaswa kujiuliza kwa nini kwa mara ya kwanza katika histosia ya CCM viongozi na wanachama wao wanaona mwenyekiti amevaa viatu vinavyompwaya!

Kuwapuuza na kuwatisha wanaowaza hivyo hakusaidii kukijenga chama chao. Wanaweza kunyamaza kwa vitisho hivyo, lakini hakuna atakayeweza kuzuia kile wanachokipanga kimya kimya.

Na hata kama watasitisha mpango wa kumwondoa mwenyekiti sasa, atabaki kuwa mwenyekiti asiye na nguvu, asiye na mvuto na asiye na kauli.

Atakuwa ni mwenyekiti aliyetikisika, ambaye anadhani njia pekee ya kujiimarisha kwenye kiti ni kuwatikisha wanaomtikisa, au kuwasaliti wale anaodhani ndio wanamsaliti.

Na mwenyekiti akishatikisika, chama chake kitakuwa legelege tu. Na kwa kuwa ndicho kilicho madarakani, itatoka wapi serikali imara?
Kwa hiyo, ingawa kwa macho ya kipropaganda wanaweza kuonekana wasaliti na wahaini kwa kufikiria kubadilisha uongozi wa chama chao, yawezekana wanafanya uhaini wa kukijenga na kukiimarisha ili kukipa mustakabali chama chao.
Wakati mwingine nadhani wasaliti na wahaini hawa wa CCM ni watu muhimu sana. Hebu kwanza tuwasikilize!


Source: Tuwasikilize wahaini hawa wa CCM
 
Ni kweli inshu hiii imo chamani, watu wanataka sasa kofia ya urais na uenyekiti wa chama itenganishwe. Jk hakubaliani japo wanaoasisi haya wana nguvu, kwanza anaona kukubaliana nao atajidhihirisha namna alivochoka na pili atapunguziwa rungu la kuendesha mambo kadiri anavotaka kama vile kumpachika mgombea anayemtaka for 2015
 
Ni kweli inshu hiii imo chamani, watu wanataka sasa kofia ya urais na uenyekiti wa chama itenganishwe. Jk hakubaliani japo wanaoasisi haya wana nguvu, kwanza anaona kukubaliana nao atajidhihirisha namna alivochoka na pili atapunguziwa rungu la kuendesha mambo kadiri anavotaka kama vile kumpachika mgombea anayemtaka for 2015

Ni kweli, ila nani wa kumfunga paka kengere CCM?
 
Kofia mbili noma, mtu anatetea kwa nguvu zote ... ati uhaini .... wakati utendaji wa kofia zote mdogo....
 
Hivi sasa uwezo wa JK hata ukatibu kata kwake ni mzigo. Apumzishwe tu kukinusuru chama.
 
Ni kweli inshu hiii imo chamani, watu wanataka sasa kofia ya urais na uenyekiti wa chama itenganishwe. Jk hakubaliani japo wanaoasisi haya wana nguvu, kwanza anaona kukubaliana nao atajidhihirisha namna alivochoka na pili atapunguziwa rungu la kuendesha mambo kadiri anavotaka kama vile kumpachika mgombea anayemtaka for 2015
Hii kitu nafikiri kama inaungwa mkono na wanaccm wengi WAMECHANGANYIKIWA! Mtu mnaetaka kumtoa kuongoza chama mnamtetea kuwa anaongoza nchi vizuri! Mtu ashindwe chama aweze nchi! Hao wote wanafiki! Waroho wa madaraka wanafanya hivyo kulenga 2015.kwanza hizi harakati zinafanywa kwa siri kwani wanataka kupindua nchi? Chama si chao? Watangazie umma dhamira yao na kutupa faida yake na wakiri aliyepo sasa kashindwa! Hawana lolote hawa! Mabadiliko yatafanywa na umma tena kwa uwazi na si hawa wezi tu wanafanya mambo gizani! Hawa ndio mafisi hawatabakiza hata mifupa! Bagladeshi!!!!
 
Swali kwako Ngurumo, zikitenganishwa kofia kwa kumuengua JK, nani awe Mwenyekiti wa CCM, Lowasa, Bashe, RA, au nani vile!!! Ngurumo ameshindwa kutambua kwamba yanayokisibu hivi sasa CCM sio suala la kiongozi mmoja, bali ni suala la kikanuni zaidi katika maisha. CCM imefika kikomo, lazima kiondoke madarakani, hakuna marefu yasiyo na ncha.

Jambo la msingi inaloweza kufanya CCM ni kuanda mazingira mazuri zaidi ya kisiasa ili hata waking'olewa waweze kurudi tena madarakani huko mbeleni, na hilo ni kuwa tayari kutengeza katiba yenye masalahi kwa taifa na sio kwa chama kilichopo madarakani.
 
Ngurumo ameishiwa ...

Hapana amekushika kubaya tu wew wala si kuishiwa .Ngurumo ni mwiba mno na kichwa kile.Mtoto wa Kipalapale Seminary hebu gusa unate .Ukitakakujua Ngurumo mwisho muulize Salva .Aliwahi kwend hadi UK kumtafuta ili asiunge mkono UPinzani na ache kuandika makala.Ritz anajua maaa alikuwa anaratibu mpango .Jibu likawa Ngurumo had no price tag hata sasa wanachachawa .Unataka tumwage zaidi ??
 
Hapana amekushika kubaya tu wew wala si kuishiwa .Ngurumo ni mwiba mno na kichwa kile.Mtoto wa Kipalapale Seminary hebu gusa unate .Ukitakakujua Ngurumo mwisho muulize Salva .Aliwahi kwend hadi UK kumtafuta ili asiunge mkono UPinzani na ache kuandika makala.Ritz anajua maaa alikuwa anaratibu mpango .Jibu likawa Ngurumo had no price tag hata sasa wanachachawa .Unataka tumwage zaidi ??

Good now I know why he so bitter with JK..kumbe seminary bana! ok
 
Swali kwako Ngurumo, zikitenganishwa kofia kwa kumuengua JK, nani awe Mwenyekiti wa CCM, Lowasa, Bashe, RA, au nani vile!!! Ngurumo ameshindwa kutambua kwamba yanayokisibu hivi sasa CCM sio suala la kiongozi mmoja, bali ni suala la kikanuni zaidi katika maisha. CCM imefika kikomo, lazima kiondoke madarakani, hakuna marefu yasiyo na ncha.

Jambo la msingi inaloweza kufanya CCM ni kuanda mazingira mazuri zaidi ya kisiasa ili hata waking'olewa waweze kurudi tena madarakani huko mbeleni, na hilo ni kuwa tayari kutengeza katiba yenye masalahi kwa taifa na sio kwa chama kilichopo madarakani.
We are still there there Nsensi! Nchi itafaidika na nini wakifanikiwa lengo lao la kumtoa?unafikiri umuhimu wa mfumo huo umepitwa na wakati au another finger to Mwl Nyerere kwa kuasisi huu mfumo? Unadhani hao wanapigana chini chini kubadili hili ni akina nani? Mbinu nyingine tu hizi za kimtandao tandao! Madaraka tu haya ya Urais wala si maslahi ya nchi!
 
JK yuko sahihi sana kumtumia Nepi ktk hili maana chama kama ccm ambayo ilijifia tangu siku nying hakiwezi kuhimili kuwa na watu be wenye infuence kubwa ndan ya nchi yetu hii. Hebu tuangalie ukweli je EL anaweza kuwa mwenyekiti au mzee 6 mmh na rahis wetu abaki salama kweli. Maana ili tuweze kuwa ktk hali hii n ngumu sn... Tuangalie mambo haya vzr kwa ccm hii ambayo kila mwanachama ana fundo lake moyon, mawazo yake mmh n ngumu sana... Labda kama wangekuwa wamoja
Ni kweli, ila nani wa kumfunga paka kengere CCM?
 
Ama kweli waseminary wanaitesa ccm kweli. Dr. Slaa, Mnyika nawengineo ambao ni matunda ya seminary.
 
Ama kweli waseminary wanaitesa ccm kweli. Dr. Slaa, Mnyika nawengineo ambao ni matunda ya seminary.

Wako obssessed na JK tu..

Tukimuweka John (mwanakondoo mwenzao) watanyamaza kimya kama kondoo ccm hao juu

Tunajua what they want ..tunajua ugonjwa wa udini waliofundishwa kanisani
 
Niliwahi kusema msaada pekee anaohitaji nMk we re kwa sasa ni kutopigiwa kura anapogombea ili apumzike maana mzigo mkubwa unamwelemea ameshindwa kuubeba na kuutua hawezi sasa wana nccm msaidieni mumtue huo mzigo no vote for mk we re
 
Apatae uongozi kimtandao huondolewa kimtandao pia ni suala la muda tu,na endapo wana magamba wanaona jk hawezi kukiongoza chama ambacho kina takribani wanachama milioni tano sembuse nchi yenye watu arobaini na nne na zaidi?????mwanzo yaliposemwa haya juu ya uwezo wa jk kuongoza nchi magamba walikuwa wabishi sana kama walivyobisha suala la ufisadi liliposikika kwa mara ya kwanza mwembeyanga, sasa naona wameanza kuelewa kuwa jk ni kilaza puuu!!!!!!!!hafai mwondoeni kukinusuru chama chenu.
 
Back
Top Bottom