Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

BABA SANIAH

JF-Expert Member
Oct 20, 2013
4,503
5,699
Habari za wakati huu wadau wa jukwaa hili.

Nilikuwa napitia katika mitandao ya kijamii, nikakutana na hii habari ya huyu mlimbwende Angelina Jolie.
Ya kwamba aliadopt watoto, mmoja wapo anatokea Ethiopia anaitwa Zahara, tangu kakiwa kachanga kabisa kama miezi mitano hivi.

So hiyo tu na watoto wengine pia kama watatu hivi, kuna wa kiume mwenye asili ya Asia na Kuna mwingine mzungu.

Na amekuwa akiwatunza mpaka Sasa, kasheshe inakuja Kwa huyu Binti Toka Ethiopia, kwamba kashakuwa mzuri na mama yake anaanza kuleta longolongo kuhusu mwanawe, wakati Angelina Jolie alimchukua kama orphan yaani yatima.

Anyway sijui itaishia wapi.

Kwa anaefahamu au mwenye kujua zaidi tujadili japo kidogo,

1. Hivi sisi wabongo tunaweza fanya hiki alichofanya huyu Angelina Jolie? Jinsi tulivyo na miroho yetu ilivyo mibaya?

2. Sisi blacks mbona tunajidhalilisha sana, Kwa mfano huyu mama wa Zahara Binti wa Angelina Jolie? Leo ndo anamuona mzuri? Zahara kanoga, kapendeza, na anafaa kabisa Kwa matumizi ya binadamu(Kwa sisi wanaume tu).

3. Binafsi nampongeza sana huyu Angelina Jolie Kwa alichokifanya kuadopt hao watoto, ningekuwa na uwezo Ile wa uumbaji basi huyu Pepo inamuhusu kabisa.

1699313829395.jpeg

 
Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakuwa peke yake kwenye safari hiyo alikuwa na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote.

Kwa mtoto wa Ethiopia jina lake Zahara, Angelina alimkuta kituo cha kulea watoto yatima akiwa ana miezi 7 tu, wahusika wa kituo wakamwambia mtoto yule ni yatima wazazi wake walifariki kwa virusi vya Ukimwi, huruma ilimjaa Jolie na kuamua kumchukua kwa taratibu zote stahiki.

Ukweli ukaja kujulikana miaka mitatu baadae, mama mzazi wa Zahara alikuwa hai, ni binti aliyepata ujauzito kwa kubakwa, huku akiishi na bibi yake na mjomba wake wakiwa katika maisha ya ufukara, baada ya kumzaa Zahara hali ilizidi kuwa mbaya, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa.

Mama mtoto alichokiomba ni kuongea na mwanae hata kwa njia ya simu, kumjulisha kuwa ana familia Ethiopia na mama yake hajafa pia anampenda, wala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.
 
Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakua peke yake kwenye safari hiyo alikua na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote,


Wala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.
Wanamchanganya mtoto tu, na Angelina naye hawajamfanyia haki.

This is very selfish.

Ukishakubali kumtupa mtoto wako, umeshakubali, usitake tamaa za kuona mtoto kakua ukataka kuongea naye.

Very selfish mother.
 
Mtoto kama ana maokoto amsaidie tu mama yake japo kuna uongo ulifanywa na kituo kilichokuwa kinamlea kwa angelina, na sidhani kama Angelina atamkataza mtoto kumsaidia biological mother wake au kuwasiliana naye, japo kiukweli mtoto kwa sasa ni wa Angelina.

Angalizo, huyo mama asije tu akaanza zile tamaa za kiafrica kumtaka mtoto kisa kaona anaweza kuponeapo

Ila mtoto kawa pisi aisee
 
Wanamchanganya mtoto tu, na Angelina naye hawajamfanyia haki.

This is very selfish.

Ukishakubali kumtupa mtoto wako, umeshakubali, usitake tamaa za kuona mtoto kakua ukataka kuongea naye.

Very selfish mother.

Ni kweli huyu mama alimtelekeza mtoto kwa bibi yake, alivyosikia mtoto amekwea pipa yupo States ndio akajirudisha akijua atapata kitu.

Selfish Mother indeed.
 
Mtoto kama ana maokoto amsaidie tu mama yake japo kuna uongo ulifanywa na kituo kilichokuwa kinamlea kwa angelina, na sidhani kama angelina atamkataza mtoto kumsaidia biological mother wake au kuwasiliana naye, japo kiukweli mtoto kwa sasa ni wa angelina.

Angalizo, huyo mama asije tu akaanza zile tamaa za kiafrica kumtaka mtoto kisa kaona anaweza kuponeapo


Ila mtoto kawa pisi aisee
Huyo Mama ni mpumbavu tu.
Sana sana ambacho angeweza kufanya ni kumuomba msamaha Binti yake tena hadharani, na Mengine amuachie Binti mwenyewe.

Ila kwa ujumla Mama wa kweli na WA halali wa Binti ni Anjela.
 
Wanamchanganya mtoto tu, na Angelina naye hawajamfanyia haki.

This is very selfish.

Ukishakubali kumtupa mtoto wako, umeshakubali, usitake tamaa za kuona mtoto kakua ukataka kuongea naye.

Very selfish mother.

Umaskini hauna adabu Kiranga. Mimi simlaumu mama yake kwa kumtelekeza kwa bibi. Na Ethiopia kuna dhiki kali hakuna mfano.

Nimekumbuka kuna binti wa kihabeshi alikuwa mzuri mithili ya ajabu, alikuwa anabembeleza aolewe na ndugu yangu apate kubaki bongo akimbie dhiki za kwao. Noma sana haya maisha.
 
Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakua peke yake kwenye safari hiyo alikua na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote,

Kwa mtoto wa Ethiopia jina lake Zahara, Angelina alimkuta kituo cha kulea watoto yatima akiwa ana miezi 7 tu, wahusika wa kituo wakamwambia mtoto yule ni yatima wazazi wake walifariki kwa virusi vya Ukimwi, huruma ilimjaa Jolie na kuamua kumchukua kwa taratibu zote stahiki,

Ukweli ukaja kujulikana miaka mitatu baadae, mama mzazi wa Zahara alikua hai, ni binti aliyepata ujauzito kwa kubakwa, huku akiishi na bibi yake na mjomba wake wakiwa katika maisha ya ufukara, baada ya kumzaa Zahara hali ilizidi kua mbaya, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa,

Mama mtoto alichokiomba ni kuongea na mwanae hata kwa njia ya simu, kumjulisha kua ana familia Ethiopia na mama yake hajafa pia anampenda sana.

Wala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.
Ukichunguza hapo huyo mama mzazi itakuwa keshakutana na wajanja wa mjini na kumwambia kuwa kuna uwezekano akapata bingo.

Huyo mtoto kama angeishia kwenye ufukara wa Ethiopia nina hakika mama wala asingekuwa na haja ya kutaka kumjua mtoto.

Ila kwa sasa hakuna anachoweza kuambilia hata kama akitaka kuleta janja janja. Binti tayari keshatimiza miaka 18.
 
Back
Top Bottom