Ananitia hasira

mnh..usipoteze muda,kwa jitu usilolipenda....
unajinyima chances zako za kuwa na mtu wako ambaye yuko perfect(kama yupo)...

mie naamini hakuna mtu 100 perfect,mwingine atakuja na vitabia vingine..usivyovipenda...sa sijui,utabadilisha wangapi?
 
Mamushaka,,, mi niulize tu kwamba are you that perfect?

kwa mtizamo wangu, umekuwa too judgemental.....na huenda pia too normative...kama ni rafiki yako tu wa kawaida, na sio mpenzi, mbona inakuwa inakuudhi hivyo hizo manners zake? ujue ambacho wewe unakiona kama weakness kwako, kwa mwengine kinaweza kisicount

una mpango wa kumpenda baadaye? kama ndio, mchukulie taratibu....usimwone kama ni too 'barbaric' the way ulivompotray hapa...
Kaizer, Im not perfect
not at all, ndo maana nimesema sorry kama ntaudhi watu kwa kuudhika kwangu, pili nikajihisi natenda dhambi labda kwa kuchukizwa na hayo, tatu sina mpango wa kua mpenzi wake ningekua na mpango nae ningejua jinsi ya kumrekebisha kwakua ningekua na sauti kwake, lakini kwakua ni just a friend ndo maana inaniuma na kumwambia nashindwa.
 
mnh..usipoteze muda,kwa jitu usilolipenda....
unajinyima chances zako za kuwa na mtu wako ambaye yuko perfect(kama yupo)...

mie naamini hakuna mtu 100 perfect,mwingine atakuja na vitabia vingine..usivyovipenda...sa sijui,utabadilisha wangapi?

mmmh, mbona unakuwa mkali hivyo Fab, au na wewe ndo ushatiwa hasira hivyo?
 
Tehe Mamushka umepatikana, nakwambia siku utakayokuja kumpenda huyo jamaa utasahau kila kituuuuu. Hehehe kuna watu walichukiana siku za mwanzo wakapelekana mpaka Polisi lkn sasa hivi wana watoto kadhaa, huwezi jua upepo utabadirika lini hahha,. Mweee vijitabia navyo vinakeraaaa utakuta dada mzuriii lkn haishi kuchokonoa chokoa mapua anatoa kamasi tena na mkono wa kulia ptuuuuuu, au kamasi anavutia mdomoni km makohozi halafu anameza au anatema barabarani ptuuuuuuu. Mwingine mnakula anabeua tu km huyo hata sorry hasemi. mwingine anatoa tongo tongo na mkono wa kulia halafu mko mnakula POP CORN anachota na KONo lake CHAAAAFUU aaaaaaaaaaghrrrrrrr
Uwiii natapika, mh siaskia neno tongotongo siku nyingi, mh my dear ikitokea nikaja kumpenda ntawaoneeni aibu kama mnaniona, lakini siwezi kumpenda aah anavitabia haa haaa.
 
Kaizer, Im not perfect
not at all, ndo maana nimesema sorry kama ntaudhi watu kwa kuudhika kwangu, pili nikajihisi natenda dhambi labda kwa kuchukizwa na hayo, tatu sina mpango wa kua mpenzi wake ningekua na mpango nae ningejua jinsi ya kumrekebisha kwakua ningekua na sauti kwake, lakini kwakua ni just a friend ndo maana inaniuma na kumwambia nashindwa.

Hapo ndo nisipowaamini kabisa nyie viumbe, mara nyingi mkisema NO, basi ndo ujue YES hiyo!!!!!!!!
 
Hapo kwenye RED, najaribu kusoma between herufi, nashindwa kupata connection!hata hivyo, naona kama kuna issue za ujana sana kama sio utoto mwingi kimtindo!Nawasilisha

Yeah ina sound kama utoto kidogo kama hujailewa vizuri, or wewe ni mzee sana labda.
 
Mamushka pole naona una hasira kweli kweli maana hata nukta hujaweka story nzima hadi mwisho. Punguza hasira kidoko mistari iwe na kina , colon, semi colon ,and full stop kwa kiswahili .

Hii inaitwa at-equate .. ni kukosa table mannerism.Inafunzishika kirahisi sana dadangu. BTW Watz wengi hawajui hayo.Unakuta mtu anavuta nyama choma kwa meno kama manati pwaa. halafu mnakula wote.
Hahaaa Mfamaji unanichekesha hee hiyo ya kuvuta nyama kama manati ndo inachekesha, kwa hiyo ukiwa karibu nae hata manundu anaweza kukupa ya uso. Mh huyo hachelewi kukupa ngumi ya mdomo.
Ni rafiki ntamwambia nikishindwa ntapotezea.
 
Mhhhhh pole best kaa nae kwa ukaribu sana uweze kumbadili

Mtu a,badili vipi wakati ashasema hampendi,kiufupi hao watu wapo sana huyo dada ana pepo ambalo alimpendi huyo jamaa lakini yeye binafsi anampenda likimtoka atampenda mpaka watu wenyewe watashangaa.
 
Kama ni kweli unamchukulia kuwa ni rafiki yako, tafuta namna ya "kumstaarabisha" kwa upole. Yaani try to be diplomatic and polite, kwa mfano jaribu kucheua mbele yake halafu mwambie 'excuse me". Kama haelewi, jaribu kumvumilia na kurudia mbinu mbali mbali za kumstaarabisha, ipo siku atajua na ataacha. Hata kunywa chai na kuvuta pumzi kama anapiga mluzi, unaweza kumfundisha akaacha. Be open to him, but in a polite/diplomatic way.

Siku moja nilikuwa nakula na mtu anayegonga kijiko kwenye sahani. Mimi ikawa inani-bore kuona kila anapoingiza kijiko au umma kwenye sahani kuna kamlio kanatoka. Sikuweza kulalamika kwa vile nilikuwa namuogopa, ila nikasema kwa upole, "hizi sahani za udongo zinapiga kelele, afadhali za plastic" Jamaa aliniangalia vibaya, lakini baadaye aliacha hako kamtindo.
Simchukii ila nachuki vitabia tu, kwa sababu ukiacha vitabia hivyo hana shida. Thank you dear will try.
 
Mamushka kama huna mpango wa kuwa mpenzi wake ni kwa nini sasa unaona aibu kumwambia kuhusu izo tabia zake??

N.B mapenzi hayana formula wala maamuzi labda utasema ngoja nimpende huyu sasa awe mylov wangu, Mamushka huyo jamaa leo anaekukasirisha anaweza siku moja akawa ndie anaekupa raha ktk ulimwengu huu
 
Mtu a,badili vipi wakati ashasema hampendi,kiufupi hao watu wapo sana huyo dada ana pepo ambalo alimpendi huyo jamaa lakini yeye binafsi anampenda likimtoka atampenda mpaka watu wenyewe watashangaa.
Ushindwe kwa jina la mungu mi sina pepo, na wala si mchukii na wala sitaki kua nae, sipendi hayo mambo tu.
 
Duh mipango ya mungu hiyo sasa mbona ntakoma.

Iko siku wewe una pepo ambalo halimpendi huyo bwana,lakini wewe binafsi unampenda....likitoka ilo pepo hutakumbuka kama ulikuwa humpendi na mara zote watu wa namna hiyo ndo wapendanao..
 
Mwambie ukweli au tumia lugha kama Nanren alivyosema hapo juu kufikisha ujumbe vinginevyo atazidi kukukera..pole
 
Mamushka kama huna mpango wa kuwa mpenzi wake ni kwa nini sasa unaona aibu kumwambia kuhusu izo tabia zake??

N.B mapenzi hayana formula wala maamuzi labda utasema ngoja nimpende huyu sasa awe mylov wangu, Mamushka huyo jamaa leo anaekukasirisha anaweza siku moja akawa ndie anaekupa raha ktk ulimwengu huu
Sio yeye tu hata angekua mschana pia ningeogopa kumwambia pia, swala la kunipa raha sijui labda kama atakua alishaacha kusema dari.
 
Back
Top Bottom