Angalia AI Midjourney Inafanya Zaidi ya Unachowaza, Hapa Imetoa Matokeo Sahihi kwa Asilimia 96%

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,875
21,551
Habari mkuu.

Naendelea kujifunza na kuwa Inspired sana na hii kitu AI, Midjourney, kadiri inavyobamba na kuzisogeza kwa karibu tasnia mbalimbali, hapa naweza kuzungumzia tasnia ya picha na filamu.

Kwa mfano kwa haraka haraka unaweza kusema nayo hivi; "Mcheza sinema Adam Sandler kiongozi wa filamu ya Mad Max".

Haya ndiyo matokeo .
20230411_201915.jpg


Yaani kwa muda mfupi utapata matokeo tofauti na ya huyo mhusika. Kwa upande mwingine, ikiwa unataka kuongeza, kwa mfano, eneo la jiji la Sao Paul lililopo kwenye sinema iliyorekodiwa na Wong Kar Wahi, kwa haraka sana utaletewa
matokeo hayatakuwa tofauti kabisa na picha unazozitegemea au mtayarishaji wa filamu husika.

Haya ndiyo matokeo 👇🏾.
20230411_201926.jpg


Kupitia vipengele tofauti na vizuri zaidi kama vile mandhari, usanifu, nguo zinazovaliwa au wakati mwingine unazowaza akilini mwako zenye mvuto zaidi, zitaletwa aina kadhaa kama zimepigwa kwa kamera.

Wadau huu mfumo ni man made ila kwa hatua hii naona kabisa wenzetu wanatumia akili zao hasa, yaani hasa.

Kitivo cha sayansi pale Chuo Kikuu chetu cha Dar Es Salaam au pale State University of Zanzibar sijui kuna nini wanafanya au wanasubiri kukopi, kuletewa watengenezaji wa hii mifumo ili waje wawafunde!
 
Back
Top Bottom