Anayebisha kwamba polisi si vibaraka wa CCM asome stori hii ya T. Daima

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wanajamvi: Stori hii nimeipenda kwani tukio la CCM kutaka kuteka sherehe za miaka 50 ya uhuru pale Mnazi Mmoja lilizimwa na vijana wa CDM. Pia inasdhihirisha kwamba polisi daima ni watumishi wa CCM katika ushindani wa kisiasa nchini. Naamini kabisa matukia kama haya yataendelea tu hadi Polisi wajue kwamba wao wanatakiwa wawe neutral kabisa katika siasa.

CHADEMA yateka mkesha wa Uhuru

• Watatu wazimia kwa milipuko ya fataki na Waandishi wetu

SHEREHE za mkesha wa miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja juzi, jijini Dar es Salaam ziliingia dosari baada ya askari kadhaa kutaka kuwakamata watu waliokuwa wakipiga kelele za kukishangilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kundi kubwa la watu wengi wao wakiwa vijana wa rika mbalimbali walishangilia kwa nguvu na kukitaja CHADEMA, kila mlio wa fataki ulipokuwa ukisikika, hali iliyowavutia wananchi wengine kujiunga na kundi hilo.

Kelele za kukishangilia CHADEMA zilidumu zaidi ya robo saa, kiasi cha kuonekana kuwaudhi baadhi ya viongozi wa serikali walioalikwa katika mkesha huo ambao mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Polisi wenye mbwa na wale waliokuwa wamesheheni silaha, walijaribu kulizingira kundi hilo na kulitaka kutokitaja chama hicho, lakini walikumbana na wakati mgumu baada ya kuambiwa wakamnyamazishe kwanza, Kapteni John Komba ambaye alikuwa jukwaani akitumbuiza kwa kuisifia zaidi CCM.

Hatua ya polisi hao ilisababisha kukusanyika kwa watu wengine zaidi, na kuzua zogo kubwa kutoka kwa wananchi, waliodai kuwa wamelazimika kuingiza kibwagizo cha CHADEMA kila ilipopigwa fataki moja, kutokana na kukerwa kwao na tukio la viongozi wa serikali kutaka kuzifanya sherehe hizo zionekane kuwa za Chama Cha Mapinduzi wakati ni suala la Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama.

Kutokana na mshikamano wa wananchi hao, polisi hao walilazimika kubaki kimya na kuacha shangwe za CHADEMA ziendelee hadi ratiba ya kuondoka kwa mgeni rasmi na wageni wengine ilipowadia.

Chanzo: Tanzania Daima
 
muwe mna summarize! Mnaweka madudu marefu hadi yanaboa,kama mtu anataka in details si atafute hiyo source mfano tanzania daima.acha ushabiki wa kisiasa.
 
muwe mna summarize! Mnaweka madudu marefu hadi yanaboa,kama mtu anataka in details si atafute hiyo source mfano tanzania daima.acha ushabiki wa kisiasa.

Pukuza munkari mwanamagamba weee! your days are numbered. Sure they are!

OK - nimeipunguza stori na kubakiza relevant sections! Bado unalo?
 
muwe mna summarize! Mnaweka madudu marefu hadi yanaboa,kama mtu anataka in details si atafute hiyo source mfano tanzania daima.acha ushabiki wa kisiasa.

Mkubwa! Acha kutapika nawewe kihivi maana ni dhahiri kwa namna moja ama nyingine una damu ya ya ufisadi na kama we ni mvivu wa kusoma,ungeacha tu kuipitia thread hii. NA UKWELI ULIPO NI KWMB POLICE TULIONAO NI WATUMISHI WALIOANGUKIA sisiem AMINI USIAMINI KWANI KITU AMBAYO KIKO WAZI.
 
Ingalikuwa Mr II (Sugu) yupo pale naye anatumbuiza na kusifia CDM nadhani dakika hii ninayosema angekuwa Lupango (Central) kungojea Jumatatu kukabiliwa na mashitaka ya uchochezi.

By the way -- kwanza wala asingeruhusiwa kufanya tumbuizo lolote pale!
 
muwe mna summarize! Mnaweka madudu marefu hadi yanaboa,kama mtu anataka in details si atafute hiyo source mfano tanzania daima.acha ushabiki wa kisiasa.

Siyo kila m2 anaweza kuipata hiyo source. Kama ww huwezi kupitia humu sread nzima c acha tu,tupo tunaopitia neno kwa neno na kudigest.
 
muwe mna summarize! Mnaweka madudu marefu hadi yanaboa,kama mtu anataka in details si atafute hiyo source mfano tanzania daima.acha ushabiki wa kisiasa.

Usiwe mvivu wa kusoma! kumbuka vyama vya siasa vina wanachama, wapenzi, wafuasi na wakereketwa, kila kundi linawajibu wake ikiwemo kushabikia! upooo! au na hii ni story ndefu.
 
hongera vijana kwa kubalance sherehe ni ujasiri ambao lazima tuupongeze ili kuwapa moyo na kuwa na taifa linaloweka utaifa kwanza.
 
muwe mna summarize! Mnaweka madudu marefu hadi yanaboa,kama mtu anataka in details si atafute hiyo source mfano tanzania daima.acha ushabiki wa kisiasa.

Tatizo lako magamba yamekujaa hadi kwenye ubongo na macho. No wonder unashindwa kusoma.
 
Taratibu ujumbe unapelekwa kwa magamba - watu hawaogopi tena vitisho na amri za polisi sinazogandamiza haki. Na pia naona polisi nao mikono yao inaanza kuwa na kigugumizi.

Magamba mpo?
 
Kubingwa ni zezeta wa kufikiri. Ndo zetu wasukuma hizo! Tumekalia kuibeba sisiem kama mataahira vile! Hongera vijana kwa kushitukia janja ya magamba!
 
Back
Top Bottom