johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,984
- 142,002
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Isack Sumbali ametoa ombi kwa Vikao vya juu vya maamuzi vya Chama hicho kuanzia Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu kuhakikisha wanatoa fomu moja pekee ya mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pindi wakati mchakato huo utakapofanyika mwaka 2025.
Amezungumza hayo kwenye Mkutano Mkuu wa UVCCM UDSM uliofanyika Abiyani njia panda ya Chuo ambapo pamoja na mambo mengine amesema fomu inayopeneekezwa iwe ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.