Amenisomesha, kaninunulia gari lakini sina mapenzi naye

MKINDE

Member
Aug 16, 2012
43
45
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 naishi Tabata Jijini Dar es salaam, nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.

Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.

Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzangu.

Ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo sio mshamba kama huyu wa zamani.

Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake.
 
jamani jamani jamani! hii mada inasikitisha sijui kama ni kweli, sharo vs mshamba kwa kweli masikini akipata maungo hulia mbwata, ngoja waje maana mimi naona kama nitakutukana buree, jamani saidia hii dada maana sharo kamzuzua vibaya.
 
Hapa ndiyo roho inauma saana... Siyo mwanaume but naweza pata picha ya maumivu, dissapointment na kukata tamaa kutakako kuja kwa huyo kaka. Roho imeniuma kana kwamba ni kaka yangu ama ndugu yangu anamfanyia hivyo. Na roho inaniuma zaidi kuwa umewaharibia wanawake wengine watakaofuata baada yako kwa huyo kaka.

Huna hata mshipa wa haya... Unadiriki kusema kuwa unaona hamuendani sababu hana elimu. MKINDE dear, hivi unaweza niambia kuwa elimu inahusiana vipi na mahusiano yenu? Kwamba ushakuwa wa juu sana sababu una elimu na yeye kawa chini ya kiwango kwako? Ni kitu gani unataka? Unataka muwe mnafanya discussions za vitu vya darasani mnapokuwa pamoja?

Naamini kabisa kuwa mapenzi hayalazimishwi! Lakini tafadhali mpe huyo kaka/baba heshima yake anayostahili kwa kumthamini, kumueshimu kiasi kwamba hata ukitaka kutengana naye weka dharau yako pembeni na ueleze juu ya hisia zako zilizo hasi juu yake lakini usianze sababu za kitoto!

Hata hivyo nakusihi, kwa age hiyo unaona huyu hafai sababu siku zote ulikuwa nae na yawezekana hujapata heka heka ya wanaume jeuri! In the dating world hakuna jipya huko, na inawezekana ukafika wakati huko mbele ukajuta na ukatamani ni kheri ungebaki huko huko.

Sad. Nina msemo... Usipotaka kujifunza toka kwa wenzio, utajifunzak wako mwenyewe (The hard way).
 
Last edited by a moderator:
MKINDE naomba nikuulize kwa msisistizo ''ARE YOU SERIOUS ON WHAT YOU ARE SAYING?''au unajoke?Yaani mtu aliyekutoa kwanye shida akakufanya uonekane mtu leo hii ndio umemuona mshamba??????aisee nimeelewa kwa nini wanaume wengi siku hizi hawataki kuwasomesha kabisa wapenzi wao.


Em tutue kiodogo halafu irudishe aliki yako hiyo miaka kadhaa ya nyuma iliyopita mara baada ya wazazi kufa ujikumbuke ulikuwa na hali gani na sasa ukoje?nadhani kutakuwa na utofauti na sasa,jiulize kwa nini kipindi kile ulikuwa tofauti na sasa na jiulize nani aliyeleta huo utofauti wako?bila shaka ni huyohuyo uneayemwona mshamba kwa sasa mabaye kwa kipindi chako cha dhiki nina imani ulimwona kama mkombozi wako na bonge la mwanaume.

Inaonekana hapa wewe ndio mshamba na wala elimu yako haikusaidii kwani unaparamia tu watu bila kuwajua vizuri,hivi we unajua tabia za masharo au unazisikia tu?kwa taarifa yako masharo sio waoaji a.k.a ni maplay boy watu wa viwanja na watu wa totoz kwa sana tu,au we ni mzuri kama Cleopatra na gundi mwilini na atakung'ang'ania wewe tu?wanaume washamba ndio waoaji na watunzaji.

Ulikuwa wapi kuuona ushamba na ukosaji wake wa elimu wakati ule ukiwa na shida,ujinga kichwani, ukauone leo?Na bila huyo umwonaye mshamba leo hii wewe ungekuwa msomi au ungeishia kuwa nani labda?leo ndio umejua kuna freemason baada ya kujua kujipaka vimake up na kumechisha sio eehh,kweli waliosema fadhila mfadhili mbuzi hawakukosea na hata sielewi unapata wapi nguvu za kuja kuomba ushauri wa kufanya roho mbaya kiasi hicho kwa hiyo unataka wana jf wakupe ruhusa ya kuutenda ufuksa wako au????????

I hope it's just a joke au unajaribu kutusimulia ndoto uliyoiota usiku huu!!!!!!!!!!!!!

Daaahh in this world wonders shall never end mkuu Tamatheo naomba uje pande hizi uone watu tunavyojua kuumizana ndani ya huu mviringo wa dunia.
 
Kha! Kaka huku mna kazi jamani... mtu kama huyu kwenye kichwa chake sijui kuna nini aisee.. Ila Inteligencia yangu inaniambia kabuni story
MKINDE naomba nikuulize kwa msisistizo ''ARE YOU SERIOUS ON WHAT YOU ARE SAYING?''au unajoke?Yaani mtu aliyekutoa kwanye shida akakufanya uonekane mtu leo hii ndio umemuona mshamba??????aisee nimeelewa kwa nini wanaume wengi siku hizi hawataki kuwasomesha kabisa wapenzi wao.
 
aise mdogo wangu hebu tuliza akili

hivi kama sio huyo mshamba kukusomesha ungemjua huyo sharo wako?

hebu muogope Mungu, na ukumbuke fadhila, usimuache huyo mwanaume aliyekusomesha please
nyie ndio mnasababishaga hadi wanaume wanaogopa kutusaidia wanawake sbb ya tabia zetu
tena fanya haraka mfunge ndoa na huyo mshamba wako usichelewe mana ukiwa chuo waweza olewa
hivo vistobe vitakupotezea muda tu
na ukimuacha huyo mshamba aliyekusomesha na kuksaidia kila kitu naaaaapa kwa jina la Mungu hutaolewa na hata ukiolewa hutadumu na hata ukidumu hutazaa....yaaaaaaaani ilimradi Mungu atakuchapa kibao tu
 
Ama kweli sasa ndio nimeamini ule usemi usemao "Bora umfadhili mbuzi akikuudhi utamchinja ule, kuliko binadamu". Yaani mambo yote aliyokutendea malipo yake ndio hayo? Leo amekuwa mshamba? Eti hana elimu? Wewe hiyo elimu ungeipata kama sio huyo mshamba asiye na elimu? Muogope mungu binti.
 
Kuna yule mwingine alisomeshwa na fundi viatu hadi Versity pia naye alimpiga chini....

Ila huwa nasympathise na hao wadada.....

Kwa mwanamke mwenye madegree yake kuishi na mwanamume ambaye hana gamba, ni sawa na kujifungia kwenye public garden ili kila mwenye shida ambake kwa muda wake....

Babu DC!!
 
MKINDE unanifurahisha sana badala ya kunisikitisha maana najua siku si nyingi utabaki kujutia upuuzi unaoufanya,lakini sishangai haya toka kwako kwani unaonekana ni mtu ambaye kichwani hamna kitu kuhusu maisha hata kama elimu unayo.
Mtu anayekusaidia leo unamwita freemason?Huyo Sharobalo wako atakufikisha wapi zaidi ya kukumega kila siku huku ukimgharamia kwa kila kitu?
Yaani umeniharibia siku yangu na ulaaniwe.
 
Asante dogo yaani we acha tu mambo mengine yanakera banah,na naomba iwe stori kweli ila kama sivyo namhurumia sana huyo mkaka wa watu,na huyo mdada atakuwa kapungukiwa akili maanake mwenye akili zake timamu hawezi kijivunia ubwege kama huo na kuuanika hadharani hivi akitegemea sijui watu wamsifie au sijui wampongeze????,aaaaaggggrrrrr dogo it's disgusting aiseee.
Kha! Kaka huku mna kazi jamani... mtu kama huyu kwenye kichwa chake sijui kuna nini aisee.. Ila Inteligencia yangu inaniambia kabuni story
 
aise mdogo wangu hebu tuliza akili

hivi kama sio huyo mshamba kukusomesha ungemjua huyo sharo wako?

hebu muogope Mungu, na ukumbuke fadhila, usimuache huyo mwanaume aliyekusomesha please
nyie ndio mnasababishaga hadi wanaume wanaogopa kutusaidia wanawake sbb ya tabia zetu
tena fanya haraka mfunge ndoa na huyo mshamba wako usichelewe mana ukiwa chuo waweza olewa
hivo vistobe vitakupotezea muda tu
na ukimuacha huyo mshamba aliyekusomesha na kuksaidia kila kitu naaaaapa kwa jina la Mungu hutaolewa na hata ukiolewa hutadumu na hata ukidumu hutazaa....yaaaaaaaani ilimradi Mungu atakuchapa kibao tu
Daaaaaahh kamusi ujue hapa nipo nacheka kama vile mazuri!!!!sio mazuri ila umenishekeshaje khaaa sio laana hiyo!!!!Ila sio sri banah inaumzia aisee mtu unajikuta unaongea hta bila kujitambua kwa sababu ya hasira.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom