Ana face Paper Ngumu sana..

Meona eeh? Mshkaji ni full kimeo, hajui anataka nini! Ka simu mbovu mara awake mara azimike, mradi anamkera mtumiaji!
Mnanionea jaman,mie ile issue ya X na Y nshaimaliza tayar wa ndugu
 
Songíto;2783775 said:
mapenzi ya siku hizi bwana... watu hawaogopi kucheza na feelings za wenzao!! sasa anaomba ushauri upi hapo mana sijaelewa...
naomba nikuambia mkubwa..kama ni wewe au kama ni kweli ni kwa ajili ya rafikiyako, inaonekana ndo tabia yake/yako hiyo, hakika nakuambia hakuna wana JF watakalomshauri akabadilika...huyo jamaa ni player na atabaki kuwa player!! Tu mwambie aendelee na mkakati wake wa kuharibu mipango ya ndoa yake ijayo kwa kuendelea kula pote pote.

katika maisha kaka feelings za mwenziwako usicheze nazo kabisa...sasa unasema R anajua kuhusu Q, nakuambia R ataingia kwenye ndoa kwa kuwa ana shida ya kuolewa kwa wakati huu...ila jua katika maisha yote ya ndoa, huyo R wako hatakuja kukuamini kwa kila utachofanya...nakutabiria huko mbeleni hutakuwa na amani katika ndoa kwa ajili ya hiyo mbegu ovu iliyopandwa sasa... Ingekuwa bora sana kuoa msichana mwingine tofauti na hao wawili kuliko huyo R au Q ambao wote wanajua maovu yako...watatumia madhaifu yako ya sasa kukuhukumu miaka ya mbele ijayo maana taswira za udanganyifu katika mapenzi sio rahisi kufutika na ikifutika inachukua mda mrefu sana mpaka kuisha na hii ni baada ya kazi kubwa ya ziada kuthibitisha umebadilika kweli, kazi ambayo sio rahisi.....

Huko mbele nakuambia huyo R hatakuamini hata chembe linapokuja suala la wanawake na atatumia uovu wako wa sasa kukusimanga kila wakati utakapomkosea hasa suala linalohusiana na wanawake...ndoa yako haitakuwa na amani na utakuja kujuta kwa nn ulimwoa..

JF ipo na wana JF tupo, utakuja kutupa ushuhuda kwa hili nililotabiri

nawasilisha

Ahsante Mkuu, nimesha mfowadia Hii Kitu tayar
 
Back
Top Bottom