Andrew Chenge achukua fomu ya kugombea Uspika. Fahamu kuhusu wasifu wake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,029
219,007
Habari ndio kama mnavyoisikia ndugu zangu, mzee wa vijisenti ambaye inasemekana ana akili nyingi kuliko wagombea wengine wote waliokwishachukua fomu, leo tarehe 12/01/2022 amejitosa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Mbunge_wa_zamani_wa_Bariadi_Magharibi%2C_Andrew_Chenge_leo_Jumatato_Januari_12%2C_2022_amechuk...jpg

WASIFU

KUZALIWA

- Mbobezi wa Sheria Barani Afrika na "Alumni" wa Chuo kikuu bora Duniani- Havard cha Nchini Marekani Mh.Andrew John Chenge alizaliwa mwaka 1947 nchini Tanzania (Tanganyika wakati huo).

ELIMU

- Nguli huyu wa Sheria alianza safari ya kitaaluma katika Shule ya msingi Sasago (Musoma) kati ya mwaka 1955- 1958

- Kisha akajiunga na St. Pius Seminary Makoko Musoma kati ya mwaka 1959-1962

- Kisha akajiunga na St.Mary's Seminary Nyegezi mwanza kati ya mwaka 1963-1966 kwaajili ya masomo ya Sekondari.

- Kati ya mwaka 1967 - 1968 alijiunga na Mkwawa High school.

- Mwaka 1969 alikuwa kati ya wanafunzi wachache waliojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwaajili ya masomo ya Sheria (LL.B) na kufanikiwa kuhitimu kwa ufaulu wa juu mwaka 1972.

- Mwaka 1974 - 1975 alibahatika kuwa kati ya wanasheria wachache Duniani kujiunga na Chuo Kikuu cha Havard kwaajili ya Shahada ya uzamili aliyohitimu kwa ufaulu mkubwa.

UTUMISHI NA UZOEFU SERIKALINI

- Kati ya mwaka 1972 - 1990 alihudumu kama mwanasheria wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

- Kati ya mwaka 1990- 1992 alihudumu kama Naibu Mwanasheria Mkuu (D/AG)

- Kati ya mwaka 1993 -2005 alihudumu kama Mwanasheria mkuu wa serikali.

- Mwaka 2006 alihudumu kama Waziri wa Kwanza wa Ushirikiano wa Afrika mashariki

- Kati ya 2006-2008 alihudumu kama Waziri wa miundombinu katika serikali ya awamu ya nne.

UZOEFU KATIKA BUNGE

- Kati ya mwaka 2005 - 2020 alihudumu kama Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi

- Kati ya mwaka 2008 - 2010 alihudumu kama mjumbe wa kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha.

- Kati ya mwaka 2012-2013 alihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha

- Kati ya mwaka 2013-2015 alihudumu kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti

-Kati ya mwaka 2015- 2020 alihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria na pia kama mmoja wa Wenyeviti 3 wa Bunge.
 
Mambo ya vijisenti yamerudi kama mvua ya mafuriko! Sidhani kweli kama hii nchi hata hiyo 2025 itafika kwa mwendo huu.

Usikute zile trilioni 1.3 za Bi Mikopo, Mzee wa Vijisenti angedai ni vipesa tu vya chenji wala havina athari yoyote kwa taifa.
 
Back
Top Bottom